Msingi ulio imara
Kutoka kwa toleo la December 8 1917 la Mlinzi wa Sayansi ya Kikristo na JOHN B. WILLIS
Ni mara nyingi roho ya ujasiri ulio tulia unapata onyesho katika nukuu ya mwandishi wa Zaburi kuhusu Mungu kama “ ngome,” kama msingi usiotingisika wa imani, uhakika, na furaha! Katika madai ya majaribu na majonzi, huu ukweli unatambulika milele kama kitu kimoja cha uhakika, kimbilio la milele hivyo tunampata akisema: “ Nafsi yangu, msubiri Mungu pekee; kwa kuwa tegemeo langu latoka kwake. Yeye pekee ndiye ngome na wokovu wangu.” Hii pia inakumbusha maneno ya Bwana kwa Petero akiheshimu utambulizi wa mtume wa Kristo, – “Juu ya ngome hii nitajenga kanisa.”
Dhana ya maandiko ya msingi wa imani hivi maajuzi ulikumbushwa na mmoja aliyesimama katika uwepo wa jumba lenye sifa la Woolworth New York. Unene wa kipande kinachoinuka mara moja ilisababisha mshangao vile msingi wowote ulivyoundwa ambao ungedhibitisha kuwa sawa na kushikiliwa kwa jengo kubwa vile. Alafu akaambiwa vile bonde kubwa lilipochimbwa katika ardhi, mpaka ukingo mkubwa ambao juu ya mabega yake hata milima ya Himalayas yangedhibitisha uzito wa manyoya, ulifumbuliwa, na juu yake kulijengwa mjengo mkubwa wa simiti na chuma, ambao haujakuwa na uzito hata kwa mzigo mkubwa, kwa sababu dunia inaushikilia.
Ya kwamba mchoraji wa mjengo alikuwa na hekima ya kuangalia kwenye mwanzo wa kazi kama ile, inaonyesha bila kusema, na ufahamu huu wa kawaida ni wa hekima kuhusiana na kujenga imani ya Kikristo. Kwa kusisitiza Yesu akawaambia hadithi walioifahamu ya mtu , aliyechimba kwa urefu, aliweka msingi wa nyumba yake juu ya mwamba, na hakuna mafundisho ya Sayansi ya Kikristo iko na busara zaidi na yenye asili kuliko kusisitiza kwake kwenye njia hii. Maombi ya Mama Eddy kwa wanadamu yanaweza semwa kuwa yenye asili ya maulizo ikiheshimu misingi ya ukweli, ikiheshimu asili ya Mungu na ulimwengu wake, na mwanadamu. Imani ambayo Sayansi ya Kikristo inasimamisha katika ufahamu wa binadamu inadhibitisha imara naya kudumu, kwa sababu inatoa ujinga na desturi zisizodhibitishwa ambazo imani za kimwili zimeacha kwa kila sehemu ya “hisia njema zenye ustadi;” na basi kufikia kwenye mwamba wa ukweli anaodhihirishwa, unaendelea kuinua mng’ao wa jengo la Mungu ambalo ni “la milele katika mbingu.”
Wakati mtu yuaja kukumbana uso kwa uso na hisia kuu ya mkasa mkubwa kama tulio nao leo, wakati tumaini imezidiwa na mafuriko ya imani zinazotofautiana za dini, au unapoitwa kukumbana na ugonjwa unaosisitiza kutopona, -basi ndio wanadamu hupata haja kubwa ya msingi usiotingisika wa kimawazo. Halafu wananena na Mzaburi wakilia, “Moyo wangu na mwili wangu wamlilia Mungu aishiye;” na katika lisaa kama lile furaha kwa Mkristo Msayantisti ambaye amedhibitisha kwake mwenyewe uwepo na upatikanaji wa ukweli wa milele ufahamu ambao ulimueka taji Kristo Yesu “Na utukufu wa ufanisi bora na ushindi wa milele” {Sayansi na afya, ukurasa 45}, hata katika kati ya mgongano wa kimwili.
Kabla njia za mawazo ya kisayansi zimekuwa za kueleweka kwa mwana sayansi ya Kikristo, ya kwamba haya nyayo zake zinaweza zifuata hata kwa giza, na katika hali hii ambazo zinasababishwa wakati mtu anakutana na wale ambao hawana mapendeleo na mafundisho ya Bibilia , kwa wakati mwingine tunapata misingi ingine ya kimawazo. Kwa mfano, katika udhibitisho wa falsafa ya Descartes’, “Nafikiria; kwa hivyo mimi ni,’’ haitahojiwa na mwanamume na mwanamke wa kawaida.
Sasa ukuu wa mawazo ya kibinadamu, michakato ambayo wanadamu wanafanya maamuzi ya mduara wa kometi kwa kipindi cha miaka mia moja, au kubaini kwa uhakika wa kushangaza eneo la kivuli cha kuzingirwa kwa jua au mwezi ambao utapatikana nusu karne kabla; mawazo ya kujenga na kupaa kwa unabii, ambayo inapendekeza mfuatiliano wa utendaji wa ubunifu na nguvu, – mafanikio haya ya ajabu ya kiakili lazima yahesabiwe kama adhari na kwa sheria ya kiulimwengu ya sababu zinazotosha, inadai maelezo ya kutosha. Hakuna njia ya kutoroka madai haya; lakini wakati mtu anasisitiza maelezo ya kutosha juu ya dhihirisho hizi za kimawazo, amepata lile ambalo haliwezi kupatikana bila hekima na nguvu. Amepata Mungu wa Kikristo, ila anaweza ita ambayo haijulikani. Wakati mwanasayansi asiye amini dini anakiri ugunduzi wa asioeleweka na ufahamu wa milele katika kila kona ya ulimwengu, – na haya bila kujali ukosefu wa imani, – hayuko mbali , alijua, kutoka kukubali mafundisho ya Kristo Yesu, na mafundisho ya Sayansi ya Kikristo ya kwamba “ yote ni Akili ya milele na dhihirisho zake” { Sayansi na Afya, ukurasa 468}.
Hivyo kwa wale wote walio timamu na wako tayari kufikiria, ambao hawabashiri bila maana, kufanya kuamini mtazamo kwa mambo yaliyo mazito, na ambao wako tayari kukubali kwa kutafuta maelezo yanayo tokana na tajiriba za kiakili,- kwa kuwa njia inayoinuka inaweza patikana kati ya mabonde ya kutoamini, kuchanganyikiwa kuliko na giza. Hata hivyo anaweza fikiria juu ya “iliyo bora kabisa” hakuna uwezekano wowote kwa mtu yeyote kuamua akilini mwake ya kwamba asili inayotawala ufahamu ina uwezo wa kufanya uovu, na kwa kiwango ambacho anakataa kufanya yale anaweza kuwa mkarimu kwa mafundisho ya Bwana, ya kwamba Mungu, msingi na maelezo ya uwepo wa ukweli, ni Upendo; na katika juhudi zake za kuzingatia kile ambacho kiko na chuki kiitwacho uovu, lazima atazame kwingine kwenye chanzo cha wema.
Ingawa haijafikiriwa na wengi, inaonekana kwa urahisi ya kwamba hukunao giza katika mwangaza, hakuna makosa katika ukweli, na hakuna uovu katika wema, ingawa kwa kiasi ambacho umeshikana katika tajiriba ya kibinadamu, hiyo ni kulingana na ushahidi wa kimwili.
Utambuzi wa wazi wa hali ya kiakili, maoni sahihi ya hali ambayo mtu anaweza jipata wakati wowote katika tajiriba, na hekima yenye mpangilio ambayo atashughulikia na kutosheleza hisia za kibinadamu zinazoyumbayumba ili kuweza kuzitoa kwa matope ambapo zimekwama, – hii huamua matokeo yenye furaha ya mapambano, na kudhibitisha mwadhiriwa wa utapeli wa kiakili au ukosefu wa mantiki ambapo juu ya msingi imara ambapo nyayo zake haziwezi tingisika tena. Ni hivyo kwamba ukweli uliodhibitishwa, katika ufahamu wa wema na hekima, inaweza kuwa mwamba wa kimbilio katika nchi yenye dhoruba; na hivyo kuhudumia wenye dhiki ya kiakili ni mojawapo ya haki maalum za kila mwanasayansi ya Kikristo wa ukweli.