Changamoto ya kushinda kukata tamaa |

Changamoto ya kushinda kukata tamaa

iliyoandikwa na PETER V. ROSS


Hatujakosa msaada katika mchanganyiko na mtikisiko wa nyakati hizi. Tuko na uwezo wa kuzima bila kelele na kwa mwisho, mshawasha wenye shauku ambao umejikita kudhalilisha tasnia na serikali, na jamii yenyewe. Waabudu nguvu wanadhani hiki kipindi cha uporaji kimefika. Wanadhani ya kwamba saa imefika ya kuvunja demokracia na ubinadamu. Sauti ya uhalisi inatambua kupotea kwa kijamii, siasa au uhuru wa Uchumi inahatarisha uhuru wa kiroho. Hivyo ni kwamba Mkristo kamwe sio mtulizaji au muafikianaji wakati uhuru upo hatarini. Silaha yetu ni ya aina ya kwamba haya madhara mabaya hayawezi ona au kushughulika nayo. Silaha yetu ni ukweli ya kwamba Kanuni hutawala wakati wote na kila mahali ikifanya nguvu zisizo na maadili zisiwe na athari. “Bwana atawacheka.”

Viongozi walio kazini, katika biashara, katika serikali lazima wasome ya kwamba Mungu huelekeza shughuli za wanadamu. Anatawala pale leo, kama vile amefanya kila wakati, bila kujali Dhahiri,utawala wa ubinafsi, ugomvi na ukandamizaji. “ Huharibu mipango ya wenye jama.” Hakuna serikali ingine ila yake. Mwishowe hii serikali itaonekana kushinda. Uyakinifu wa kimabavu uliopungukiwa na mantiki, lazima uporomoke kwa kuchanganyikiwa na kushindwa inapokabiliwa na nguvu za kawaida na za kiroho za Sayansi ya Kikristo. “ Bwana Mungu mwenye nguvu zote anatawala” sio kupiga kelele. Wala uhakikisho, “ Huharibu mipango ya wenye jama.” Ahadi za Bibilia zinahifadhiwa kwa sababu ni zaidi ya ahadi, ni ukweli usiyoshindwa.

Kila mtu binafsi anatakiwa aombe kwa dhati ya kwamba taifa lake liendelee kwa hekima na haraka katika mzozo. Kila siku anatakiwa kutenga mda kutambua: “ Mungu yuko Katikati yao; hatatingizika.” Haya maombi inapaswa kupanuliwa kwa kusisitiza ya kwamba wanaume na wanawake katika nafasi za majukumu watakuwa na ujasiri na uwezo wa kufanya majukumu yao katika uigizo wa dunia.

Nguvu za uovu hubeba ndani yake zenyewe mbegu za uharibifu wake. Hazina ufahamu. Zinakaribia wazimu. Tunatakiwa kusema na kujua haya mambo, kila mara na kwa matarajio. Ukweli kwa hivyo unapoachiliwa hautarudi bure. Ni neno la Mungu ambalo linakamilisha ambayo lilikuwa limetumwa.