Nyungu ya mafuta
Kutoka kwa toleo la Aprili 6, 1929 la Jarida la Mlinzi la Sayansi ya Kikristo
Katika sura ya nne ya Wafalme wa pili kuna ujumbe mfupi wa mjane aliyeshindwa kulipa deni yake. Zaidi ya haya, alikabiliwa na madai ya kwamba wana wake wawili wangepatianwa kuwa watumwa ili kuridhisha wenye deni. Lakini alikuwa amekiri imani yake katika Mungu na sababu yake ya kutarajia suluhisho juu ya ugumu wa maneno yake kwa Elisha, nabii, “ Unajua ya kwamba mtumishi wako anamcha Mungu.”
Katika orodha ya maneno katika kitabu cha Sayansi ya Kikristo, “Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko” {Ukurasa 593}, Mary Baker Eddy anapatiana maana ya kiroho ya “Nabii” kama mhubiri; kuangamia kwa hisia za kiasili mbele ya ufahamu wa ukweli wa kiroho.” Elisha akauliza yule mwanamke ni kitu gani alichokuwa nacho nyumbani mwake; na akajibu, “ Hakuna kitu ila nyungu ya mafuta.” Akiangalia mbali na hitaji, na mbali na nyungu ya mafuta, – mbali na kimwili na ushuhuda wa hisia za kimwili, na kutazama wingi wa wema wote, nabii alisema, “ Nenda uombe vyombo kutoka kwa majirani wako wote, hata vile vilivyo wazi;” na akaagiza hasa asiombe “kidogo.” Ni kwa mshangao upi mwanamke yule alisikiliza madai aliyopatiwa siku ile! Hakukuwa na kusita, kugombana, hakuna kulegea kwa madai ya Elisha: “ Wakati unapoingia, utafunga mlango nyuma yako na kwenye wana wako, na utamimina mafuta kwenye vyombo hivi, na utaweka kando ile ambayo imejaa.”
Wakati aliingia katika ufahamu wa uwepo na nguvu za Mungu, na kufunga mlango kwa shida zote, wasiwasi na madai, basi alikuwa “amimine mafuta.” Hakuna shaka alipoenda kwa Elisha kupata usaidizi alikuwa anafikiria ni nini atakachopokea; na akaambiwa “amimine mafuta.” Aliye na maono ya kiroho alikuwa amegeuza mawazo yake kutoka kwa ubinafsi na maslahi ya kibinafsi, hofu, na ukosefu kwa upendo wa Kimungu unaotenda na ulio karibu. Utendaji wa uhakika ulikuwa unahitajika kwake. Alikuwa “amimine” kile alichokuwa nacho pekee kwa nyumba. Wanae hawakuwa wamsaidie. Ukweli, walikuwa na kazi yao kufanya – ya kuleta vyombo vilivyo wazi, vyovyote wangepata. Na wakati kila moja ya hizi ilijazwa, “ mafuta yakabaki” : udhihirisho ukafanyika. Alafu mwanamke akaenda kwa Elisha kuripoti aliyofanya kwa kutii maelekezo yake. Utiifu wake ulikuwa umemtayarisha kwa hatua iliyofuata: “ Nenda, uza yale mafuta, na ulipe deni, na muishi wewe na wanao kwa yale yatakayobaki.”
Mafuta yalikuwa ya thamani siku zile na yalikuwa na matumizi mengi. Natuzingatie matumizi ya neno katika maana yake ya kiroho, kama inavyoonyeshwa katika maelezo ya maneno ya Sayansi na Afya {Ukurasa 592}: “Mafuta,kutakaswa; hisani; upole; maombi; hamasa ya mbinguni.” Christian Scientists of today, tunamimina haya mafuta? Hakuna hitaji kubwa, hofu inayosisitiza, hali ya dharura, lakini katika kila nyumba kupatikane nyungu ya mafuta ambayo inangoja kumiminwa; na kuwe na vyombo ambazo viko wazi, “sio kidogo,” ambazo zinangoja kujazwa. Mioyo inayopenda na mikono iliyo tayari inahitajika ndio hazina ya Ukweli na Upendo imiminwe katika nafasi zilizo wazi.
Kila hali ya ugonjwa au uchochole katika kimwili ni chombo kilicho wazi ambacho kinangoja kujazwa kwa “ hamasa ya mbinguni,” ikingoja maombi ya uthibitisho, shukrani, na pongezi. Kila mwananfunzi wa Sayansi ya Kikristo ako na nyungu ya mafuta ya thamani nyumbani mwake, hata ufahamu wa Mungu, wema, ambao unangoja tu umiminaji kuhakikisha kuweza kukutana na mahitaji yoyote. Mungu ndiye chanzo pekee cha ugavi, na uangalifu wake kwa wana wake haushindwi. Wazo moja la Ukweli katika hekalu ya utakatifu ya ufahamu wa Kimungu, milango ikiwa imefungwa ili kwamba hisia za kimwili haziwezi ingia na mapendekezo yake, ni ya kutosha – kama imemiminwa. Fikiria juu yake! Katika usimulizi wa agano la kale, nyungu ya mafuta ilikuwa alama ambayo kupitia kwake dhihirisho la ajabu la wingi wa Mungu ulitambulikana kupitia ufahamu wa kiroho wa Elisha, mtumishi wa Mungu.
Leo, labda zaidi kuliko hapo awali, kuna haja ya kujitakasa kwa kila laini ya utendaji wa maana. Kuna haja ya hisani, upole, na hamasa ya mbinguni. Uwezo au ustadi wa kufanya kitu , na kufanya vizuri, inaweza kuwa nyungu ya mafuta inayongonja kumiminwa ili kudhibitisha wingi wa wema. “Ni nini ulichonacho nyumbani mwako?” Kuna kipimo cha mafuta ya dhamani, inaweza kuwa imekusanywa kutoka kwa msongo wa mawazo ya majaribu na tajiriba ambayo imeleta ufahamu wa kuendelea kwa ukaribu wa Mungu? Wakati Elisha alimuelekeza mwanamke ya kwamba anatakiwa “kumimina” hata kwa wakati wa hitaji lake kuu, alikariri ukweli muhimu, akapatiana muongozo wa udhihirisho ambao unaweza kufuatiliwa katika kila sehemu ya maandiko, na ambayo inapata onyesho lake kamili katika maisha na kazi ya Kristo Yesu, ambaye alisema kwa wanafunzi wake, “ Toa na itatolewa kwako.”