Ombi la furaha
Kutoka kwa toleo la Oktoba 1922 la jarida la Sayansi ya Kikristo na ELLA W. HOAG
Baada ya Yesu kuwaongelesha wanafunzi wake juu ya umuhimu wa kuishi ndani mwake. – kuishi kulingana na mafundisho yake na kudumisha amri zake alizowapatia, kama alivyodumisha amri za Baba, – aliendelea kusema, “Haya mambo nimenena kwenyu ndio furaha yangu ibaki ndani mwenyu, na ndio furaha yenyu iweze kujaa.” Basi alipozingatia furaha, aligusia juu ya kipengele muhimu katika kazi yoyote yenye ufanisi, na kwa kuonekana ile ambayo inahusu mafanikio ya kiroho. Bila kipengele cha furaha, kazi yoyote inawezakuwa bila roho, ya kuchosha, na isiyo na ufanisi. Kazi isiyo na furaha kwa wakati wote hukosa kuendelea kwa utendaji sahihi, na lazima ife kwa kufilisika kwake.
Sasa, furaha ya kweli ni sifa ya kiroho, na inagusia moyo kwa kuthamini wema wa kiroho. Inaanza baraka yake mapema sana katika bidii ya sayansi ya Kikristo kudumisha amri yake. Hakuna juhudi ndogo kutii lakini ina kiwango chake cha furaha, kwani hakuna kitu kinachojaza moyo wenye ukweli na amani na kutosheka kama ufahamu wa kutii. Mwadishi mwenye hekima wakati mmoja akasema, “ Tunapo ongea kuhusu furaha, sio kitu ambacho tunafuata, lakini kitu ambacho chaja kwetu wakati tunapomfuata Mungu na majukumu yake.” Kwa hivyo furaha ni zawadi kwa wakati wote. Haiji kama haijafanyiwa kazi. Kuwa wenye furaha kwa kweli moyo lazima uwe msafi, lazima uwe unatafuta yale mambo ambayo yanatosheleza. Na ni nini ambayo inaweza tosheleza ila utambuzi na udhibitishaji kwa kiwango cha umoja wa mtu na Mungu, wema wa Kimungu? Hakuna ufahamu wa wema wa kweli lakini waleta mwangaza wa furaha.
Haya yote yakiwa ni kweli, furaha wakati ule ule lazima ilindwe kwa bidii ama inaweza kuonekana kupaa mbali. Haiwezi dumu kwa hali ya ukosefu wa shukrani. Kukosa ufahamu wa wema ni kumaanisha kukosa furaha; kwa hivyo, kutambua na shukrani juu ya zawadi za Mungu lazima ije mbele ya ufahamu wa furaha ya kweli. Mtu pia lazima awe amefunguka juu ya uwepo wake kama ukweli wa kiroho, au itakaa kupotea. Kwa maneno mengine, kama sifa zote za kiroho lazima ipendwe na kuthaminiwa, au hataweza kuwa na ufahamu wa uwepo wake. Furaha pia ni sifa ya utoto. Nani hajaridhishwa na furaha ya watoto wadogo. Na kwa nini tunapata ndani yao furaha yenye kuridhisha? Sio kwa uhuru wao na kuwa mbali na mawazo ya hofu, kuwa kando na majukumu ya uongo; na juu ya yote kwa sababu ya ukosefu wa ubinafsi? Kama wema mwingine wowote wa kiroho, adui mkubwa wa furaha ni ubinafsi.
Isaya anatuambia , “ Kwa furaha mtateka maji kutoka visima vya wokovu.” Kiongozi wetu mpendwa anaongea kuhusu furaha katika maandishi yake. Katika “ Sayansi na afya na ufunuo wa maandiko” {Ukurasa 265} anasema kwamba “ Furaha ni ya kiroho;” lakini hakuna mahali popote ameweka katika kikundi kitakatifu kama alipotupatia mstari mtakatifu katika shairi lake {ukurasa 4} inayojulikana na wanasayansi ya Kikristo: “ Uwepo mpole, amani na furaha na nguvu.” Mara ngapi tumepata maneno yale machache kuwa kisima cha wokovu! Wale wameonja kwa wepesi “ maji ya uhai” yaliyo katika ufahamu unaofumbuliwa wa Upendo wa Kimungu ulio mpole, amani, na nguvu na tunajua vile furaha iko kwa kila wakati – upendo ule ambao ni wa kina kama bahari na wenye urefu na upana kama anga; kwa maneno mengine, furaha ambayo haina utulivu usiovunjwa pekee, lakini mwangaza mkubwa na uhuru na kung’aa. Kwa haya yote tumepata kuona kwa mtazamo mdogo.
Lakini kuna mahali kwingine ambako hatuna haraka ya kutia nguvu uwepo wa furaha. Wakati Yesu anatuambia, “ Wapendwa, ihesabu kuwa furaha ukianguka kwenye majaribu mengi,” alafu tunauliza, naweza pata furaha aje? Kwa kweli uzoefu katika hali kama ile ni kuchukia kutajwa kwa furaha! Wakati majaribu yanaonekana kukusanyika yakizingira mtu, inakaa kama kejeli hata kuzingatia uwezekano wa furaha; ilhali Yakobo anaendelea kutufahamisha kwa nini tuwe na furaha katika majaribu. Anasema: “ Kujaribiwa kwa imani yenyu kunaleta uvumilivu. Lakini uvumilivu uwe na kazi njema, ili muwe wakamilifu bila kuhitaji kitu chochote.” Na kukamilika huku huja “ tukihesabu kama furaha” kukumbana na majaribio mengi.
Kwa kweli zawadi inastahili kwa jitihada. Kwa kweli tunaweza furahia kwa utiifu, “kwa furaha isiyo kipimo,” ingawa aje urefu wa tajiriba, kwa kuwa tunajua kuwa na furaha kati yao, – kwa kusifu Mungu ya kwamba tunapitia ndani mwake – Hii ndio itatutia nguvu na kudumisha mpaka ukamilifu umepatikana. Alafu ni katika majaribu ambapo furaha inakuwa msaidizi wetu; kwa sababu inatubeba juu ya vizingiti vyote, inatuongoza kwa shangwe katika kila matatizo, na kutuhimiza kuendelea mbele bila kujali vizingiti vyovyote mpaka ushindi umepatikana.