Uwepo mara mbili wa Roho wako |

Uwepo mara mbili wa Roho wako

Kutoka kwa toleo la Aprili 1911 la jarida la Sayansi ya Kikristo

iliyoandikwa na Ada C. Best


Katika sura ya pili ya Wafalme wa Pili tunasoma: “Na yakaja kupita, walipofika, Eliya akamwambia Elisha, niulize kile ambacho nitakufanyia, kabla nimechukuliwa kutoka kwako. Na Elisha akasema, nakuomba upako mara mbili wa roho yako uwe juu yangu.” Vifungu ishirini na mbili za kwanza za sura hii zinajumuisha somo la kustajabisha la uaminifu na upendo. Elisha alipokuwa akilima kwa shamba la babake alimtambua Eliya kama nabii wa Ukweli na kumfuata na kumhudumia, kwa hivyo tunampata akitajwa kama mfuasi mwaminifu wa Eliya.Somo la maakini la sura hii laonyesha mwanafunzi ya kwamba hakuna wakati wowote Elisha alithubutu kuchelewa, lakini alikuwa tayari kwa wakati wowote kufuata kwenye njia iliyoelekezwa na Ukweli kwa Eliya. Wala hakujaribiwa kuvunjwa moyo wakati katika kila mji aliulizwa na wana wa nabii, “Unajua Bwana atamchukua bwana wako kutoka kwako?” kwa sababu alikuwa anaangalia zaidi juu ya hisia za kimwili na angejibu “Ndio najua; kuweni na amani.”

Hivyo ikaja kupita wakati Eliya alimwambia , “Nikufanyie nini kabla nichukuliwe kutoka kwako,” Elisha alikuwa tayari kuuliza ufahamu zaidi wa ukweli ambao uliwezesha Eliya kuponya wagonjwa, kufufua wafu, na kutawanya maji ndio waweze kutembea kwa nchi kavu. Kwa kujibu ombi hili, Eliya alijibu na kusema, “Umeuliza jambo ngumu: Hata hivyo, ukiniona nikichukuliwa kutoka kwako, itakuwa vile utakavyo juu yako.” Kwa maneno mengine , kama Elisha angeweza kuona ukweli juu ya kanuni na kutambua mwanadamu wa Mungu kama yule hajawai zaliwa na ambaye hawezi kufa” {Sayansi na afya, ukurasa 258}, angepokea upako mara mbili wa roho na ombi hili lingejibiwa.

Natufuate manabii hawa kufikia mahali “ upendo ulio kamilika unaangamiza hofu” na mwanadamu kama mfano wa Mungu anafumbuliwa. Maji ya mto Jorodani yametawanywa na hawa watu wawili wanaomcha na kumpenda Mungu wamevuka kupitia nchi kavu. Wanaendelea na safari yao bila kuongea juu ya tashwishi juu ya upendo na wema wa Baba, juu ya maisha ambayo haijui kifo. Ghafla kukatokea gari la vita na farasi wenye moto na wakatengeneza njia, na Eliya akabebwa na upepo mbinguni. “Na Elisha akaona, na akalia, Baba yangu, Baba yangu, gari la vita la Israeli, na waendeshaji.”

Sherehe kuu! Ajabu kubwa! Hakuna wakati hata mmoja wa kuhuzunika – kulikuwa tu na wakati wa kusherehekea. Elisha alikuwa amemtambua Mungu wake kama Mungu wa uhai, sio Mungu wa kifo, na hakukubaliana hata kwa wakati mmoja na ushuhuda wowote wa hisia za utengano. Hapana; alichukua vazi la juu lililoanguka kutoka kwa Eliya, na akarudi akasimama kwenye kando ya mto Yorodani. Akachukua vazi la Eliya na akachapa maji akasema, “ Wapi aliye Bwana Mungu wa Eliya?” Na alipochapa maji, yakagawanyika na Elisha akapita.

Mwandishi hatasahau kisa cha matibabu ya haraka yaliyofuatia kusoma kwa sura hii. Mama Eddy anasema: “ Sayansi ya Kimungu ni kamilifu, na hairuhusu msimamo nusu katika kusoma kanuni na sheria zake – ikiimarisha kwa kudhibitisha.” {Ibid.,p. 274}. Kama Eliya aliamini kwa wakati mmoja angekuwa kwa nafasi moja ya mawazo kama wana wa nabii ambao baadaye walituma wanaume kwenda kumtafuta Eliya. Elisha alienda kazini, kuweka kwenye utendaji yale aliyofundishwa. Alienda katika nguvu za Roho na “Ishara zikimfuata.” Na wakati wana wa nabii walipomuona wakasema, “Roho ya Eliya iko juu ya Elisha.”

Sayansi ya Kikristo inafunza ya kwamba wote wanaweza kudhihirisha ukweli wa haki ya uzao kama mwana wa Mungu. Kiongozi wetu mpendwa amesema, “ Fuata kiongozi wako, kufikia tu vile anavyomfuata Kristo.” {Ujumbe kwa kanisa la kwanza, ukurasa 78}. Njia imeonyeshwa . Inabaki sisi Kutenda. Natuanze masomo ya nakala yetu kwa upako mara mbili ya roho, na kwa vazi la sifa tugawanyishe maji ya akili za kimwili na tuvuke kwenye nchi kavu. Ndipo “wana wa nabii” watatambua nguvu zinazoleta uhai za Roho, na kuja kunyenyekea mbele ya Ukweli katika kukubali “ Mungu Pamoja nasi;” alafu tutasema tukiungana na mshairi