Peke yangu na Mungu
NA MUSA ICHADO
Wapendwa,
Ningependa kuwahadithia hadithi hii fupi ya nabii Danieli. Nimehamasishwa kuandika hadithi hii ndogo juu ya Danieli wakati nilkuwa nasoma Sayansi na Afya na maisha ya Danieli katika Bibilia.
Kuwa peke yako na Mungu inakuwezesha kumjua Mungu kwa njia ya kweli na kuona yale anaweza Fanya. Kwa wakati mwingi tunatubu ya kwamba Mungu anaweza fanya kila kitu, bila kuiamini kwa udhabiti. Hisia yetu ya matarajio ni nadra. Lakini, “watu ambao wanamjua Mungu wao watakua na nguvu, na watafanya makuu.” { Danieli 11} Kunjua Mungu kwa njia ya kweli huingiza nguvu katika utu wako.
Utakua na nguvu kufanya makuu. Hii ndio ilikuwa hali ya nabii Danieli. Alikuwa mtu aliyejua hali ya kuwa pekee na Mungu. Ni ushindi wa aina mingi ambao Mungu alileta kupitia kwake! Mungu anaweza fanya vile vile kupitia mtu yeyote ambaye atamtafuta.
Kulikuwa na tukio hili kuhusu ndoto ambayo Nebukadneza alikuwa nayo, lakini akasahau. Hakuna watu wenye hekima katika nchi ambao wangeweza kutafsiri ile ndoto. Danieli alishauriana na wapendwa wake ili kuutafuta uso wa Mungu juu ya jambo hili, baada ya kumuambia mfalme ya kwamba atapata tafsiri kutoka kwa Mungu. “Alafu ndio siri ilifumbuliwa kwa Danieli katika maono ya usiku. Alafu Danieli akambariki Mungu wa mbinguni.” {Danieli 2}
Danieli alikuwa na akili ya Mungu kwa sababu alimpenda Mungu wake, na alichukua mda kuwa naye peke yake. Kama uko katika uwepo wa Mungu, ukitafakari na kuwaza juu ya ukuu wake, imani yako hujengeka.
Pole pole utajipata umejawa na imani ya kutosha ya kuamini Mungu kwa kitu chochote. Hii inaweza kuwa ya kweli kwako. Unaweza jawa na ufahamu wa mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho. Wapendwa, wakati umewadia kufahamu ya kwamba Mungu alimzawadia Danieli, mtumishi wake ambaye alichukua mda kuwa peke yake naye, akiomba ili apate neema, ufahamu na ufunuo wa kimungu.
Kuwa peke yako na Mungu, kunamaanisha “ kuvalia silaha kamili ya Mungu,” ambayo itakufanya kuwa salama. Chukua upanga wa Roho ambao utakufanya usionekane; na uenende katika imani na ujasiri mkuu wa kukabiliana na adui yako.
Funga uovu katika jina la Yesu na utafungwa. Tangaza, na itaimarishwa. Ukisimama kuhesabiwa, ukijipatiana kwa bwana kuwa shujaa wa maombi, atakutumia, na maisha yako yataleta baraka zisizoeleweka kwa watu wengi, na sifa kuu kwa Mungu.