Kutuhusu sisi
Historia ya uhuru wetu
Ikiwa tarehe Februari 23, 1987, mahakama kuu ya New Jersey iliamua kuwa kanisa la Plainsfield liko na haki ya kutumia jina ” Sayansi ya Kikristo.” Uamuzi huu wa kihistoria ulimaliza vita ya kisheria ya miaka kumi na mbili ilioanzishwa na bodi ya wakurugenzi wa Sayansi ya Kikristo dhidi yetu.Kwa sababu ya uamuzi huu, kanisa letu limebadili jina na kuwa Kanisa huru la Sayansi ya Kikriso la Plainsfield.
Udhalilishaji wa kanisa la Plainsfield ulianza mwaka wa 1975 wakati bodi ya wakurugenzi wa Sayansi ya Kikristo, wakifuata mwelekeo wa bodi ya wakurugenzi wa kuingilia shughuli za matawi ya kanisa, waliagiza kubadilishwa kwa bodi ya waaminifu walioheshimika sana wa kanisa la Plainsfield na kuleta bodi mpya ambayo ni tayari kuapa kiapo cha uaminifu kwa wakurugenzi wa Boston. Kwa majibu yaliyo kuwa na mkazo juu ya kuingiliwa kusipokuwa na msingi kwa maswala ya ndani ya kanisa letu, washiriki walikataa maagizo ya Boston wakiashiria kwa wakurugenzi kuwa wao wenyewe walikuwa wamevunja mwongozo wa Kiongozi wetu hasa makala XXIII, sehemu 1 na 10, na makala XI, sehemu 13. kukataa kwa kanisa la Plainsfield kutii maagizo ya wakurugenzi kulifanya kanisa letu kutolewa kwenye orodha ya jarida Juni 16 , 1977. Wakurugenzi pia walitufahamisha kuwa hatukuwa na haki tena ya kutumia jina “Sayansi ya Kikristo” kwa njia yoyote.
Mwakani 1983, miaka tatu baada ya kanisa letu kujiita upya ” Kanisa huru la Sayansi ya Kikristo,” wakurugenzi walitupeleka mahakamani na wakapata amri ya mahakama kutuzuia kutumia jina “Sayansi ya Kikristo” kwa kutambua kanisa letu. Kanisa likaanza kutumia jina, ” Kanisa la jamii la Plainsfield, Kanisa huru linalo utendaji wa Sayansi ya Kikristo” na kufanya rufaa kwa mahakama ya chini dhidi ya uamuzi kwa mahakama ya rufaa ya New Jersey ambayo ilibatilisha amri na kuamuru kwamba jina “Sayansi ya Kikristo” ni neno la jumuia na sio alama ya biashara iliyomilikiwa pekee na bodi ya wakurugenzi. Huu uamuzi ulidumishwa na wengi na kwa nguvu na mahakama kuu ya New Jersey Februari 23 1987. Garama yote ya kesi ya $ 257,000 ililipwa kwa michango kutoka kwa washirika na waunga mkono kila mahali.
Bodi ya wakurugenzi ilikuwa na siku 90 kuomba rufaa ya kesi kwa mahakama kuu ya Marekani. Siku zaidi ya 90 zimepita na kwa hivyo wameacha kipao cha haki milele kwa mahakama kuu ya Merikani kuhusu swala hili. Sasa tumepata haki ya kulitumia jina “Sayansi ya Kikristo” popote tunapochagua. Uamuzi huu wa kisheria kwa kweli ni wa kihiistoria. Inaweka huru kanisa letu kutumia jina ” Sayansi ya Kikristo” na inafungua njia kwa tawi lolote la kanisa – bila uoga wa mashtaka – kudai uhuru wa kuchukua hatua ambao umehakikishiwa na Mama Eddy kwa mwongozo wake nambari 88, toleo la mwisho aliloliidhinisha kiongozi wetu kwa utawala wa makanisa yote ya Sayansi ya Kikristo.
Kutoka tuwe huru, kanisa la Plainsfield limeshuhudia ukuaji na ustawi. Tuko na ushirika mkubwa na unaopanuka ikiwemo washirika wengi kutoka nje ya jimbo na nje ya nchi. Uponyaji ndio moyo wa kanisa la Plainsfield na kazi ya ajabu ya uponyaji imekuwa ikiendelea hapa kwa miaka mingi. Huduma zetu zinapatikana kwenye mtandao, moja kwa moja na za kurekodiwa kwa wale wangependa kuzisikiza. Wageni kila wakati hutoa maoni kwa anga ya upendo na raha wanayoisikia kwa ibada zetu.
Mwakani 1979 kanisa letu lilianza kuandika masomo yetu sisi wenyewe na mwakani 1980 likaanza kuchapisha jarida huru la robo mwaka, ikiwa na msingi wa Bibilia na kitabu chetu cha masomo , Sayansi na Afya kilichoandikwa na Mary Baker Eddy. Haya masomo rahisi yanawafikia kwa nambari kubwa washirika ambao wengi wao huandika kila wakati kushukuru.
Katika Mei 1986 tulianza kuchapisha jarida la kanisa yetu, “Mawazo ya kuponya”. Hivi karibuni tuliona vema kugeuza jina ya jarida ikawa , “Upendo ndio mkombozi” ikiwa na sisitizo ya kuondoa dhana potofu kuhusu Sayansi ya Kikristo inayotokana na shirika la kati. Tumepokea shukran za dhati kutoka duniani kote kutoka kwa watu wanaotamani maandiko ya Sayansi ya Kikristo iliyo safi na ya kuponya.
Mwakani 2008 waumini wa Herbert W. Eustace waliona sawa kutuamini na jukumu ya kuwa wasambazaji wa kipekee wa kitabu bora cha Bwana Eustace, “Sayansi ya Kikristo, Ufundishaji wake sahihi,” na Maandishi Kamili. Hii ilikuwa ni kuaminika pakubwa kwa uaminifu na udhabiti wa kanisa letu. Bwana Eustace alikuwa mmoja wa wafanyi kazi wakubwa wa Sayansi ya Kikristo. Ingawa alikuwa mteule wa waumini wa chama cha kuchapisha hapo mwakani 1912, ni wazi Bwana Eustace ” hakufanya kamwe kusahau ama kutelekeza wajibu wake kwa Mungu, kwa kiongozi wake na kwa binadamu,” ile ambayo ilimfanya kutetea chama cha uchapishaji wakati wa” kesi kubwa.” Ingawa hivi vita vya kisheria vilipotea kimsingi,- na akafukuzwa juu yake – Bwana Eustace alipata uhuru mpya wa kiroho kutoka kwa udhibiti wa kibinadamu kuwa baraka kuu, na ikamwezesha kuponya na kufundisha Sayansi ya Kikristo kwa miaki imezidia 40 kama mwanasayansi ya Kikrito aliye huru.
Kutoka kwa ” Uangalifu kwa wajibu” ilioyoandikwa na Mary Baker Eddy,katika mwongozo wa kanisa wa 88.