Binadamu anaishi bila kikomo
Kutoka kwa Hotuba za Sayansi ya Kikristo na PETER V. ROSS
Binadamu hana lingine ila kuishi bila kikomo, kwa sababu ametengenezwa kwa vipengele visivyoharibika. Angalia ndani yako; angalia ndani ya ufahamu.Unapata nini? Uaminifu, kusudi, azimio na wingi wa sifa za kiroho. Chukua moja wapo – uaminifu kwa mfano. Uaminifu unaweza kuwa na mgongano? Unaweza kuwa na gesi, au kuvimba au kuzimwa? Kuna uwezekano sifa yoyote ya kiroho kupata ajali au uchungu? Inaweza pata tajiriba ya kuzaliwa, kuoza, kuvunjwa? La kamwe. Kisha mwanadamu, kama wingi wa sifa za kiroho, hawezi teseka au kupata tajiriba ya hali kama zile.
Kwa nini tusishikilie ukweli huu Dhahiri na kukataa ufahamu wa uongo wa magonjwa, ajali, uzazi wa kimwili, umri, na uangamizo? Binadamu wa kiroho, na hakuna mwingine, hajaanguka; hawezi anguka akiwa na mikono ya milele ya Kanuni chini yake. Nafsi yako halisi haijaondoka mbinguni Kwenda duniani. Sio zaidi ya ndoto ya kwamba umezaliwa katika ufalme wa hatari na uharibifu.
Moja ya hatua za kwanza za kushinda imani ya kifo, ni kushinda imani ya uzazi wa kimwili. Mradi tu mtu anakaribisha imani ya kwamba amealikwa katika bonde la machozi, itakuwa vigumu kuwa na matumaini ya kutolewa huko. Kwa kweli, mtu anaweza tarajia kwa uhaba kupata kinga ya kudumu kutoka kwa magonjwa na ajali, mradi akiendelea kujiingiza kwa dhana ya kwamba ameingia na kukaa kwa dunia isiyo na sheria na maambukizi.
Wakati Yesu anatangaza, “Nilikuja kutoka kwa Baba na nimekuja duniani; tena naacha dunia na ninaenda kwake Baba,” anatangaza ukweli wa kiulimwengu, ambao kila mtu binafsi anatakiwa kuutumia mwenyewe. Haujawai ondoka kutoka kwa makao ya usalama, uwepo wa Mungu; nafsi yako ya kweli haijawai. Hivyo ukosefu wa msingi wa hofu.
Wakati unadai kwa ufahamu urithi wa sasa wa mwana wa Mungu, unaanza kuamkia binadamu wa maumbile yake, na mwanadamu wa kimwili mwenye utelezi ambaye hisia za kimwili zinadai anaanza kusambaratika na kufifia. Halafu unaanza kupata ndani yako afya na nguvu na uwezo Mwenyezi amekuazimu. Kama haujaribu kutambua ya kwamba nafsi yako ya kweli kwa wakati wote imeishi na itaishi kwa wakati wote kama mshuhuda wa kuonekana kwa Uhai usio na mwisho na kwa hivyo uzazi na kifo ni waongo, unashindwa kutumia ukweli wa kimsingi wa Ukristo. Kwa maneno mengine, haufanyi utendaji wako au matibabu kama ya kutafuta na yenye mabadiliko kama upasavyo.
Ukitupilia hofu ya magonjwa na kuimarisha ujasiri ni kipengele cha msingi katika uponyaji wa Sayansi ya Kikristo. Uthabiti wa utendaji huu ni dhahiri tukikumbuka mafikira ya kibinadamu na mwili yanahusikana kwa karibu kwa kweli ni kitu kimoja. Kwa hivyo wakati mtu binafsi amejawa na hofu – na hii ndio hali ya kawaida ya wanadamu – kukosa kufanya kitu au kufanya zaidi katika mwili haiepukiki. Wakati, katika mahali pa hisia ya hofu, hisia ya usalama inaimarishwa, mwili utafanya kazi vile unastahili.