Kukubali Udhihirisho
Kutoka kwa Toleo la Februari 1947 la Jarida la Sayansi ya Kikristo na Margaret Morrison
Msingi wa udhihirisho wote katika Sayansi ya Kikristo ni Ukweli mkuu kwamba Mungu ni Roho na umbaanji wake wote ni wa kiroho, akisi iliyo kamili na iliyokamilika ya uwepo wake. Mary Baker Eddy, mgunduzi na mwanzilishi wa Sayansi ya Kikristo, anafanya haya wazi katika nakala ya Sayansi ya Kikristo, Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko, katika ukurasa wa 259 anaandika, “Ufahamu wa Kikristo wa uwepo wa kisayansi na uponyaji wa kimungu unajumuisha kanuni na wazo kamili, – Mungu aliye kamilika na mwanadamu kamili, – kama msingi wa wazo na dhihirisho.” Kukubali ukamilifu uliopo wakati wote kama msingi wa “mawazo na dhihirisho,” mtu tayari anaona kwamba kazi yake sio kuifanya bora iitwayo kimwili, kuibadilisha, kuvumisha , au kuiongeza. Kazi yake nikugeuka mbali na udanganyifu wa hisia ya nyenzo za kimwili na kupitia ufahamu wa kiroho kuleta kwenye mwangaza ukamilifu usiokatizwa na utendaji wenye uwiano wa Roho.
Yesu Kristo alipeana msingi wa kweli wa udhihirisho wakati alisema, “ Kuweni wakamilifu, kama vile baba yenu aliye mbinguni.” Tusifafanue haya kumaanisha, “ Kukubali kama uwepo wako wa kweli onyesho kamilifu la kanuni iliyokamilika, ambayo ndiyo chanzo cha uwepo wako?’’ Tukikubali ukweli huu kama dhana ya Kimungu na utangazaji wake, mtu yuaja “kwa ujasiri kwenye kiti cha neema” na kupata “ neema ya kumsaidia katika wakati wa hitaji.” Kama mtu amekubali kwa ukamilifu msingi wa kweli wa udhihirisho, hakutakuwa na woga katika kutangaza ukweli, hakuna nafasi, uwili wa mawazo. Mama Eddy anasema katika ukurasa wa 264 wa mkusanyiko wa maandiko: “Umoja ni asili muhimu ya Sayansi ya Kikristo. Kanuni yake ni moja, na kudhihirisha Mungu, inadai umoja wa mawazo na vitendo.
Wakati mwingine tunakutana na ile ambayo inawezaitwa kama “ndio, lakini –“ mwanafunzi wa Sayansi ya Kikristo anafanya kwa wema tangazo la ukweli alafu anafunga mlango kwa ile ambayo anaita udhihirisho ikiwa na “lakini.” Si kwa wakati mwingine mtu husikia tangazo kama hili: “Ndio, najua kwamba upendo ndio ugavi wangu, naya kwamba ipo na kwa wingi – lakini ukweli huu haujadhihirishwa”? Si hii inamaanisha imani katika ugavi wa aina mbili, moja ya kimwili na ingine ya kiroho na ya kwamba bidii inafanyika kutumia moja kudhibiti ingine? Kuweka jicho moja kwa Roho na jicho lingine kwa kimwili, kutazama athari, ni kuwa na mawazo mawili na ni mbali na kudhihirisha Mungu.
Upendo ndio dutu ya uwepo wa binadamu, chanzo na ugavi wa wema wote. Wakati mtu anafahamu haya, na katika maisha yake ya kila siku anaakisi.
Upendo katika mawazo na vitendo, akiikubali kama dutu ya kweli, anadhihirisha dutu. Kuwa umetosheleka kamili na kufurahia bila hofu katika Upendo wa Kimungu inapatianwa kikamilifu – hiki ndicho kilele cha udhihirisho. Vitu vyaongezwa na mahitaji yote ya kibinadamu inakidhiwa kwa utendaji wa ufahamu wa Upendo ulio akisiwa. Usiwai funga mlango kwa “Lakini” kwa vitu vilivyo ongezwa. Kukataa kwa kuelewa kwa kiroho udhihirisho kamili hupoteza uzuri wake ulioongezewa na uwiano katika tajiriba ya kila siku.
Wakati mwingine “ lakini” yaja kwa njia ya mahali na mazingira, na tunasikia kitu kama hichi: “ Ndio, Najua Mungu yupo kila mahali, uwepo wote, na nguvu zote – lakini haijadhihirishwa katika mahali hapa.” Hapa tena “lakini” inakaa kufunga mlango kwa dhihirisho la kweli na kumfungia mtu katika imani ya mahali pasipo ridhisha pa kimwili au watu wasiokubalika au wenye chuki, labda zote mbili. Katika kesi kama ile mtu lazima atangaze ukweli wake wa kiroho kwa ujasiri, bila tashwishi. Na atimize madai ya “umoja wa mawazo na vitendo,”na akubali kama udhihirisho wa mwisho ufahamu wa kiroho wa Mungu aliyekamilika na binadamu aliyekamilika. Kama atafanya haya na atosheke kikamilifu na afurahie katika udhihirisho katika uwepo wa Akili akiimarisha maono moja, kwa kweli ukungu wa kimwili utaondoka na uwepo uliokubalika na ulioakisika na nguvu za Mungu zitafumbuli mahali pale.
“Lakini” ingine ambayo inakaa kufunga mlango ni, “lazima nidhibitishe.” Wakati mwingi mtendaji anatoa tangazo la uponyaji lenye nguvu na umaakini, ila tu anakutana na majibu, “ Ndio, haya yote ni kweli – lakini lazima ni dhibitishe.” Kuna wale hujifungia mbali na utambuzi wa ufalme wa Mungu na hii “Lakini.” Acha ikumbukwe ya kwamba tunadhibitisha ukweli kwa sababu ni ukweli. Sio kweli kwa sababu tumefikiria tumeudhibitisha. Acha mtu akubali kwa hiari yake na kwa moyo wake wote; acha atangaze kwa ujasiri na kwa imani kinyume cha kiroho kuhusu ubandia wa kimwili, bila kusita kwa kiakili wa “lakini” – na atapata ukweli ukijidhihirisha na ukimueka huru. Yesu hakusema, “ Utaujua ukweli – lakini lazima utaudhibitisha.” Ni ukweli ambao unafanya huru, au kudhibitisha. Ni utendaji wake mwenyewe.
Hali ya kujua ukweli ilikuwa ya kuendelea katika neno la Yesu, utiifu wa kuaminika kwa mafundisho yake. Ya kilele ilikuwa ufahamu wa ukweli. Kukaa katika ufahamu wa ukweli, kufurahia ndani mwake, kutosheka naye,kuakisi katika mawazo na vitendo vya kila siku ni tena udhihirisho. Vitu ambavyo vinaongezwa vyaja, lakini vitu vyenyewe sio udhihirisha hasa. Sayansi ya Kikristo inadhihirisha kwanza na kwa kila wakati Akili ya Kristo katika ukamilifu na umoja wake. Katika Akili ile hakuna hitaji, hakuna ukosefu wa ukamilifu, hakuna tamaa isiyotimizwa.
Kama mtu anajua ukweli, kufurahia na furaha isiyo na kifani katika ukweli wa uwepo wa kweli;
Kama yuajijua kama amelishwa kiroho na kupatiwa makao, amehifadhiwa katika utakatifu na uwiano; kama ametosheka kikamilifu na ufananisho wa Upendo, ukijionyesha katika mawazo ya ufahamu na vitendo, ikiwa aminifu kwa Roho, zile ambazo zinaitwa mahitaji ya kibinadamu na uwiano vinaongezwa kwake kama zimejaa, na haviwezi epukika, na kwa kipimo kilichojaa na kumwagika. Hivi vyachukua nafasi yake sahihi katika seheme ya pili ndani ya shauku na mapenzi yake. Kwa kweli zaja kama hazitambulikani, na mtu yuajipata amekua kwa kiwango zaidi juu ya matamanio ya ndani na inayosemekana kama mahitaji ya dharura. “Ameagizwa katika ufalme wa Mbiguni.” Amejua kutii agizo la kiongozi wetu katika ukurasa wa 203 wa Kanisa la kwanza la Kristo, mwanasayansi, na mkusanyiko: “ Omba kwa usahihi na kudhihirisha maombi yako; imba kwa imani.” Natusome “ kuomba kwa usahihi. Natuimbe kwa imani.”