Malaika wa ukombozi
Na ALBERT M. CHENEY
Bibilia imejaa simulizi za ajabu juu ya ukombozi wa wanadamu na, katika visa vingi, wanajeshi kutokana na hatari kubwa kwa nguvu za Mungu, ikiongozwa na malaika wake.
Katika matoleo ya awali ya Bibilia, malaika wanaonyeshwa kama wanadamu walio na mabawa. Watu wengi wanaamini ya kwamba malaika wanaishi mahali pa maada panapoitwa mbinguni, ambako kunaweza fikiwa kwanza kwa kupitia tajiriba inayoitwa kifo pekee. Nadharia iliyo na makosa ya kwamba malaika ni viumbe walio na umbo la maada, wakiishi katika makazi ya maada zaidi ya anga, sio ukweli.
Sayansi na Afya inafafanua malaika kama, “ Mawazo ya Mungu yanayopita kwa binadamu; hisia za kiroho, zilizo safi na kamilifu; himisho la wema, usafi, na uhai wa milele, ikikabiliana na uovu wote, hisia za kimwili, na uhai wa milele.” Kufahamu ukweli juu ya malaika kunaleta kuangaziwa kwa wazo, na maelezo ya kimantiki vile malaika wako mahali Mungu yupo, na wanaonyesha nguvu zake zisizo kuwa na mwisho na upendo.
Simulizi lililo na himisho la Danieli kuhusu ulinzi wake katika pango la simba ni mfano dhahiri wa vile malaika wako karibu kusaidia wale wanaomtegemea Mungu. Danieli hakuwa na hofu, na hata kama alilala katika pango la simba, alijibu mamkuzi ya mfalme kwa furaha asubuhi iliyofuata kwa maneno, “ Ewe mfalme, uishi milele.” Na kwa maelezo juu ya ukombozi wake akasema, “ Mungu wangu ametuma malaika wake, na amewafunga midomo yao simba, ya kwamba hawajaniumiza: kwa sababu makosa haijapatikana kwangu; na pia mbele yako, ewe mfalme, sijafanya makosa.”
Sayansi ya Kikristo inafichua upatikanaji wa haraka wa malaika wa Mungu, wema na nguvu ambazo zinatosha kuokoa hatarini, kulinda kutokana na dhambi, kupumzisha kutokana na umasikini, na kuponya ugonjwa na majonzi ya wale wanaokaa kuwa katika hali isiyokuwa na matumaini.
Yesu alidhihirisha kwa kikamilifu ukweli wa uwepo kuliko mtu mwingine yeyote, na kutegemea kwa uthabiti Malaika wa Mungu kumuongoza na kumdumisha kila wakati. Utambuzi wake, na kutegemea malaika wa Mungu inatupa mfano kwa wote ambao ni wafuasi wake.
Tajiriba ya Gideoni ni mfano wa kipekee vile mtu ambaye ni mnyenyekevu, mtiifu, na wa kuaminika anaweza kumkaribisha malaika wa Mungu, na kupokea mwongozo, ulinzi, na ukombozi kutokana na uovu wa kukandamiza katika dhihirisho zake zote. Ingawa Gideoni na genge lake ndogo walikuwa wamezidiwa kwa kiwango na wengine mara nyingi, na mashujaa wake hawakuwa na vifaa vya kivita kama adui, bado, wakitegemea nguvu za Mungu, na maagizo ya malaika wake, Gideoni aliviangamiza kabisa vikosi vyote vya upinzani na kushinda ushindi mkuu. Je, hii ni kweli kwa kiasi gani, ya kwamba yule anaechukua upande wa Mungu, upande wa haki kamili, atajipata kwamba atakuwa upande wa ushindi!
Labda tunaweza sema, nyakati zimebadilika tangu enzi za Gideoni na Yesu. Mungu habadiliki kamwe. Nguvu zake ni zile zile. Mwanadamu, taswira ya Mungu ya kiroho, kwa uhakika ni umbo la Mungu la upendo na ulinzi leo kama alivyokuwa enzi zilizopita. Uhusiano ambao upo kati ya Mungu na binadamu unabaki bila kuvunjwa, hausitishwi, na uko na uwiano. Kupita kwa miaka na kubadilika kwa imani za wanadamu hakuwezi ingilia utendaji wa sheria za upendo wa kimungu.
Manabii, mitume, na wakristo wa awali walikuwa wanajua uwepo wa malaika, na wengi wao walikombolewa kutokana na hatari, kifo, na gereza kupitia ufahamu wa huu ukweli, na utiifu kwa amri walizopewa.
Kama tunavyoendelea na safari, tukiamini Mungu, malaika wa uwepo wake ndio walezi wasiosita katika dhoruba au utulivu. Ingawa tunaweza kuwa katika shimo la hofu na kukata tamaa, na mawingu ya makosa yakikusanyika juu yetu, na makosa ikituambia hakuna njia ya kutorokea, hata hivyo kuna njia wakati wote, inayongoja kukubali kwetu, wazo safi la malaika, ujumbe uliotumwa na Mungu, ambao unaweza kuondoa na kuangamiza hali zilizo na makosa au mawazo ya uongo yenye imani, na kuleta uhuru kamili na uponyaji kamili. Jinsi gani maneno ya mtunzi wa Zaburi huleta kufarijiwa, “ Atawapa Malaika wake umiliki juu yako, kukuhifadhi katika njia zako zote!”
Hatuhitaji kamwe kuwa wasiokuwa na msaada au bila matumaini, kwa sababu malaika wa Mungu wa ukombozi wako karibu. Hawa wajumbe wa kiroho huangazia na husababisha amani na kupumzika. Mama Eddy alisema kwa uwazi usiokuwa na kifani, malaika ni nini, na walimaanisha nini kwake. Anaandika katika Sayansi na Afya: ‘’ Malaika wangu ni mawazo iliyotukuzwa, ikijitokeza kwenye mlango wa kaburi, ambapo imani ya kibinadamu imezika matumaini yake ya thamani duniani. Kwa vidole vyeupe vinaonyesha juu kwenye imani mpya na yenye utukufu, kwenye maadili ya juu zaidi ya maisha na furaha yake.