Msimamo wako ni upi? |

Msimamo wako ni upi?

Kutoka kwa Sayansi ya Kikristo, mafundisho yake safi na sahihi iliyoandikwa na

HERBERT EUSTACE

UKURASA 751 MPAKA 753


Tuchunguze haya na tuone ni msimamo upi ambao tunachukua. Kwa shughuli za dunia na vile zinakaa kuwa, kuna hitaji kubwa kuona mahali tumesimama, kwa kuwa kwa kweli kamwe hakuna wakati shughuli za dunia zinakaa kuwa na matatizo, kamwe zaidi ya wakati Yesu alirejelea akisema, “Mioyo ya wanadamu ikiwakosea juu ya hofu, na kuangalia zile vitu ambazo zinakuja duniani.” { Luka 21:26}

Hata hivyo , kama unavyojua , yale ambayo yanakaa kuwa na vile iko kwa kweli, kwa mmetafizikia, ni umbali mkubwa. Kwa kweli hakuna uhusiano wowote kati ya hizi mbili na ndio sababu Sayansi na Afya inatangaza , “ Kando na imani na ndoto ya maisha ya kiasili, ni uhai wa kimungu, ukifunua ufahamu wa kiroho na ufahamu wa utawala wa binadamu juu ya dunia yote.” {S & A 14:25} Tena kwa kugeuza kauli ile, tunaweza tangaza kwa usahihi, kando na imani na ndoto za shughuli za dunia na inayoonekana kama migawanyiko na hofu, ni ukweli wa kimungu, dunia ya kimungu, ikifunua ufahamu wa kiroho na ufahamu wa utawala wa binadamu juu ya dunia yote.

Je, unafikiria inatimiza kitu kimoja kwa mwelekeo unaofaa kwa mwana sayansi ya kikiristo kutazama dunia na kusema iko vile na kuikubali kuwa katika hali tatanishi na sitofamu? Uko na nguvu kamili na mamlaka kama Mwanasayansi ya Kikristo kulainisha yale ambayo yanayoonekana kama hali ya dunia au hauna usaidizi wowote na unalazimishwa kunyenyekea na kuzikubali?

Unajua kama Mkristo msayantisti ya kwamba yoyote unakubali kama Akili bila shaka lazima ijidhihirishe kwako kama vile. Ni nini unakubali kama Akili ambayo inaweza kufanya kukubali hali iliyo na utatanishi na ya kuvunja moyo katika dunia? Hakujakuwa na wakati mwingine mwafaka wa kukutana na kukabiliana na swala hili na kuona iwe hivi au la kama tunaamini ya kwamba Akili ni yote kwa yote. “ Chochote mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni:” {Mathew 16:19} Haya yakiwa kweli, tutanyenyekea na kukubali hali zinazoonekana kama vile aitwae binadamu anafanya na kusema , Vema, labda itachukua mkondo wake?