Mungu Mzawadia
Iliyoandikwa na REV. G. A. KRATZER
Katika sura ya 11 ya Wahibrania, tunasoma: “Anayekuja kwa Mungu lazima aamini kuwa yeye ni mtoaji wa zawadi kwa wale wamtafutao kwa bidii.” Mstari huu ukieleweka kwa usahihi na kutumika vilivyo, hutupatia mwelekeo wa kushinda magonjwa ya mwili, pamoja na aina zingine zote za uovu na vikwazo. Kufanya haya kuwa ushahidi, tutumie mda kwa kukagua madai mengine ya makosa.
Kinyume na imani ambayo kwa kawaida imekubalika, mwili hauna uwezo wa kusikia maumivu au raha. Ingekuwa unaweza maiti ingeweza kusikia uchungu au raha. Ni wakati tu ufahamu umeshikanishwa na mwili ndio uchungu na furaha zinaweza sikika. Hii inaonyesha, katika ukweli, ni ufahamu ambao unaumia, au kuchomeka au unadhoofika. Neno ugonjwa linamaanisha ukosefu wa urahisi; na ni ufahamu ambao umekosa urahisi, kama kuna ugonjwa wowote na sio mwili. Wakati kuna ugonjwa, mwili kwa kawaida hauko katika hali ya kawaida kupitia uvimbe, vidonda kwa mwili; na usumbufu unaonekana kuwa katika sehemu hizi zisizo za kawaida za mwili. Kwa hivyo, imejulikana kwa kawaida ya kwamba hali zisizo za kawaida za mwili zinasababisha kuwa na usunbufu katika akili; lakini kinyume ndio ukweli, kama inavyodhibitishwa kwa njia mbili.
Ufahamu unapotenganishwa na mwili kupitia kifo, uvimbe, vitu vilivyo kua kwenye mwili visivyo vya kawaida, vidonda vinaweza baki kwa mwili, lakini hazileti usumbufu tena kwa njia yoyote, kwa mwili au kwa akili, ikionyesha mwili hauna uwezo wa uchungu. Wala hali zisizo za kawaida { isipokuwa hali za kawaida za kuoza} zikikua katika mwili, wakati ufahamu hauhusikani nao. Hii inaonyesa mgawanyiko siyo ya kwanza katika mwili, na baadaye katika ufahamu lakini ni ya kwanza katika ufahamu, kisha inaonekana kwa mwili kama matokeo.
Kwa uhakika, inapaswa kukubaliwa ya kwamba uvimbe au kidonda, kwa kawaida hukua kwa kiwango kwenye mwili , kabla akili kujua kuwepo kwake pale au kupata uchungu kutoka kwake, na huu ukweli umefanya wengi wa wanadamu kuamini ya kwamba ugonjwa unaanzia katika mwili na baadaye unaanza kusumbua akili, lakini ukweli ni, akili ya kibinadamu { ambayo ndiyo akili ambayo lazima tukabiliane nayo wakati tunachambua madai ya makosa} iko na awamu ya fahamu isiyo dhahiri, ambayo kupitia kwake mwili kwa kiasi kikubwa hutawaliwa, isipokuwa serikali ya Mungu inadhihirishwa kisayansi. Ugonjwa unaanzia katika awamu hii ya ufahamu usiokuwa na dhahiri wa akili ya kibinadamu na kuwa dhahiri katika mwili na mwishowe huanza kusumbua akili iliyo dhahiri. Katika uchambuzi wa makosa, uongo au ukosefu wa uhalisi, ni ile inayojulikana kama akili isiyo dhahiri, ambayo utendaji wake umejulikana kwa kiasi kidogo mpaka hivi karibuni, hio ndio njia kuu na kiti cha ugonjwa na dhambi, kwa Kadiri binadamu wa kimwili anahusikana. Katika kutokuwepo kwa udhibiti wa akili ya Kimungu, akili dhahiri na akili isiyo dhahiri ya kibinadamu inatenda na kujibu kwa yenyewe na kujielimisha katika dhambi na ugonjwa ikitumia mwili kama njia ya kupitia, – mchezo tu wa mpira, kama vile imekuwa, kwa kuchezwa huku na kule kati ya ufahamu na awamu ya ufahamu usio dhahiri ya majibizano ya uovu: lakini akili yenye ufahamu usio dhahiri ndio mwenye dhambi asili, na kama haitazuiwa kufanya vile na akili ya Kristo, itajirudia na kwa kuendelea, itarusha kwenye ufahamu wa akili aina zote za hisia za dhambi na za uchungu, na ufahamu wa akili unafikiria ya kwamba mwili ndio chanzo au sababu ya hizi hisia za dhambi au uchungu, badala ya kubaini chanzo cha ndani cha uovu katika maadili ya ufahamu usio dhahiri. Ni ufahamu huu usio dhahiri wa kibinadamu ambao lazima usafishwe kwa kutumia akili ya kimungu, ili kuondoa ufahamu wa akili na mwili wa uovu na migawanyiko. Mfano wa kufanya haya utaongelewa baadaye.
Ushahidi wa pili ya kwamba mabadiliko yasiyo ya kawaida katika mwili sio ambayo yanaleta kutokuwa na raha katika ufahamu, ni ukweli kwamba uchungu au hali ya usumbufu katika akili inatolewa kikamilifu masaa au kwa wakati mwingine wiki kadha, kabla ya uvimbe au kiuongp cha uongo kilicho kwenye mwili, ambacho kwa wakati mmoja kilionekana kuwa na uchungu, kimeangamia kutoka kwa mwili. Ikiwa haya mabadiliko yasiyo ya kawaida yalikuwa ndio sababu ya usumbufu wa akili, usumbufu wa akili haungeondoka mpaka mabadiliko haya yasiyo ya kawaida haijashindwa. Kwa wakati wote, kutolewa kwa usumbufu katika akili kupitia matibabu ya Sayansi ya Kikristo, yanafuatwa, mapema au baadaye, na hali za kawaida za mwili.
Sasa imeonyeshwa kwa wazi ya kwamba magonjwa yote inatokana na akili, na inapatikana katika ufahamu na kwamba hali zisizo za kawaida za mwili sio, kuongea kwa ukweli, ugonjwa lakini ni onyesho au adhari za ugonjwa, sio sababu yake kamwe. Hivyo ni dhahiri ya kwamba jitihada zinazofaa za kuponya ugonjwa lazima ziweke kazi yake kati kwa kutoa uovu katika ufahamu, na kama; imetolewa kwenye ufahamu, itatoweka kutoka kwa mwili moja kwa moja. Ile ambayo inafaa kutibiwa ni akili na sio mwili.
Lazima iwe dhahiri, kwa kauli, ya kwamba ugonjwa au akili iliyo na ugonjwa ni akili yenye uovu; na ya kwamba njia ya kushinda akili ovu ni kuishambulia na ile ambayo inaipinga, kwa jina Akili ya wema. Sasa kuna Akili moja njema. Kristo Yesu alitangaza: “Hakuna aliyemwema, ila mmoja; yeye ni Mungu.” Tukigeukia kwa ufahamu na kwa ustahimilivu kwa Akili hii njema, Mungu, Akili ile itatoa uovu kutoka kwa ufahamu wetu kwa njia asili kama vile jua huondoa giza kutoka machoni mwetu, wakati tunageuka kutoka kwenye giza kwenye jua.
Yeyote anayetazama mwangaza wa jua, anatazama mionzi ya zambarau, samawati, kijani,njano, chungwa, nyekundu, na kivuli kingine chochote kilicho kati cha rangi, yote iliyochanganyishwa vizuri kwa ile tunayoita mwangaza. Kwa njia ile, yeyote anayemgeukia Mungu kwa bidii, na kumtazama kwa akili, hawezi kosa kumtazama kwa wingi, na kupokea kwa utaratibu katika ufahamu wake, upendo, furaha, amani, nguvu, uwiano, afya, dutu, tele, burudani, ufahamu, na maisha yaliyochanganyishwa kwa uzuri kwa “samawati ya kweli ambayp huangazia kwa kila mwanadamu ambaye hukuja duniani.” Kwa sababu Mungu yupo kila mahali, na sio zaidi ya kufikika kwa mtazamo wa kiakili wa mwanadamu yeyote; ndio, yuko katika roho ya kila mwanadamu, wakati yule mtu atafungua moyo wake kwa bidii kwa Mungu.
Kwa hivyo tukimgeukia Mungu, tukijua kwamba yupo hapa, na tukimtafuta kwa bidii, atatuzawadia kwa kung’aa katika mioyo yetu, na akili kwa kila aina ya wema uonekanao; na kwa kiwango ambacho haya yaja kupita, kwa kiwango kile giza ya dhambi na ugonjwa zinatolewa kwa kila awamu ya ufahamu wa binadamu, na tunaponywa au kufanywa wazima katika ufahamu, pale ambapo tunatakiwa kuponywa, na mwili baadaye moja kwa moja unaangazia uwiano wa Kimungu ambao kupitia nguvu za Mungu imeimarishwa katika akili. Hivyo hivyo, katika uponyaji wa magonjwa, ushauri wa Mtume Paulo ni bora: “Kuwa tayari {Chagua} kutokuwepo kutoka kwa mwili {katika mawazo}, na kuwa na Bwana.” Kwa kuwa Mungu ndiye mponyaji; na atatuzawadia na uponyaji, tukija kwake kwa bidi.
Dhani giza ijisemezee, “Nitainuka na kushambulia mwangaza.” Nini itafanyika kwa giza baada ya kukaribia mwangaza? Ni yapi itafanikisha ila uangamizaji wake?
Somo: Kama hakuna makosa {Giza} katika ufahamu wa mtu,makosa ya mababu zake, na mashawishi yote ya mafikira hayatakuwa na nguvu za kumdhuru kama vile giza haina nguvu za kudhuru mwangaza . Na haya ni kweli kwa kibadiliko na kwa kweli kama jambo la mafanikio kamili. Kuondolewa kwa kiwango chochote cha makosa katika ufahamu wa mtu, kwa kumgeukia Mungu, inampa kinga kutokana na mashambulizi ya aina ypyote ya makosa kutoka nje.