Imani ya uvamizi |

Imani ya uvamizi

Iliyoandikwa na Mildred Leblond


Kuwepo hakuwezi ingiliwa sasa au wakati mwingine wowote, kwa sababu uwepo wote ni Mungu. Mungu hawezi na hafanyangi kujivamia mwenyewe. Hakuna kipato chochote kinachoweza kufikia taifa lolote isipokuwa Mungu, na Mungu anaunda kila uwepo. Uwepo ambao ni ” Mimi na Baba yangu ni mmoja.” “Kanuni na wazo lake ni mmoja,” ndio tu kitu kilichopo, na hakuna uwepo mwingine.Ufahamu huu ndio ” kila -kitu” kwetu sisi wenyewe na kwa watu wa mataifa yote. Kujua huku ndio tunataka sisi wote na ambao lazima tusambaze kwa kujua kila mtu ako na kila kitu.

“Mambo yote”kwa taifa lolote ni ufahamu ambao unatoka kwa Akili, kwamba uwepo wote ni mzima na ni kamilifu ndani yake. Uwepo huu wa kazi unafanyikia wapi?

Iko huko? Tunafanya kazi kubadilisha kitu katika nchi zingine? Kama ni hivyo tunafanya kazi kimakosa.

Dhihirisho itafanyika ndani ya ufahamu wako na sio pahali kwingine.

Uovu hauwezi kuingia katika wema. Uovu hauwezi kushambulia Mungu. Akili ya Kimungu haihitaji ulinzi. Tukiona kwamba Mungu ndio Akili ya binadamu, tunaweza elewa nafasi yetu wakati huu. Pahali popote binadamu yupo, kuna Akili.Na pahali popote Akili iko, Mungu yupo. Akili, ambayo milele ni wema, haitambui nguvu yoyote ingine tofauti na yenyewe, haitambui binadamu muovu na mwenye dhambi, hakuna vita. Hili azimio la Akili kuwa Akili ni mashambulizi kwa imani ya uovu.

Jisemee mara nyingi kwa siku, ” Mahali Mungu yuko, Niko, na mahali Niko kunayo nguvu ya Mungu.” Mahali ambapo nguvu ya Mungu iko, hakuna nguvu yoyote ingine, hakuna vita, kulipua, chuki au uvamizi. Kuna uhuru wa uwepo usio na mipaka – shujaa kwa nguvu zake mwenyewe, wema na uwezo.