Msamaha
Kutoka Kwa Toleo La Jarida Ya MLINZI LA SAYANSI YA KIKRISTO La Novemba 8, 1919 La Iliyo Andikwa Na Ella W. Hoag
Mengi yamesemwa kuhusu msamaha. Mengi yamekuwa maombi ambayo yamekuwa na mzigo aidha hamu ya kusamehewa au hamu ya kujua kusamehe. Hakuna wakati ambapo mwanadamu hajawai kuwa na matamanio ya kupata msamaha wa dhambi. Mara tu mwandamu akipata ufahamu kuwa amevunja sheria za Mungu, yeye mara moja hutafuta namna vile anaweza pata uhuru kutokana na matokeo ambayo kimsingi anahisi yatakuwa matokeo ya uasi kama huo.
Hofu ya adhabu ya dhambi iliyotendwa imeambatana kila wakati moja kwa moja na imani kwa dhambi, na mengi na mbalimbali yamekuwa majaribio ya kuepuka adhabu kama ile. Inachukua kiasi kidogo cha uaminifu kutambua kuwa upendo wa dhambi uko chini ya majaribio ya kuepuka mateso yale, lakini bado atashikilia ile dhambi. Mradi dhambi inapendwa na kufurahiwa, kutabakia hofu ya adhabu ambayo dhambi yenyewe kila mara hulipisha kwa yule anayejiingiza kwa madai yake. Imani ya kuwa kuna kuridhika katika uovu imefunga macho ya binadamu kwa maumbile mbaya ya uovu na matokeo yake mabaya. Ni upofu huu ambao unafunga uwezekano wa kuona kuwa hakuwezi kuwa na msamaha wa kweli mpaka dhambi yenyewe imeachwa na kwa hivyo kuangamizwa; kwa kuwa hakuna anayewezatosheka na msamaha usioshikamana na kufutwa kwa ukumbusho wa ile dhambi. ‘ Sitakumbuka dhambi zao tena,” ni ahadi moja ya thamani zaidi katika ahadi zake Mungu.
Tukiongea vile binadamu ataokolewa kutoka dhambi, Mama Eddy anasema {Maandishi Mbalimbali ukurasa wa 90}: “Lazima ajue Mungu ni mwenye nguvu zote; kwa hivyo dhambi haina nguvu. Lazima ajue nguvu ya dhambi ni raha ya dhambi. Ondoa hii raha, na umetoa uhalisi wa nguvu yake. Yesu alidhibitisha ya kuwa dhambi na kifo hazina nguvu. Huu ukweli wa vitendo huokoa kutoka kwa dhambi, na utaokoa wale wanao ufahamu.” Kuamini ya kwamba dhambi huleta raha, ya kwamba inaweza zalisha wema ni kuamini mema yanaweza kuja kutoka kwa uovu, na hii ni kukana maumbile na nguvu za Mungu, aliyemwema. Ndipo mtu aweze kumpenda Mungu, aliyemwema, kwa kutosheleza awe tayari kusema kwa kila majaribu na kuingia kwa imani ya dhambi, ” Hauwezi nindanganya, kwa sababu hauwezi leta raha,” ndio mwanzo wa kudhibitisha uongo wa dhambi. Wakati mtu ako tayari kukiri ya kuwa dhambi haileti furaha, ameanza kushinda ufahamu wa maana ya msamaha wa dhambi. Mama Eddy anatwambia { Sayansi na Afya, ukurasa wa 5}, “Dhambi inasamehewa wakati inapoharibiwa na Kristo, – Ukweli na Uhai.” Hii inafungua kwa binadamu uwezekano wenye utukufu wa kufuta dhambi, ambayo inaleta msamaha kamili; kwa sababu dhambi inasamehewa kama imetelekezwa.
Kwa moyo uliyojaa mizigo na tamanio la kuondoa dhambi, hata kama imefungwa kwa kupitia elimu ya uongo, sio tu kwa imani ya uhalisi wa dhambi lakini pia kwa hofu yake, Sayansi ya Kikristo yaja na pendekezo la furaha la ukombozi na inainua mtu mara moja kwa hisia ya tumaini, ambayo shule hazijawai patiana. Haifunui tu kutotamanika kwa dhambi, lakini inafundisha vile makataa ya kuridhika kutoka kwa msimamo wa kufahamu mara kwa mara kwa utoshelezaji wa wema, itachangia kuongezeka kila wakati kwa nguvu za kupinga na kukataa madai yote ya dhambi na kuleta ufahamu wa msamaha ule ambao haujui wala kukumbuka dhambi. Kwani wakati dhambi imetelekezwa kwa kweli, hakuwezi tena kuwa na hitaji au majaribu aidha kuiogopa au kufikiria juu yake kutoka kwa mtazamo wowote.
Yesu alitufundisha kuomba, ” Tusamehe makosa yetu, kama vile tunawasamehe waliotukosea sisi,…kwa maana mkiwasamehe wanadamu makosa yao, Baba yenyu wa Binguni atawasamehe pia: lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenyu hatawasamehe pia.” Furaha na uhuru ambazo zinaongezeka kwa mtu kutoka kwa msamaha wa kisayansi – ikifuta, kuangamiza hata ukumbusho wa dhambi zake, inaweza tu zindiwa na furaha inayomjia wakati kupitia hii mbinu anajipata akiweza kusamehe na kusahau – dhibitisha sio ya kweli -makosa ya nduguye kwake. Wengi wakristo kabla ya Sayansi ya Kikristo kufunuliwa kwao walikuwa wameomba kwa dhati na kwa mda mrefu ili kusamehe jeraha na wakati mwingine alihisi maombi yake yamejibiwa,- ya kwamba ilikuwa inawezekana kumpenda ndugu yake licha ya makosa yake; wakati tazama na uone, makosa ya pili kutendewa dhidi yake na ndugu yuleyule, na hapo ndio makosa ya kwanza inajiwasilisha kusamehewa tena! Basi jinsi inavyoonekana ngumu kazi ya kusamehe mpaka ” sabini mara saba” amri ya Yesu!
Jinsi ambavyo ni tofauti sasa, kwa mwanga wa ajabu ambao Sayansi ya Kikristo inatupa, ikituonyesha vile kufahamu na kufuata mafundisho na mfano wa Bwana wetu mpendwa. Inaonyesha kwa uwazi kwamba sababu ambayo mtu hutenda dhambi, au anaendelea hata kuamini dhambi aidha ndani mwake au kwa wengine, ni kwa sababu anaamini – mara nyingi hila – ya kwamba anawezapata raha kwa kufanya hivyo. Basi nani anaweza kuwa mjinga hivi kwa kuendelea kwa mateso haya ya mawazo maovu, wakati anachohitaji kufanya ndio apate amani na starehe na furaha ni kugeuka mbali na dhambi kwa upendo wa Mungu, aliyemwema. Furaha ya kushangazaje inayopatikana kwa kupenda wema kinyume na kila imani isiyo na msingi mpaka hakuna imani ya dhambi itakuwa na nguvu za kupotosha au kutushikilia kwa nguvu za chuki. Basi tuinue huu upendo wa wema kwa roho zetu mpaka watu wote waone nguvu za Mungu za kubariki kwa kipimo kilichozidiwa kwa wale wote wanasamehe kama vile wangesamehewa.