Wapende Adui Zenu |

Wapende Adui Zenu


KUTOKA mkusanyiko wa maandiko ILIYOANDIKWA NA MARY BAKER EDDY Ni nani adui yako ndiyo umpende? Ni kiumbe ama kitu nje ya uumbaji wako mwenyewe?

Unaweza ona adui, ila kwanza umtengeneze huyu adui alafu uangalie kipande cha maono yako mwenyewe? Ni nini kinachokuumiza? Je urefu na kina ama kiumbe kingine chochote kinaweza kukutenganisha na upendo ambao ni heri ambayo ipo kila mahali, – ambayo inabariki wote bila kipimo?

Kwa urahisi hesabu adui yako kuwa kile kinachodhalilisha, kinachoharibu, na kung’oa taswira ya Kristo ambayo unatakiwa kuangaza. Chochote kinachosafisha, takasa na kuweka wakfu, uhai wa binadamu, sio adui hata tukipata dhiki kwenye mchakato huo. Shakespeare anaandika ; ” matumizi ya kipingamizi ni tamu.” Yesu alisema: ” Heri ni nyinyi watakapowashutumu, na kuwaudhi na kuwanenea kila neno mbaya kwa uongo juu yangu….kwa maana ndiyo waliowaudhi manabii waliokua kabla yenu.”

Sheria ya Kiebrania pamoja na “Usifanye” yake, madai yake na hukumu yanaweza tu timizwa kwa baraka za injili. Alafu, “Kubarikiwa ni nyinyi.” kama vile ufahamu wa wema, neema, na amani zaja kupitia dhiki, ikieleweka sahihi,kama ilivyo takaswa na usafishaji inayoleta kwa mwili, -kujivuna, kujidhalilisha ,mapenzi binafsi, upendo wa nafsi, kujitetea. Ni tamu kwa ukweli matumizi haya ya fimbo yake! Je, nikusema kuwa mchungaji wa Israeli anaongoza kondoo wake kwa fimbo yake hadi wanaingia kwa zizi lake; akiwahesabu, na kuwa kimbilio kutokana na mambo ya dunia.

“Wapende adui zenu ” ina maana sawa na ” hauna adui” Hitimisho hii iko wapi kwa wale wamekuchukia bila sababu?

Kwa urahisi ni kwamba wale watu ndio marafiki wako wa dhati. Kimsingi na hatimaye, wao ndio wanakufanyia wema mbali na hisia za sasa ambazo haziwezi karibisha wema. Wale tunaoita marafiki huonekana wakitia sukari kikombe chamaisha na kuijaza na nektari ya miungu. Tunainua hiki kikombe kwa midomo yetu ; lakini inateleza kutoka kwa mikono yetu na kuanguka na kuvunjika kwa vipande mbele ya macho yetu. Labda , baada ya kufyonza divai yake, tunakuwa walevi; wachovu, vitu vimejaa ndoto za kujitosheleza; ilhali, yaliyomo katika kikombe hiki cha ubinafsi wa binadamu wa kujiburudisha, baada ya kupoteza ladha yake, kwa hiari tunaiweka kando kama kisicho na ladha na isiyofaa kwa malengo ya binadamu.

Na kwa hivyo tunarefusha kushindwa kwetu kufurahia hisia hii inayopita kwa haraka, na ladha yake tamu ya urafiki ambapo wanadamu wanaelimishwa kwa kufurahishwa na raha ya kibinafsi na kufundishwa kwa amani iliyo hatari? Kwa sababu ndio hatari kubwa na pekee kwa njia iendapo juu. Hisia ya uongo ya kile kinachounda furaha ina hatari zaidi kwa maendeleo ya binadamu kuliko yale yote adui ama uadui unaweza ingilia kwenye akili ama kuingiza katika .malengo yake na mafanikio ambapo inazuia furaha ya maisha na kuzidisha majonzi yake.

Hatuna adui. Chochote wivu, chuki, kulipiza kisasi – mikoa isiyo na huruma ambayo inatawala akili ya mwanadamu -chochote inajaribu kufanya ” itafanya kazi kwa wema kwa wale wanaompenda Mungu.”

Kwa nini?

Kwa sababu amewaita wale wake, akawapa silaha, akawapa vifaa, na akawapa ulinzi ambao hauwezi penyeka. Mungu wao hatawaachilia wapotee; na wakianguka watainuka tena, wakiwa na nguvu zaidi ya kabla kuteleza. Walio wazuri hawawezimpoteza Mungu wao, usaidizi wao wakati wa shida. Wakikosea amri ya Kimungu, watapata ahueni, watarejelea amri, kurudia hatua zao, na kurejesha amri yake wakiwa na uhakika wa kuendelea kwa usalama. Somo lao bora la maisha linapatikana kwa kupishana upanga na majaribu, hofu na shida za uovu; kwa kiwango ambacho wamejaribu nguvu zao na kubaini; kwa kiwango ambacho wamepata nguvu zao kufanywa kamili katika udhaifu, na hofu yao inajichoma.

Maangamizi haya ni kemikalishaji ya maadili, ambapo mambo ya zamani yamepita na mambo yote kufanyiwa upya. Mwelekeo wa dunia na kimwili wa mapenzi na shughuli ya kibinadamu zinateketezwa; na huu ndio mwanzo wa kuhamazishwa kiroho. Bingu zinashuka duniani na wanadamu hatimaye wanajifunza somo ya kwamba, “sina maadui.”

Hata kwa imani, uko tu na adui mmoja na huyu adui ni wewe mwenyewe – imani mbaya ya kwamba una adui; ya kwamba uovu ni halisi; Ila wema unapatikana kwenye Sayansi. Hivi karibuni au baadaye adui yako ataamka kutoka kwa kudanganyika kwake na kuteseka kwa nia yake mbaya; kugundua ya kwamba, ingawa wamezuiliwa kufanya uovu, adhabu yake ni mara kumi.

Upendo ni kutimiza sheria: ni neema, rehema na haki. Nilikuwa nafikiria imetosha kutii sheria za jimbo; ya kwamba mtu angelenga mpira moja kwa moja kwa moyo wangu, na mimi kwa kupiga risasi kwanza ningeweza kumuua na niokoe maisha yangu, ya kwamba hii ingekuwa sawa. Pia nilifikiria, kama ningefundisha wanafunzi maskini bila malipo,na baadaywe kuwasaidia kifedha, na si kusitisha kuwafundisha wale wapotovu hata baada ya mwisho wa kipindi, lakini niliwafuata kanuni kwa kanuni; kuwa maagizo yangu iliwaponya na kuwaonyesha njia sahihi ya wokovu, – Nilikuwa nimefanyawajibu wangu kwa wanafunzi.

Upendo haukubali haki ya kibinadamu, lakini rehema ya Mungu. Ikiwa maisha ya mtu ilishambuliwa , na angeiokoa kulingana na sheria za kawaida, kwa kuchukua maisha ya mwingine, je angekubali kupatiana maisha yake mwenyewe? Lazima tuwapende adui zetu kwa dhihirisho zote kama vile tunawapenda marafiki zetu; na ni lazima tujaribu tusifichue makosa yao, lakini tuwatendee wema kila wakati nafasi inapopatikana. Kutoa adhabu tukitumia haki ya kibinadamu kwa wale wanaotusaliti na wanaotutumia kwa dhihaka sio kuacha malipo yote kwa Mungu na kurudisha baraka kwa laana. Nafasi maalum ya kufanya wema kwa maadui wako isipopatikana, mtu anaweza kuwajumuisha kwa juhudi za jumla za kufaidi wanadamu. Kwa sababu naweza tenda mambo mazuri kwa jumla kwa wale wanaonichukia, nikifanya kwa uangalifu maalum na kwa dhati – kwa sababu hawaniruhusu kwa njia yoyote ingine, ingawa kwa machozi nimejitahidi kuipata. Wakati nimepigwa kwenye shavu moja, nimegeuza upande mwingine: Niko na upande mbili kwa sasa.

Ningependa kuwashika mkono wote ambao wasionipenda, na kuwaambia, ” Nakupenda na siwezi kukuumiza kwa makusudi.” Kwa sababu na hisi nikiambia wengine; Usimchukie mtu yeyote; kwa sababu chuki ni pigo ambalo linaeneza virusi viake na hatimaye kuua. Ikichukuliwa kwa uzito, inatutawala; inaleta mateso juu ya mateso kwa mmiliki kwa wakati wote na hata baada ya kaburi. Kama umetendewa ubaya, samehe na usahau: Mungu atalipisha ubaya huu na kuwaadhibu , kwa ukali zaidi kuliko vile ungemwadhibu aliye jitahidi kukuumiza. Usirudishe uovu kwa uovu; Juu ya yote usidhanie umekosewa ilhali hujakosewa. Wakati wa sasa ni wetu; mda ujao, mkubwa na matukio. Kila mwanamume na mwanamke leo anatakiwa awe sheria kwake mwenyewe, – sheria ya uaminifu kwa mahubiri juu ya mlima ya Yesu. Njia za kufanya dhambi isiyoonekana na isiyo na adhabu zimeongezeka ya kwamba kama mtu sio mwangalifu na imara kwenye upendo, majaribu ya dhambi inaongezeka mara mia. Akili ya mwanadamu kwa kipindi hiki inafanya kazi ikiwa kimya kwa maslahi ya wema na uovu kwa njia isiyoeleweka; hivyo kuna haja ya kukesha, na hatari ya kujiachilia kwa majaribu kutokana na sababu ambazo mbeleni katika historia ya binadamu hazikuwapo. Kitendo na adhari za ijulikanayo kama akili ya binadamu kwa mjadala wake kimya, bado hazijagunduliwa na kushughulikiwa kwa haraka na haki ya Kimungu.

Katika Sayansi ya Kikristo, sheria ya upendo inafurahisha moyo; na upendo ni uhai na ukweli. Chochote kinachodhihirisha kinyume kwa adhari juu ya mwanadamu kwa dhahiri sio upendo. Tunatakiwa kupima upendo wetu kwa Mungu kupitia kumpenda binadamu; na hisia za Sayansi zitapimwa kwa utiifu wetu kwa Mungu, – tukitimiza sheria ya upendo, kutenda wema kwa wote; kuhamasisha kama vile tunaangazia , Ukweli, Uhai na Upendo kwa wote ambao wako kwenye duara la mazingira ya mawazo yetu.

Haki ambayo na hisi kwa sasa ikiwa na uwezo ni rehema na hisani kwa wote, – kama vile mmoja na wote wataniruhusu kutekeleza hisia hizi kwao, – nikiwa mwangalifu kujishughulisha na mambo yangu mwenyewe.

Uongo, ukosefu wa shukrani, kosa la kuhukumu na kurudisha uovu kwa wema kwa ukali, -ndiyo, makosa halisi { Kama uovu unaweza kuwa kweli} Yale ambayo nimestahimili mikononi ya wengine – imenifanya kwa furaha sheria ya kuwapenda adui zangu.Hii sheria nawaomba sasa kwa kuzingatia kwa maakini kwa Wanasayansi wa Kikristo.Yesu alisema, ” Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Kwa sababu wenye dhabi hufanya hivyo.”