Mwaka Mpya |

Mwaka Mpya

Kutoka kwa toleo la 1927 la jarida la Sayansi ya Kikristo na Ella W. Hoag


Katika shairi moja yake ya awali Mama Eddy ameandika { Mashairi ukurasa 28}

“Baba wa kila enzi,

Wa kila duara linalozunguka,

Tusaidie kuandika ukurasa usiokuwa na kifo

Wa ukweli, mwaka huu unapoanza!”

Na kunaweza kuwa na tumaini la utakatifu kushinda hili kwa kila mwana Sayansi ya Kikristo katika mwanzo wa mwaka huu wa elfu moja mia tisa na ishirini na saba?

Kuna kitu cha kuridhisha kila wakati katika mwanzo wa kila mwaka mpya. Watu wengi huwaza, hata kwa mda mfupi, kuna nini katika maisha yao. Hakuna moyo wa kibinadamu ambao hauwezi guzwa na mvuto unaotokana na enzi mpya kama mwanzo wa mwaka mpya. Kupitia mawazo ya mwaka mpya kunao hisia ya uwezo wa kuacha mambo ya awali na kushikilia yale mapya, nafasi ya kufunga akaunti mzee na kuanza upya. Ni kama mtu amepatiwa nafasi kuchukua mkataba mpya wa maisha yake; ni kama nafasi ilikuwa inapatianwa ambapo mtu angeongeza thamana kwa kile kipya kuliko kilivyo onekana zamani.

Katika ibada ya kujitolea inayopatikana katika, “ Jukwa la mahubiri na vyombo vya Habari” { Ukurasa 1} Mama Eddy anasema, “ Mwaka mpya ni mtoto wa kunyonyesha, mtoto kwa wakati, unabii na ahadi ikiwa imevalishwa nguo nyeupe, ikipigwa busu – na kukumbatiwa kwa salamu – ikiwa imejawa na hofu na shukurani.” Kila mwaka mpya, kwa hivyo, waja kwa mwanadamu kwa matumaini na uhakika wa wema! Waja ukipatiana kuachiliwa kutokana na makosa na kuidhinishwa kwa haki; inapatiana mwanzo mpya, ambapo ni jukumu la kila mtu la kuweka ambacho ni cha dhamana na kizuri, kisafi na kitakatifu, kikuu na chenye nguvu – karatasi ambayo kila mtu anatakiwa kuandika ukweli na ukweli pekee. Na nini kingine ila Sayansi ya Kikristo ingewezesha mtu yeyote kutimiza kusudi kubwa kama hii!

Wakati katika maombi matakatifu kiongozi wetu alimuomba Baba wetu wa mbinguni, akiomba usaidizi wake kwa kuandika ukurasa ambao unatakiwa kuwa wa milele kwa sababu ya kuungana kwake na Ukweli, alitawaza mbele yetu maono ya ajabu ya wema unaotarajiwa. Hapa anaonyesha nafasi ambayo ni ya kuvutia. Hapa kuna njia ambayo makosa ya awali yanaweza futiliwa, kufuta madeni, urekebishaji wa makosa, kuachilia tabia za uongo, makosa kurekebishwa, kutubu dhambi na kuzitupilia mbali. Hakuna kitu, ingawa hivyo, ila kufahamu na kudhihirisha Sayansi ya Kikristo ambako kunaweza leta uwezo wa kuchukua mwanzo mpya wenye matumaini, na wenye ufanisi kwenye hatua za maisha, bila kujali chochote ambacho mambo ya awali imekuwa ikidai kuwa au kushikilia; na kando na kuandika “ukurasa wa ukweli usiokuwa na kifo” ambayo inaweza futa yote ambayo yamekuwa ni maovu, ya uongo, na yasiyo kweli katika tajiriba ya kila mmoja.

Na ukurasa kama huu utaandikwaje? Kwanza, hauwezi anziwa bila usaidizi wa Baba. Isipokuwa kazi ifanywe katika roho sambamba na roho ambayo Yesu alijua na kudhihirisha wakati alipotangaza, “ Mimi siwezi Fanya kitu chochote.” na “ Baba anayeishi ndani yangu, ni yeye anayetenda kazi hizi,” hakuna matokeo yanayoweza kufuata. Ila kila mmoja atambue ya kwamba hawezi kua na nguvu za wema ila zile anaangaza kutoka kwa Mungu, Ukweli wa Kimungu, hawezi hata kuanza kuandika ukurasa ule ambao hautawahi futika au kupotea, lakini ambao utasimama milele kwa wale watakousoma.

Pointi ingine ya maana ya kukumbukwa ni kwamba hakuna kitu cha kuwekwa katika ukurasa ule ila ukweli. Yote lazima yaandikwe kulingana na sheria za Kanuni na uwiano na usahihi wa mbinguni. Na hii inadai ufahamu unaoongezeka wa maandiko na roho ya Sayansi ya Kikristo. Inadai kukubali kuchukua kwa sasa kukabiliana na tajiriba za awali ambazo hazijakamilika mpaka yote ambayo iko na makosa inaondolewa na ambayo ni kweli pekee inabaki. Pia inahitaji msukumo kukabiliana na shinda mpya na kujitenga na kuzikabili mpaka suluhisho kamili. Ndipo tu ukurasa mpya unaweza kuwekwa mbali na kuchafuliwa na makosa au kushindwa.

Kama vile Mwanasayansi ya Kikristo anataambua mahitaji haya muhimu, ataanza kwa furaha safari hii ya mwaka mpya. Ni utarajio wa uzuri! Ni furaha kwa hisia ya utendaji upya! Uovu wa awali ukipunguzwa na uwezekano wa wema wa sasa ukiongezeka, anahisi hakuna kitu kinachoweza kuzuia maendeleo ya matarajio ya udhihirishaji. Anafikiria anaweza kuwa na maono ya kutimika kwake! Na ni vizuri kwamba maono ya fikira zake kuwa mapana na yenye umbali; na mtazamo wake kuwa na tumaini na ujasiri; na ajue kutoka mwanzo ya kwamba yote yanawezekana kwa wale wanaoamini!

Ukurasa huu usiokua na madoadoa na kifo ambao atauandika utakuwa umejaa maoni ya ukweli kama vile kila sheria ya Ukweli inaeleweka na kutii. Kila neno linalotumika, kila kitendo kinachorekodiwa, lazima iwe ni matokeo ya mawazo inayotawaliwa na Mungu. Hii mawazo sahihi lazima ishikiliwe katika uaminifu kwa Ukweli ya kwamba yaliyo kweli ndio pekee yanayozingatiwa na kukaribishwa. Kwa uvumilivu mkuu kila wazo linalokabili kukubali lazima lichunguzwe katika mwangaza wa Ukweli, ya kwamba yale ambayo ni sahihi na mema ndio yatapatiwa nafasi.

Ni Furaha aje kujua ya kwamba kupitia bidii ya mwaka ujao sio tu usaidizi wa Baba utakuwa karibu kuwezesha mwanasayansi ya Kikristo kuandika ukweli uliokamilika katika ukurasa wake, lakini pia utamuonyesha vile kufuta kupitia majonzi, toba, na kukubali wema, na makosa hata iliyo ndogo ambayo bila kuzingatia, au kwa makusudi, amedhihirisha hapo awali. Utiifu kwa uvumilivu kwa mapenzi ya Mungu, ambayo itamuezesha kudhihirisha Ukweli ule pekee ni ya kweli, pia itapanguza alama yoyote ya mchafuko kutoka kwa ukurasa msafi wa juhudi zake. Kisha yale tu ambayo ni ya Ukweli yatabaki kutukuza Baba – Mama Mungu, na kuthibitisha umoja wake.

Oh, na maombi ya dhamani ya kiongozi wetu yajibiwe mwaka huu kwa mawazo na maisha ya kila mwanasayansi ya Kikristo!