Muungano wa mioyo inayofahamu |

Muungano wa mioyo inayofahamu

NA WILLIAM P. MCKENZIE

KUTOKA KWA TOLEO LA NOVEMBA 15, 1919 LA JARIDA LA MLINZI LA SAYANSI YA KIKRISTO


Katika mkusanyiko wa mashairi ya kidini inayohusishwa na Mfalme Daudi kuna zaburi moja ambapo analalamika kwa wale wasio mheshimu Mungu asiyebadilika. Anaonyesha vile binadamu anaweza kwa maringo na maongeo yenye uongo , kufunika makusudio yake potovu. Kwa mmoja kama yule, anasema: “Amenyoosha mkono wake dhidi ya wale walio na amani naye: amevunja agano lake. Maneno ya kinywa chake yalikuwa nyororo kuliko siagi, lakini vita ilikuwa moyoni mwake: maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, ila bado yalikuwa panga zilizochomolewa.” Bwana wetu alitoa ufunuo juu ya makazi ya makosa wakati alisema, “Kutoka ndani ya mioyo ya wanadamu, ndio kunakotoka mawazo maovu, uzinzi, usherati, mauaji, wizi, tamaa, uovu, undanganyifu, ulegevu, jicho la uovu, kufuru, kiburi, ujinga: uovu huu wote hutoka ndani ya moyo na kuchafua mwanadamu.” Sasa kama vita na treni yake ya uovu itakoma, lazima inyimwe makazi na irudi mahali mafichoni inaweza chuchumaa nyuma ya skrini ya maneno ya uongo na yaliyo nyororo. Ikifurahishwa katika moyo hukua kama mtoto wa simba marara aliyewekwa kama kitu cha kuchezea, ambaye kwa unene wake anaweza shambulia mwenyeji wake. Kutoka nyakati za awali imesemekana, “Wale wote wanaouchukua upanga wataangamia kwa upanga.” Sio kwa ushindi katika vita, lakini kwa ushindi juu ya vita ndio wanadamu watajipata wamekombolewa. Mama Eddy amesema {Maandishi mbalimbali, ukurasa 281}, “Vita itaisha wakati mataifa yatakuwa tayari kwa maendeleo.”

Wakati mwingine inafanyika ya kwamba walio na mawazo sahihi na walimwengu wenye ucheshi wanaitwa kupigana na wale wanaoamini vita. Watu wanaoshughulika na njia za amani watafanikiwa; kutakuwa na mashamba yenye rotuba, kondoo na ng’ombe, nyumbani mahali sanaa inatoa mapambo na hazina. Mkuu wa kabila aliye na vita katika moyo wake huita wapiganaji wake kutazama ya kwamba wanaweza iba magala, kuhamisha mifugo, kuiba na kuharibu manyumba, na kuwashika mateka ambao kupitia amani wamefaulu na wako na furaha. Hivyo anakataza sheria ya maadili na kutangaza sheria ya shetani, akiahidi ya kwamba wataiba na kuua na kufanya uzinzi, na kuekelea mikono kwa chochote watakachotamani. Ni muhimu, basi kama sio kwa ulinzi wa mali yao, ila kwa ulinzi wa wanadamu, wa wanawake na watoto, ya kwamba wafanyi kazi wa amani wakati mwingine watachukua vyombo vya vita na kupigana. Wanaweza fanya haya wakiwa hawana vita katika mioyo yao, lakini kwa ujasiri, azimio, na imani. Lakini kama wote katika dunia wanaoheshimu sheria ya maadili, kama wale wote wanaopenda amani na njia zenye utaratibu na furaha ya kazi yenye mpangilio, walikuwa wameungana, wangetangaza ‘Hapana’ inayokataza kwa wale wote wanaopendekeza vita na hivyo unabii ungetimika kwa kiasili ambao unasema kwa mataifa: “Wataunda panga zao za vita kuwa majembe, na mikuki yao kuwa ndoano za kupogoa: Taifa halitainua upanga wake dhidi ya taifa lingine, wala hawatasoma vita tena. Lakini wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mti wa mkuyu wake; na hakuna atakaye watia hofu.

Wakati kunao katika binadamu akili ile ile “ ambayo pia ilikuwa ndani ya Kristo,” kutoka kwa maisha yake hutiririka mvuto na athari kama ilivyodhihirisha maisha ya wale Bwana aliita wanafunzi wake. Kuwa na uponyaji katika moyo ni kinyume cha vita katika moyo. Kila karne iko na myanyasaji mwenye kiburi ambaye anaweza fanya dunia kutingisika kwa sababu ya upanga wake unao tetemeka. Kwa hamasa yake huwasumbua wanadamu, akiwatuma majeshi yake kushinda na kuharibu. Anahalalisha ukatili na unyanyasaji kama itasaidia kusudi lake, na kwa hivyo kutoka duniani kunatoka kuchanganyikiwa, ukame, magonjwa, kubomoka, huzuni, kifo. Karne kwa karne imekuwa vile, lakini kwa kweli ni wakati ujinga wa dunia kuwa na mwisho wake. Na tukumbuke ya kwamba ni mabakia wachache duniani wanaoimani ya vita. Wanawezaje kwa mvuto kuwashawishi wengine kuingia kwa mipango yao kama hawa wengine walikuwa na mawazo sahihi? Waudaji nakala za uongo na wadhibitishaji wa akaunti na watazamaji waongo hawapotoshi wale wanaofikiria kwa isabati na kwa kweli. Fikiri basi, ya kwamba kutakuwa na makubaliano kati ya wanadamu kufikiria mawazo ya Kikristo na ya kisayansi; hiyo ni, kukubali Mungu kama Kanuni na Kristo Yesu kama mfano; si wanadamu wangefahamu ufanyaji kazi wa Kanuni ya Kimungu, na kusema kama mwandishi wa Zaburi alivyosema, “ Anafanya vita kusita mpaka mwisho wa dunia?”

Wanasayansi ya Kikristo duniani kote wameungana kwa kusudi la heshima. Wanafanya bidii kuwa wamepona wenyewe, na kudhibitisha kwa wengine wema wa Mungu wetu ambaye anasema, “Mimi ni Bwana anayekuponya.” Wanaona mbele kwamba kama Ukristo unakuwa wa vitendo na wanadamu wanasita vita juu ya maoni ya kidini na faida za kisiasa, kutaja umoja wa kimataifa kwa sababu kutakuwa na utiifu wa sheria ya maadili, na muongozo katika maisha ya wanadamu juu ya mafundisho ya Somo la Mlimani. Kwa asili, wanasaidia na kuendeleza juhudi zote za ukweli kustawisha utakatifu duniani, iwe ni muungano wa kimataifa au kuungana kwa uhusiano wa kifamilia uliovunjika. Kwa kweli, wale wote wanaotii Kanuni wako katika muungano na makubaliano kwa kusudi hii, ya kwamba ufalme wa Mungu na uje. Muungano huu wa wale ambao wako mioyo iliyo na ufahamu ni muhimu, kwa kuwa wapinzani wa Mfalme wa amani wameshikana na kuungana. Mama Eddy amesema {Mkusanyiko wa maandishi ukurasa 177}, “Nguvu za uovu zimeshikana pamoja kwa jama ya kisiri dhidi ya Bwana na dhidi ya Kristo wake, kama inavyoonyeshwa na kutendwa katika Sayansi ya Kikristo.” Alafu anauliza: “Utafanya nini juu yake? Utakuwa maakini vilevile katika ukweli?” Utaachilia utulivu wako na kuwa shujaa aliyetakaswa? Utajipatiana kikamilifu na bila kurudi nyuma kwa kazi kuu ya kuimarisha ukweli, injili, na Sayansi ambayo ni muhimu kwa wokovu wa dunia kutokana na makosa, dhambi, ugonjwa, na kifo? Jibu mara moja na kwa vitendo, jibu kwa usahihi!”