Moyo Mpya
Kutoka kwa kitabu cha Mlinzi cha Sayansi ya Kikristo Januari 5 1918 na WILLIAM P. MACKENZIE
Kuna uwezekano kwamba katika nyakati zote za Ukristo na katika Uyahudi, ukombozi wa Yerusalemu umefanya watu kusoma kwa uangalifu sura ya thalathini na sita ya Ezekieli. Agano ambalo limeahidiwa kwa kinyume kwa uhusiano na maono ya awali ya nabii inafanywa moja kwa moja hapa na ya kiulimwengu ikiwa na idhini, “Bwana Mungu anasema.” Hii ndio agano: “ Pia nitawapa moyo mpya, na nitaweka roho ndani yenyu: na nitatoa moyo wa mawe katika mwili wenyu, na nitawapa moyo wa nyama. Na nitaweka roho wangu ndani yenyu, na kuwafanya kutembea katika sheria zangu, na mtaziweka hukumu zangu, na kuzifanya.”
Ikawa sehemu ya mila za Israeli vile Farao na waMisri walifanya mioyo yao ngumu, na kuingia katika maangamizo; na bado, baada ya onyo hili, tunapata kizazi baada ya kingine cha Israeli kikianguka kwenye kuabudu sanamu, na kwa uwazi wakiwa hawasikii neno la Mungu kama waMisri walikuwa. Kuhusu hali hii methali ilikuwa, “ Furaha ni yule mtu anayehofu kila wakati: lakini anayefanya moyo wake kuwa mgumu ataanguka kwenye utapeli.”
Tunapata kiongozi wetu akiwa mwenye huruma na mvumilivu kwa wale wenye kukosa imani na mioyo yenye baridi ya wafuasi wake. Mariko anarekodi kushangaa kwao juu ya dhihirisho lake la kutembea juu ya mawimbi na kutuliza dhoruba. Akaelezea hali yao ya kutoamka ya kwamba “ hawakuzingatia muujiza wa mikate: kwa sababu mioyo yao ilikuwa ngumu.” Tena, wakati Yesu aliwatahadharisha wafuasi wake dhidi ya chachu ya mafundisho ya uongo, wao kama wafuatiliaji mambo moja kwa moja, wakafikiria wakisema: “ Ni kwa sababu hatuna mkate;” ambapo alijibu: “ Kwa nini mnafikiria ni juu hamna mkate? Hamjaona hadi sasa, wala kuelewa? Mioyo yenyu badi iko ngumu?’’ Alikuwa anawauliza mbona hawakuridhishwa na mambo ya kiroho na kujibu Kanuni, ambayo kwake ilikuwa muhimu.
Paulo, akinukuu kutoka kwa Zaburi ya watu wake, anapatia sifa hamasa yake kwa Akili ya Kimungu, akisema: “ Kama vile Roho mtakatifu alisema, Leo kama utasikia sauti yake, usifanye moyo wako kuwa mgumu….Lakini inuaneni mmoja kwa mwingine kila siku, kama bado inaitwa leo; isiwe hata mmoja wenyu asifanywe mgumu kupitia udanganyifu wa dhambi.” Moyo uliofanywa kuwa mgumu hauwezi sikia ushawishi wa kiroho kwa sababu umedanganyika na dhambi. Lakini moyo mpya kwa kweli unamaanisha ufahamu unaoonyesha ushawishi wa Roho ambao huponya na kubariki, ufahamu wa wema ambao hakuna uovu unaweza vamia. Lazima iwe ni ufahamu mpya wa uhai wenyewe, ukitimiza ahadi ya Sayansi na Afya ukurasa 264, “ Tunapogundua kwamba Uhai ni Roho, kamwe sio ndani ya mwili au wa kimwili, ufahamu huu utapanua kuwa ukamilifu wa kibinafsi, ukipata yote katika Mungu, wema, na usipohitaji ufahamu mwingine wowote.”
Tunaweza pata neno lingine bora zaidi la moyo huu mpya unaopatianwa na Mungu ila kwa kuuita Roho wa Kristo? Unaofanywa hai na haya, tunataambua mambo ya zamani yamepita, na kupata kufanywa upya kama alfajiri ikileta mwangaza kwenye bonde, au chemichemi ikileta uhai katika nchi nzima, au maono ya nabii yakileta mwangaza katika dunia yote, ambapo furaha na uhai na upendo wa kindugu unatutajirisha. Kukosa haya, tajiriba ya binadamu itakuwa na giza na baridi na yenye chuki. Mama Eddy anaongea kujihusu kama anayejua ya kale na yaliyo mapya, lakini amekuwa mfafanuzi ambaye wote katika dunia watakuja kufurahia kujua yaliyo mapya, -watafurahia katika alfajiri, na kwenye chemichemi, na kufahamu.
Katika “Mkusanyiko wa maandishi” (p. 178] kiongozi wetu anasema: “Katika mwili, sisi ni ukuta wa kugawanyisha kati ya mambo ya kale na mapya, kati ya dini ya zamani ambayo tumefundishwa, na mpya, inayo uhai, wazo la Kristo lisilo na ubinafsi ambalo limepatianwa kwa dunia leo.”
Kwa wakati huu, ambapo mengi yanasemwa kuhusu mwaka mpya, matarajio mapya, maazimio mapya, sio vizuri kutamani moyo mpya, joto mpya ya upendo? Ambapo nguvu, udhibiti,na sheria katika mapenzi ya kibinafsi, au akili ya kibinadamu, kunapatikana moyo wa mawe, kama historia yaonyesha. Wengine kama Machiavelli wamefundisha ya kwamba mwana wa kifalme lazima ajitoe mwenyewe kutokana na huruma; na laini ndefu ya wana wa kifalme kanisani na nchi wameonyesha haya. Hivyo wakati umekaribia kwa wanadamu waangalie mbali na msaidizi wa kijamii, “ mwana wa binadamu, ambapo hakuna usaidizi,” na kugeukia Kanuni yenyewe, Upendo wa Kimungu, ambao unamkaribisha mwanadamu ukisema, “ Nitazame, na uokolewe, mwisho wote wa dunia.”
Paulo na Barnaba walinukuu unabii kuhusu Mesia, “ Nimekuweka kuwa mwangaza kwa mataifa, ndio uwe kwa wokovu mpaka mwisho wa dunia.” Sayansi ya Kikristo inaonyesha ukamilifu katika kuendelea kwa unabii huu, kwa sabu inaonyesha vile wanadamu kila mahali wanaweza fahamu na kuokolewa, na inawafundisha vile kuwa na “ moyo mpya,” au roho wa Kristo, leo. Mwandishi wa Sayansi na Afya, katika ukurasa wa 141 wa nakala hii, anafumbua uwezekano mbele yetu sisi wote: “ Katika kuponya waliowagonjwa na wenye dhambi, Yesu akafafanua ukweli ya kwamba Athari ya uponyaji ilifuatia ufahamu wa Kanuni ya Kimungu na roho wa Kristo ambao ulitawala Yesu katika mwili. Kwa Kanuni hii hakuna ufalme, hakuna mnara wa kidini. Kichwa pekee kilichowekwa taji ni utawala wa milele. Kasisi pekee ni binadamu wa kiroho. Bibilia inatangaza ya kwamba wanaoamini wote wanafanywa kuwa “ wafalme na kasisi kwa Mungu.