Kufanya Maamuzi Sahihi |

Kufanya Maamuzi Sahihi

Iliyoandikwa na Clara Schrader Streeter


“Maamuzi yako yatakutawala, mwelekeo wowote yatakayochukua.” {S$H} Ukweli wa kauli hii unathibitishwa katika maisha ya kila siku. Kama mwandishi wa mashairi James Russel Lowell ameandika:

Mara nyingi kwa kila mwanadamu na taifa, Waja mda wa kuamua,

Katika vita ya Ukweli na uongo, Kwa upande wa wema au uovu.

Tunaamua vipi nini sahihi? Mtume Yakobo anatupatia jibu la usaidizi kwa swali hili ambapo anasema, “Ikiwepo yeyote wenyu anaye upungufu wa hekima, na aombe kwa Mungu, ambaye anawapa wanadamu wote kwa wingi na hashutumu; na atapata.”

Tukimgeukia Mungu kwa dhati kama chanzo cha hekima na hukumu sahihi, tutapata mashaka na hofu zikipungua, na amani na utulivu zikibadilisha mchanganyiko wa kiakili. Mawazo ya kiroho yanaanza kujaa kwa akili, na tunaona hatua ya kwanza ya kuchukua katika mwelekeo wa kufanya maamuzi sahihi. Hatua zingine huonekana kama tunaendelea. Kama mawazo yamekubaliana na sheria ya Mungu, maamuzi sahihi yatafunguka. ” Hoja kwa kila mmoja kuamua ni , kama ni akili ya mwili au Akili ya Kimungu ndiyo chanzo.” {S&H}

Hakuna hali ambayo ni kubwa au ndogo kuuliza muongozo wa Mungu kwa kufanya maamuzi sahihi.

Katika Sayansi ya Kikristo tunajifunza kwamba mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu, huakisi akili ya Kimungu. Lakini kama mtu amefanya makosa mbaya, au hatua ambayo amepiga haikuwa sahihi, na amekubalisha uovu kuvuruga afya yake, furaha au ufanisi, anahitaji kuuliza hekima ya Mungu kwa dhati, ambaye ” hashutumu.” Wakati mtu amechukua hatua ambayo ilikuwa inakaa bora kwake kwa wakati ule, anatakiwa atambue ya kwamba imempatia mtazamo wazi zaidi wa hali ile ambayo ingawaje hangekuwa nayo. Hapaswi kujihukumu kwa ile makosa, lakini aone mafunzo aliopata kama sehemu ya kutatua shida. Kama anafahamu nguvu dhabiti za hekima ya Kimungu kumwelekeza, kwa furaha ataacha matokeo kwa Mungu.

Wakati, kupitia kutaka kwa dhati na kupuuza haki za wengine, mtu ametenda kosa mbaya, kurudi kwenye hisia ya uadilifu na mapenzi ya undugu inaweza onekana refu na ngumu. Hii inaweza onekana kwa maisha ya Yakobo ambaye kwa kudanganya aliiba haki ya kuzaliwa ya nduguye Esau, na alilazimika kukimbia kutoka nyumbani kwao kwenda katika nchi ya kigeni, ambapo aliishi kwa miaka mingi. Alipotubu yakutosha, Mungu alimwelekeza njiani mwake nyumbani, akamuahidi ulinzi na amani. Yakobo alirudi na familia yake kwa nchi yake, na baada ya mapambano makubwa na nafsi yake, akapatanishwa na nduguye Esau.

Ukweli kwamba maamuzi yetu hututawala, ni dhahiri katika mitindo yote ya maisha. Maamuzi yetu hushawishi afya yetu, amani akilini, na ufanisi, na inaunda msingi wa shughuli zetu. Tunapotafuta hekima ya Kimungu na kutatua shida tumetumia maarifa, hoja na hukumu sahihi, ambao ni urithi wa kila mtoto wa Mungu, tunapaswa kusimama imara na yale yamefunuliwa kwetu, tukijua wema ndio tu unafanya kazi na Akili ya Kimungu ndio chanzo, na matokeo yataleta wema pekee kwetu na kwa wengine wanaohusika.

Katika ” vita ya Ukweli na uongo,” ni Akili ya Kimungu ambayo inaweza ongoza wanadamu na mataifa katika maamuzi makubwa wanayokabiliana nayo. Kutumia ufahamu wa Mungu na kuelewa kwa uwezo wake wa kuponya na kuokoa, kuhusu mgogoro wowote kati ya mataifa, huleta ushawishi wa uponyaji wa Roho ya Kristo kwa tukio na huongoza kwenye ubinadamu wa juu, ubinadamu ambao utaweza kufanya maamuzi kulingana na mpango mkamilifu wa Mungu.