Maswali na majibu |

Maswali na majibu

Maswali na majibu kuhusu Sayansi ya Kikristo na kanisa hili.


Meza ya maudhui



Ni vipi Mungu mwenye upendo anawezaruhuzu uovu kama huu duniani?

Sayansi ya Ukristo ni nini? Kwa nini mko huru?

Je, sayansi ya dini ni moja na Sayansi ya Kikristo? Unaona aje kupata msaada wa matibabu?

Mbona utumie Sayansi ya Kikristo kwa matibabu wakati sayansi ya matibabu imeendelea sana? Je, si ni ujinga kujifanya wewe si mgonjwa ilhali ushahidi unaonyesha unaugua?

Katika Sayansi ya Kikristo, naweza hisi hatia nikiwa na shida ama nikienda kwa daktari? Ni nini inayotofautisha Sayansi ya Kikristo na mbinu zingine za kiakili?

Kanisa lako linatofautije?

Kuna tofauti gani kati ya toleo la 1910 la Sayansi na afya na funguo za maandiko ya Bibilia lilioandikwa na Mary Baker Eddy na toleo lile lisemekanalo kama la “Iliyoidhinishwa” linalotumika na kanisa la Boston?

Ni vipi Mungu mwenye upendo anawezaruhuzu uovu kama huu duniani?

Swali bora ni, “Ni Mungu wa aina gani anayeweza ruhusu uovu kama huu duniani?” Mungu aliyemkali ama aliyemakosa? Hakika ni Mungu aliyeumbwa na Binadamu. Mary Baker Eddy anatoa majina mengine saba sawa ya Mungu amabayo yanasaidia wazo kuachilia “binadamu mkubwa hewani” dhana potofu: Akili, Kanuni,nafsi, roho, uhai, ukweli na upendo. Haya majina yote yametolewa katika umoja, na hayana mwisho, kama vile Mungu ni mmjoa na hana mwisho.

Kama hivyo hakuna nafasi ya uovu, kama vile hakuna nafasi ya makosa katika kanuni ya hisabati. Je,unweza laumu kanuni kwa makosa? Wakati unaotumika kuuliza kwanini kanuni iliruhusu makosa ni wakati uliopotea. Kadri unavyotumia mda mwingi kujiingiza kwenye makosa badala ya kutumia kanuni kurekebisha, kadri inavyodumu zaidi.Vile tu kama dhambi na magonjwa duniani yanaonekana sio halali,na kinyume na sheria za Mungu, ndio tu tunaweza kuyashinda.



Nini Sayansi ya Kikristo?

Katika maneno ya Mary Baker Eddy, katika kitabu cha masomo ya Sayansi ya Kikristo, Sayansi na afya na unfunguo wa maandiko ya Bibilia tunasoma kwamba: Neno SAYANSI YA KIKRISTO lilianzishwa na mwandishi kuweka alama mfumo wa kisayansi wa uponyaji wa kimungu.

Ufunuo unajumuisha sehemu mbili.

  1. Ugunduzi wa sayansi hii ya Kimungu ya kuponya, kupitia hisia za kiroho za maandiko ya Bibilia, na kupitia mafundisho ya Mufilisi kama alivyoahidiwa na Bwana.
  2. Uthibitisho kupitia kipimo cha sasa, ya kwamba miujiza inayoitwa ya Yesu haikuwa hasa inayohusiana na kipindi kilichopita lakini inaonyesha kanuni inayoendelea kufanya kazi. Ufanyaji kazi wa kanuni hii unaashiria umilele wa utaratibu wa kisayansi na kuendelea kwa uwepo wa Mungu.

Sayansi ya Kikristo Inafundisha tu kile ambacho ni cha kiroho na cha Kiungu na sio cha kibinadamu. Sayansi ya Kikristo haina makosa na ni takatifu; Hisia za kibinadamu zina makosa kwa sababu ni za kibinadamu.

Ingawa inatumika kama hivyo, Sayansi ya Kikristo SIO kikundi cha dini ama sekti pamoja na wafuasi, na sio alama ya biashara ya kanisa la kwanza la Sayansi ya Kikristo Bosto MA.

“Mungu wa Sayansi ya Kikrito ni wa ulimwengu mzima, ni wa milele, upendo wa Kimungu, ambao haubadiliki na hausababishi uovu, magonjwa ama kifo.” Kama vile tunavyoielewa, Sayansi ya Kikristo inajumuisha sheria {za kiroho} za ulimwengu na zinawezafanyishwa kazi na mtu yeyote, mahali popote – kuambatana na mafundisho ya Kristo Yesu aliyempongeza mkaribu wa Kirumi kwa kuwa na imani kuu kuliko watoto wote wa Israeli, na aliye katika metali ya Msamaria mwema alionyesha Msamaria mnyenyekevu kuwa ” mkristo” zaidi kuliko kuhani na mchungaji mwenye kijivuni na kiburi

Mungu hana kipendeleo cha watu” – Matendo



Kwa nini mko huru?

Mama Eddy alitangaza ya kwamba Sayansi ya Kikristo ni ya Kiungu sio ya kibinadamu. Kwa hivyo haiwezi kuwekewa mipaka ya kuwa shirika la kibinadamu. Aliweka zana ya kanisa kama chombo cha uponyaji na sio taaluma. Alitambua kwamba shirika lililo na nguvu za katikati lingekandamiza mzinduko, na kwa hivyo uponyaji. Tumeona hii kuwa kweli. Uhuru wetu umehamasisha nguvu na uhai ambao usingekuwa na uwezekano endapo tungekuwa bado tawi la shirika la Boston.



Je sayansi ya dini ni moja na Sayansi ya Kikristo?

Sayansi katika majina yote mawili ndio uhusiano pekee. Zifuatazo ndizo tofauti zinazodhihirika.

  1. Sayansi ya Kikristo iligunduliwa na Mary Baker Eddy: Sayansi ya dini ilianzishwa baadaye na L. Ron Hubbard.
  2. Mama Eddy alifikia Sayansi ya Kikristo kupitia ufunuo na kuiona ni ya kimungu na sio kibinadamu. Alisema Bibilia ndiyo rejeo lake pekee kwa ufunuo huu; Bwana Hubbard alifikia dianetics, mawazo na mazoea kupitia akili na ufahamu wake mwenyewe: Anadai hana kipimo chochote cha ushawishi wa kidini.
  3. Mama Eddy alisisitiza umuhimu wa wanafunzi kusoma Bibilia pamoja na kitabu cha maandiko cha Sayansi na afya na ufunguo wa maandiko ya Bibilia; Bwana Hubbard hakuweka umuhimu kama huo kwenye Bibilia.
  4. Bi Eddy alishikilia uzazi usio na dosari, maisha, uponyaji,kufundisha,kuteseka na ufufuo wa Kristo Yesu katika heshima kubwa na kwa kina kuadhiri kila kipengele cha uzoefu wa Sayansi ya Kikristo katika adiko na katika roho angalia mahsusi kipengele cha pili cha kitabu ” Kuondoa dhambi na Ekaristi.” Bwana Hubbard? Tunaungama kwa dhati, hatujui, lakini tumeona ushahidi mdogo wa hilo katika mtazamo wa haraka wa tovuti ya sayansi ya dini.



Unaona aje kupata msaada wa matibabu?

Hakuna dhambi zaidi katika kupata msaada wa matibabu kuliko katika kula na kulala! Jambo muhimu ni kuendelea kutambua Mungu kama mkuu kwa lolote tunalolifanya. Tunaamini hasa katika matukio yanayohusiana na watoto kwamba ikiwa kuna tatizo la kimwili na halijapata matokeo ya haraka chini ya matibabu ya Sayansi ya Kikristo, ni vizuri kupata usaidizi kutoka kwa daktari wa matibabu.

Katika matibabu ya Sayansi ya Kikristo, jambo la kwanza ni kutoa hofu, sio kujaribu imani. Mungu wetu ni

Mungu mwenye upendo na hatuachi kamwe bila faraja na hiyo inajumuisha ofisi ya daktari ama dani ya hospitali.



Kwanini kutumia Sayansi ya Kikristo kwa matibabu ilhali sayansi ya matibabu imeendelea sana?

Ona ushuhuda ulio orodheshwa katika tovuti yetu. Uponyanji wa Sayansi ya Kikristo umeleta uponyaji huu licha ya hukumu za “haiponyeki” za sayansi ya matibabu. Sayansi ya Kikristo ina ufanisi zaidi na ni kamilifu kwa sababu haitoi tu dalili za ugonjwa lakini inatoa hofu iliyofichika inayohusikana na shida ile. Uponyanji wa Sayansi ya Kikristo ni ishara ya ” Immanueli ama Mungu pamoja nasi, athari ya Kimungu.” { Sayansi na afya} na kwa hivyo haitatanishi.

Hata hivyo kama utaomba mtu matibabu ya Sayansi ya Kikristo, usidhani kitu chochote. Hakikisha unaweza amini uaminifu wa maadili wa yule unaemuomba. Mama Eddy anaweka wazi kwa nguvu, ” Heri uteseke na daktari aliyeambukizwa na ugonjwa wa ngozi wa koribori akuhudumie badala ya kushughulikiwa kiakili na asiyetii masharti ya sayansi ya Kimungu. {Sayansi na Afya} Hakuna shirika linaloweza kudhibitisha utiifu wa aina hii.



Je, si ni ujinga kujifanya wewe si mgonjwa ilhali ushahidi unaonyesha unaugua?

Ndio, ni ujinga, hata ni hatari kujifanya wewe si mgonjwa ilhali unaugua. Lakini utenda kazi sahihi wa Sayansi ya Kikristo uko mbali sana na kujifanya! Ni kushikilia kanuni isiyobadilika kama vile mwanahisabati hushikilia lile analolijua kama ukweli, mpaka shida inatatuliwa. Mwanahisabati hana hofu ya kukiri hajatatua jedwali, wala Mkristo wa sayansi hatakiwi kuwa na hofu ” kusema ukweli juu ya uongo,” tukisema hivyo.

Mama Eddy alisema, ” Ukisema, mimi ni mgonjwa, unakiri hatia.” Lakini alikuwa anarejelea mapambano ya akili ya mawazo ndani ya mtu mwenyewe sio matumizi halisi katika ulimwengu wa watamazanji, labda bila kujua vile Sayansi ya Kikristo hufanya kazi. Kukataa kwamba jambo liko na makosa kwa roho inayopenda na ambaye anachamia ustawi wako inazindisha hofu na sio sayansi sababu sio upendo.



Katika Sayansi ya Kikristo, naweza hisi hatia nikiwa na tatizo ama nikienda kwa daktari kwa matibabu?

“Kitu cha muhimu, kiini cha Sayansi ya Kikristo ni upendo.” – Sayansi na Afya iliyoandikwa na Mary Baker Eddy.

Upunguzaji wa ubora wa Sayansi ya Kikristo ndio tu waweza kufanya uhisi hatia. Kuhisi hatia ni njia ya nabii wa uongo kuanzisha udhibiti wa mtu binafsi. Mashirika ya kidini hujaribu kudhibiti imani ya watu ndio yaweze kudhibitisha mfumo wao maalum wa imani. Tukiwa na Thomas Jefferson tunatakiwa ” apa juu ya madhehebu ya Mungu uadui wa milele juu ya kila aina ya ukandamizanji wa akili ya mwanadamu.”

Ni makosa kwa mwanasayansi wa Kikristo kuteseka na hatia kwa kumuona daktari ama kwa kutumia dawa ama kwa kuwa na tatizo lingine la aina yoyote. Ni matumizi ya mapenzi ya binadamu yanawezaleta kosa kama hili! Sayansi ya Kikristo SIO mfumo wa imani. Taasisi yoyote ama mtu anayejaribu kuilazimisha juu ya mwingine anachezea sheria za ulimwengu.

“Haki za binadamu zinavunjwa wakati mpangilio wa Mungu unapotatizwa na mshambuliaji wa akili anapata adhabu ya Kiungu kwa uhalifu huu.” Sayansi na Afya



Nini inatofautisha Sayansi ya Kikristo na mbinu zingine za kiakili?

Maduka ya vitabu yamejaa vitabu vya kujisaidia ambavyo vinatumia njia za kiakili kuboresha maisha ya wanaovisoma. Ni dhahiri vinafanya kazi kwa kiwango na kuboresha kujiamini, la si hivyo havingekuwa na umaarufu. Katika maadili sahihi ya Sayansi ya Kikristo hata hivyo, kila onyesho la ufanisi wake linaachia mtu na hisia kubwa zaidi ya Mungu. Ukaribu wake na upendo. Pia inamfanya amfanye Mungu kuwa tegemeo lake na amkaribie zaidi.

Kwa maelezo zaidi, kama unahitaji nafasi ya kuegesha gari katika eneo lililojaa magari, mifumo mingi ya kiakili inapendekeza mbinu za ufahamu na matarajio chanya. Wakati nafasi ya kuegesha gari inapatikana kwa muujiza, unafurahia uwezo wako. Kwa Sayansi ya Kikristo sahihi, unaweza kosoa nia yako, kama iko na ubinafsi ama kimakusudi. Hapo ndio tu unaweza tarajia kwamba, Mungu, anayejua yote, atafungua njia kwako. Mahali pa kuegesha pakipatikana, ni dhihirisho la upendo wake,na kutambua utawala wake, ” Mambo yote hufanya kazi pamoja kwa ajili ya mema kwa wale wanaompenda Mungu.” {Mtume Paulo} Tazama kuwa tukio la hapo awali, unaweza kuwa umepata kile unachokitaka lakini inaweza kuwa sio bora kwako kwa sababu ya hali zisizotarajiwa. Kwa tukio la mwisho, ikiwa Mungu ndiye anatawala, kwa kusema, mahitaji yako yatakidhiwa ikiwa ni bora kwako. Kwa sababu hii, ni njia salama ya uendeshaji, ilhali katika tukio la awali, kwa sababu unapata unachokitaka, hakuna ulinzi kutokana na usiyoyatarajia.

Tunaelewa njia hii ni sahihi na utenda kazi wa sayansi ya Kikristo ikiwa moja kwa moja na muonyesha njia, Kristo Yesu.



Kanisa lenu linatofauti gani?

Watu kadha wamaeuliza jinsi gani kanisa la Plainsfield ni tofauti na matawi ya kanisa la Boston. Kipande hiki cha andiko kinakusudia kuonyesha tofauti muhimu zaidi.

Hizi tofauti za kutekeleza Sayansi ya Kikristo zinatakiwa zichukuliwe kama wito wa vitendo kwa wote wanaopenda sayansi safi ya Mama Eddy. Kurekodi tofauti hizi ni kwa faida ya watu sasa na kwa na kwa vizazi vijazo. “Mambo yanayotambaa” yalitambaa ndani ya shirika la Boston kwa sababu hawakuwa maakini na waangalifu na mifumo ya uovu. Kama hatuko waangalifu, uovu, makosa, ama akili za kibinadamu zitatambaa tena na zijaribu kuharibu Sayansi ya Kikristo.

  1. Tunatumia muongozo wa toleo la 88, toleo la mwisho ambalo Bi Eddy aliidhinisha.
  2. Tunajibu kwa Mungu sio kwa bodi ya wakurugenzi ya Boston. Yale yoyote tunafanya, tunajiuliza kama Mungu anaweza idhinisha, na kama Mama Eddy anaweza idhinisha.
  3. Tunajiandikia masomo yetu na kuchapisha jarida letu. Hii inahitaji kuonyesha mara kwa mara.
  4. Tunatafakari kila siku kama ilivyofanywa nyumbani mwa Mama Eddy.
  5. Tunajitahidi kudumisha shirika la kiroho. Hakuna hatua za birokrasi ili kufanya kazi. Wakati mmoja wetu anapata wazo nzuri, maamuzi yanafanywa haraka.
  6. Maandishi ya wafanyikazi wa hapo awali yanapatikana ili yasomwe hapa. Hakuna maandishi ambayo “haijaidhinishwa,” hakuna mtu ambaye atakwambia ni lipi unaweza soma na lipi hauwezi.
  7. Katika shirika la Boston, maelekezo ya darasa ni ya siku kumi na ilikuwa tu kwenye maandishi. Maelekezo ya Plainsfield ni ya mwingiliano na ni endelevu; sio ya siku kumi pekee.
  8. Sisi ni wa kipekee. Kwa urahisi tunafuata uongozi wa Mary Baker Eddy. Hii ndio tunazingatia. Tunazungumzia tofauti kwa sababu watu wameuliza.
  9. Kutoka Maryland – Kuna hisia kubwa ya uwajibikaji kwa kuwa hapa amabao sikuwa nao katika kanisa hilo lingine. Kila uchao ilikuwa ni kusoma somo na kuhudhuria ibada jumapili; Hakuna kazi iliyopaswa kufanywa. Lakini hapa tunatakiwa kufanya kazi kila siku Ndio sababu mikutano ya ushuhuda ni tofauti kwa sababu tunawezashiriki yale tumekuwa tukisoma na kutekeleza, na matokeo ni nini. Katika kanisa hilo lingine, mikutano ya ushuhuda ilikuwa kinyume -hakuna mtu aliyekuwa na jambo la kusema kwasababu hakuna mtu aliyekuwa anafanya chochote. Kwa jukumu hii huja hisia kubwa ya nguvu za Mungu,kwa sababu tunajua kuna kitu ambacho kinaweza fanywa – sio lazima tuketi hapa natukubali chochote ambacho ni kibaya – kuna kitu tunaweza fanya juu yake.
  10. Kutoka Ugerumani – Hapa Plainsfield makosa yanagunduliwa alafu ukweli na upendo zinakubalishwa badala ya kusema “Mungu ni upendo” na kupuuza kila kitu. Hapa tunafundishwa kufichua uovu, kuuona na kuurekebisha.
  11. Kutoka Carlifornia – Katika matawi ya kanisa la Boston kulikuwa na ukarimu, na kila kitu kilikuwa chakupendeza na kizuri; lakini hapa Plainsfield, ni halisi. Unaweza hisi ukweli uliokomaa ndani yake. Huo uzuri unafunika dhambi nyingi. Tunatoa mambo nje yaponywe.
  12. Kutoka Georgia -Katika shirika hakuna aliyeshughulikia mabadiliko ya maadili ambayo yaliambatana na uponyaji. Hakuna aliyeongea kuhusu ubinafsi, kujivuna ama jambo lolote kama lile kuhusu mwenzake. Sikuona jambo kama hili likishughulikiwa – Hakuna mtendaji aliyetaja jambo lingine lililohitajika kulifanyia kazi. Ilikuwa tu ni, ” acha upendo ufanye kazi.” Lakini kuna mambo ambayo yanahitaji kubadilika. Mama Eddy anaongea kuhusu uponyaji wa Sayansi ya Kikristo ukikabiliana na mabadiliko ya tabia, sio kupata faraja tu. Ndio sababu ni hatari kuendelea ukifikiria, ” mimi ni mwanasayansi ya Kikristo na kila kitu ni sawa,” ilhali kila kitu sio sawa.
  13. Kutoka California – Mama yangu aliniambia kuhusu Plainsfield. Alinipatia nakala ya jarida ya kanisa la Plainsfield na nikaaza kusoma – na nikapata hakuna haya ndani yake. Nilihisi hatia kwa kanisa hilo lingine kwa wakati wote lakini sio hapa.
  14. Kutoka Pennsylvania – Mafundisho ya mashiko ya wanyama ni dhahiri katika kanisa hili. Mambo niliyoyasoma mbeleni haikuwa dhahiri, yote ilikuwa tu katikati mwa barabara. Hapa hakuna katikati mwa barabara na hiyo ni muhimu sana.
  15. Kutoka Ujerumani – Nikifanya kazi na mtendakazi wa Plainsfield, kwa wakati wote mimi hupatiwa kitu cha kufanya kazi nacho na kutafakari. Unapata ushirika -ni kama kuendelea kwa maelekezo ya darasa.
  16. Kutoka Georgia – Plainsfield inasisitiza umuhimu wa kuweka Mungu mbele – Mungu lazima awe mbele. Sikusoma somo kila wakati kitu cha kwanza asubuhi – labda nitaifanya baadaye, ama nifanye sehemu yake. Lakini hapa , Mungu ndio wa kwanza; lazima tumuweke mbele – kisha umuhimu wa kutumia unachojifunza. Siku yako yote hizi vitu vidogo vinafanya kazi na zinabadilisha maisha kwa kweli, kutenda sayansi vile inapaswa kutendwa.
  17. Kutoka Virginia – Kitu cha kuridhisha sana kuhusu kanisa hili ni kwamba kila kitu ki wazi na ni cha kuaminika, kila mtu anashiriki katika mambo yote,hakuna siri na kila mtu anafaidika kutoka kwa kila kitu ambacho mmoja anachosema na anachopitia. Hii inaendelea bila majivuno,unajua wakati mtu kwa kweli ameweza kushinda kitu, vile wanawezazungumza juu yake na waone ilikuwa makosa na haikuwa wao wenyewe.
  18. Kutoka New York – Kanisa la Plainsfield liko na wajibu wa kusimamia fedha zao wenyewe. Kanisa la Boston lilijiangusha kifedha na haingekubali kwamba imefanya makosa yoyote.



Ni tofauti gani iliyomo kati ya toleo la 1910 la Sayansi na Afya na funguo za maandiko ilioandikwa na Mary Baker Eddy na isemekanalo kama “toleo lililoidhinishwa” linalo tumika na Boston?

Tunapendelea toleo la 1910 la Sayansi ya Afya na funguo za maandiko ya Bibilia lililoandikwa na Mary Baker Eddy kwa sababu hili ndio toleo la mwisho la kitabu chake alichokiidhinisha Mama Eddy. Kwa kuwa hatufuatilii njia za Boston, ila kwa yale yametolewa kwetu. Lazima tuachilie yale wengine wameandika kuhusu maada hii. Hii imeandikwa na Helen Wright;

…..wakurugenzi wakuu wamefanya mabadiliko kwa Sayansi ya Afya .Wametoa picha ya Bi Eddy kwenye sura ya kitabu; wamehamisha na kufuta ushuhuda ambao Mama Eddy aliouchagua kwa maakini; wamebadilisha vichwa vidogo vya pembeni; wameongeza ” Maandiko yaliyo indhinishwa na kanisa la kwanza la Kristo mwanasayansi,

Boston,Massachusetts”; wameorodhesha vitabu na vitabu ndogo na vipeperushi kwenye ukingo wa

Sayansi na Afya; wamepunguza ukubwa wa msalaba na alama ya taji kwenye Sayansi na Afya, na kadhalika.”- kipande kutoka kwa Mwongozo wa kanisa ya Mary Baker Eddy na” kanisa ulimwengu na ushindi” iliyoandikwa na Helen M. Wright, ukurasa 143.

Shuhuda mbili za matunda za mwisho zilibadilishwa.” kipaumbele kisicho na bei.” {ukurasa 698-699} ilitolewa kabisa, na ” wazimu na kipanda usemi kapona” { ukurasa 604-605} ikabadilishwa na ” Tatizo la mgongo na kuhisi kichefuchefu kapona”.

“Mwakani 1908, taji kwenye picha ilibadilishwa ikawa ya kibingu ama taji la Kikristo,” – Muundo ule uliboreshwa kidogo mwakani 1971.”– Kutoka kwa maktaba ya Mary Baker Eddy, Boston.

Zaidi ya hayo, Helen Wright ako na sura katika kitabu chake Kama wangetii mwongozo wake Mary Baker Eddy ambayo ina tarehe, nakala za hati,rekodi zahatua zilizochukuliwa za haki miliki na bodi ya wakurugenzi kabla na baada ya 1910. Andrew Hartsook pia anazungumzia maada hii katika kitabu chake Sayansi ya Kikristo baada ya 1910 kwa ukurasa nambari 72.