Kushikana |

Kushikana

Kushikana, Umoja, na Uvutio Na JULIA WARNER MICHAEL


Kuna sentensi katika ukurasa 124 wa Sayansi na Afya, ufahamu wa kiroho ambao utaachilia mizigo mingi ya mateso kwa wanadamu, na kutoa nira ya hofu, na kuvunja kamba za sheria za kimwili. Ni kama ifuatayo: “Kushikana, umoja na uvutio ni sifa za Akili. Wanamilikiwa na kanuni ya Kimungu.” Katika Sayansi ya Kikristo tunasoma kwamba nguvu hizi sizo za kimwili, lakini ni za kiroho na za kimungu. Tunavyo sikiza huu ukweli, unatuongoza kwa upole mbali na imani za zamani ya kwamba kushikana, umoja na uvutio ni sifa za kimwili.

Akili ya kimwili imekuwa ndanganyifu kutoka mwanzo. Imedai kwamba uovu uko na nguvu ya kushikamana kwa mwanadamu katika hali nyingi, na kwamba mwanadamu hana nguvu ya kujitenga nao. Imeenda zaidi kuliko hapa kwa kushawishi wanadamu ya kwamba wamevutiwa na uovu na walikuwa wanatamani kutambuliwa nao. Akisikiza huu uongo na kuuamini, mwanadamu wa kimwili amekuwa mtumwa asiyekuwaa na matumaini kwa matatizo ya kimwili, kwa matukio mengi asipate nafuu kutokana nao kwa sababu anaamini hakuna yoyote. Tunasikia maneno haya mara ngapi: Masikini mtu, aliridhi muonjo wa pombe, na hawezi jisaidia. Hatawai shinda shida yake kwa sababu ni ya kuridhi. Ni asili yake kuwa na hasira kali, kwa sababu hawezi jidhibiti.

Alafu kuna mapendekezo yaliyofiche ya kwamba kuna uvutio kwa mtu kwa yale ambayo ni mabaya, mvuto ambao hawezi ukataa; Ila anapokubali mapendekezo haya, lazima atateseka kwa tendo ambalo hakuwa na nguvu ya kulikataa! Hivyo, akili ya kimwili inasisitiza juu ya uongo ya kwamba uovu unashikamana na mwanadamu, na kwamba mwanadamu anavutiwa na uovu.

Habari yote hii ya kimwili ni “uadui dhidi ya Mungu,” Bibilia inatangaza, kwa kuwa Mungu alimpa mwanadamu utawala juu ya dunia yote. Vipi Mama Eddy aliweza kubaini wazi ya kwamba “kushikana, umoja na uvutio ni sifa za Akili.”

Uovu hauna nguvu ya kushikana na binadamu, kwa kuwa kama sifa ya Akili, kushikana ni kwa wema pekee. Furaha, afya, utajiri, heshima, upendo, ukweli, uhai, kiroho, kwa sheria ya Mungu kunashikana milele na mwanadamu, na mwanadamu nao. Mwanadamu sio lazima ang’ang’ane kushikilia au kuwa na hofu ya kuzipoteza sifa zile, kwa sababu zinashikana na uumbaji wote wa Mungu. Hii kwa kweli ni habari ya amani ya mbinguni kwa roho nyingi ambazo zinasumbuka. Na anayepigana na imani ya kwamba tabia ile ya pombe iliyomshikilia babake, na ambayo inamshikilia licha ya yale yote atakayoyafanya, aamke na ajue ya kwamba haina nguvu.

Na aliyeambiwa na matibabu ya kiasili ya kwamba uvimbe umeshikana na mwili wake na kwamba hata kisu hakiwezi tawanya, atapata kufahamu ya kwamba sheria ya upendo wa Kimungu milele unatawanya mawazo ya Mungu kutokana na uovu wote, na mwenye kuteseka anaweza dhibitisha kwa kila saa na siku kutawanywa huku kuwa kweli, na kwamba binadamu katika mfano wa Mungu hawezi kuwa mgonjwa au mwenye dhambi kamwe. Na anayehofia uvutio usemekanao wa uovu kwa mpendwa, akumbuke ya kwamba uovu haumiliki kitu chochote, hata uzuri, kwa kuwa wema unamiliki yote. Roho, wema wa kimungu, yote ambayo ni sahihi na njema, kwa kiasili, daima huvutia mwanadamu, ambaye ni umbo na mfano wake. Anafahamu juu ya uvutio huu, anaujibu na kupata ukuu wake.

Mawazo maovu, kama hofu, tamaa, chuki, wivu, hasira, fitina, shaka, kukata tamaa, kujipenda, kuona hatia, hazina nguvu za kushikana. Haziwezi jishikilia kwa mwanadamu au kushikamana naye, na kujigamba kwake haramu juu ya uwezo kama ule kunanyamazishwa na ufahamu wa ukweli ya kwamba wema pekee umeabatanishwa na ufahamu wa binadamu.

Karne kumi na tisa zilizopita, Yesu Kristo alidhibitisha kwa kikamilifu kutojishikilia kwa uovu. Kwa kuponya mtu mara moja dhidi ya kifafa, mwingine upofu, na mwingine pia kupooza, kwa kumuinua binti wa Jairasi, na Lazaro kutokana na kifo, alidhihirisha umoja wa milele wa mwanadamu na wema na kutawanywa kwa sasa dhidi ya uovu.

Ni haki maalum ya mwanadamu kugundua na kudhibitisha, kupitia ufahamu wa Mungu, ya kwamba uovu wa jina lolote au asili yoyote hauna nguvu ya kushikana naye kama mtu, au jamii, Taifa au kabila. Kwa kiwango ambacho inakuwa safi kama wimbo wa kusifu utainuka kutoka dunia yote. Kwa kuwa Roho wa bwana utaweka huru wote ambao wamefungwa na imani za uongo, wakiendeleza mishikamano ya ukamilifu na amani, ufalme wa Mungu na Kristo wake.