Nyumbani kwetu ni ndani ya Mungu |

Nyumbani kwetu ni ndani ya Mungu

Vipande Kutoka kozi ya uungu na mkusanyiko wa jumla ambazo zimeandikwa na Mary Baker Eddy


Nyumbani kwetu ni ndani ya Mungu,ndani ya ufahamu wa kiroho, usawa wa milele wa Roho. Muumbaji na mtengenezanji wa hii nyumba ni Mungu. Imejengwa na iko imara milele. Hakuna kitu kinachoweza kuharibu usawa wa nyumbani kwetu. Mungu ameijaza na utukufu wa ufalme wake. Hakuna hofu ya dhambi, magonjwa na kifo inayoweza kuingia nyumba hii; hakuna hisia ya umaskini ama hitaji. Hakuna upungufu wa ugavi unakuwepo hapa. Hizi ni ndoto. hakuna kitu ila mvuto mbaya wa kinyama – dhambi,imani kwa nguvu kando na Mungu. Haziwezitupata kwa sababu tunaishi mahali fiche ndani ya aliye juu zaidi, Mungu, na tuko na ufahamu wa milele wa utajiri usio na mwisho na wingi wa upendo.

Mungu ni ugavi wetu , na hauwezi isha. Uongo unaobishana na ya kuwa umaskini hautujui sisi. Hatuujui, hatuwezi uona, ogopa, sikia, ama kuudhihirisha, kwasababu tunaishi ndani ya Mungu. Ni Mungu anayetawala nyumbani mwetu. Ukweli umejaa nyumbani mwetu, umetambulikana, unapokelewa na kutafutwa.

Hakuna upinzani, hakuna kukataliwa, hakuna ubaguzi. Upendo huangamiza chochote kilicho kinyume – na hutoa kila kitu ambacho ni kibaya.

Ufahamu wa nyumbani iliyo kamilika ya kiroho utafanya nyumba yetu ya sasa kuwa bora.