Msaada wa karibu katika shida |

Msaada wa karibu katika shida

Iliyoandikwa Na Duncan Sinclair


Ni uhakikisho wa kina wa utunzaji wa Mungu, na wa nguvu zake za msaada ambazo hupatikana kwenye Zaburi! Zaburi 46 inasema, “Mungu ni kimbilio na nguvu zetu, msaada wa karibu wakati wa shida,” na Zaburi 91 tunasoma, ” Nitasema juu ya Bwana, yeye ni kimbilio na ngome yangu: Mungu wangu; yeye ndiye nitaamini….. Hakuna uovu ambao utakupata, wala balaa yoyote kukaribia makao yako.”

Ni imani gani ndani ya Mungu haya maneno yanaonyesha! Na bado yaliandikwa mda mrefu kabla Yesu kupatiana ujumbe wake wa upendo wa Baba kwa mwanadamu, na bado mda mrefu kabla Sayansi ya Kikristo kupatiana mafunzo yake kuu kwa ulimwengu. Kama wahibrania wa siku hizo za jadi walimuamini Mungu kabisa, ni kiasi gani zaidi kwa wale wanaishi leo,wakiwa na mwangaza mkuu na mwingi zaidi wa kiroho wanao uwezo wa kufanya hivyo!

Sayansi ya Kikristi inaonyesha kila shida inayokabili mwanadamu ni juu ya fikira potofu juu ya Mungu na uumbaji wake. Wengi wa wanadamu wanafikiri vipi leo? Je, si wao huamini kuwa uovu ni kweli, mzuri na wenye nguvu,kama si zaidi ya hayo? Kwa kuamini haya , wanatenda uovu kila wakati,- wakiendelea kufikiria juu yake kwa mawazo yao na wakidhihirisha kwa vitendo vyao. Matokeo ni shida za aina zote ikiwemo magonjwa, huzuni na ukosefu.

Shida zile zinakabidhi mwanadamu kama zitaisha, wanadamu lazima wafikirie kwa njia sahihi; hiyo ni kufikiri mawazo ambayo ni ya haki na mema. Kufanya hivi, Lazima waelewe Mungu, wema ni nini. Mungu lazima ajulikane kama Upendo wa Kimungu, au wema wa milele, na kama Mungu ni Upendo wa milele au wema wa milele, ni nini wajibu wa wale wanaoufahamu ukweli huu mkuu? Lazima wakane uhalisi na nguvu za uovu na kuukanusha kwa aina zote zake! Lazima wabadilishe imani za uovu kwa sifa ambazo ni njema, sifa kama huruma, uaminifu na uthabiti; kwani hizi kwa uhakika zitadhihirika kwa upendo, usafi, hekima na afya.

Wakati wanadamu wanasahau au hawajui kuhusu upendo wa milele wa Mungu ,wanaweza wakati mwingine hisi kama walikuwa wakizidiwa na kile kinachoonekana kuwa upweke wa uhai. Lakini Mungu hakosekani kamwe katika uumbaji wake. Ile katika hisia za mwanadamu inaonekana kuwa saa ya giza, Upendo wa Kimungu uko karibu; kwani moyo wa mwanadamu ni mpokevu kwa ujumbe wake wa uponyaji. ” Kwa upweke wa ufahamu wa mwanadamu,” anaandika Mama Eddy,Upendo wa Kimungu husikia na kujibu wito wa mwanadamu wa usaidizi. Na sauti ya Ukweli hutamka misingi ya Kimungu juu ya uwepo ambao hukomboa wanadamu kutoka kwa mashimo ya ujinga na maovu.” {Mis.}

Mungu ni Upendo; na Mungu ni mwenye nguvu zote. Kristo Yesu kwa uhakika alielewa haya wakati alitangaza, ” Baba yenyu anajua ni vitu gani mnahitaji kabla ya kumuuliza.” Ni kubwa vipi haja ya mwanadamu kujua zaidi upendo wa Baba na kuamini huo upendo, kama vile watoto wadogo hueka imani yao kwa wale wanaowapenda! Juu ya njia hii ya imani na ufahamu wa kiroho inapatikana ukombozi wa dunia yote kutoka katika mizigo yake mizito.