Tangazo la siku ya kunyenyekea
Iliyoandikwa na Abraham Lincoln
Tangazo la siku ya Kunyenyekea, Kufunga na Maombi la 1863
Ambapo, seneti ya Marekani, inatambua kwa uaminifu mamlaka kuu na serikali ya haki ya mwenyezi Mungu, katika shughuli zote za wanadamu na mataifa, imefanya kwa ,azimio , imemuomba rais kuteua na kutenga siku ya maombi na kunyenyekea kwa taifa;
Na ambapo, ni wajibu wa mataifa, na pia wa wanadamu wote kumiliki utegemeaji wao juu ya nguvu za utawala za Mungu, kutubu dhambi zao na makosa, kwa unyenyekevu na huzuni, hata hivyo kwa tumaini la uhakika ya kwamba toba ya ukweli itaelekeza kwa rehema na msamaha, na kutambua ukweli mkubwa unaotangazwa katika maandiko matakatifu, na inayodhibitishwa kwa historia yote, ya kwamba mataifa yale tu yamebarikiwa ni yale Mungu ni Bwana.
Na,kama tunajua yale,kupitia sheria ya Kimungu, mataifa kama watu binafsi wanakabiliwa na adhabu duniani, hatuwezi kuwa na hofu ya majanga mabaya ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaharibu nchi, inaweza kuwa tu adhabu iliyowekwa juu yetu kwa sababu ya dhambi za dhihaka, kwa hitaji la kukamilisha urekebishaji wa taifa kama watu waliokamilika? Tumekuwa wapokevu wa chaguo bora la mali ya mbinguni. Tumehifadhiwa, miaka hii mingi, katika amani na ufanisi. Tumeongezeka kwa idadi, utajiri na nguvu, kuliko vile taifa lingine lolote lishawai kuwa. Lakini tumemsahau Mungu, tumesahau mkono wa rehema uliotuhifadhi katika amani, na ulifanya tuongezeke na kututajirisha na kutuweka nguvu; na tulidhani bure, kwa udanganyifu wa mioyo yetu ya kwamba hizi baraka zote zilitolewa na hekima ya juu na uzuri wetu. Kama tumelewa na ufanisi usiovunjika, tumekuwa wa kujitegemea sana kuona haja ya kukomboa na kuhifadhi neema, wenye kiburi hata kuomba kwa Mungu aliyetuumba!
Inatubidi basi tunyenyekee mbele ya nguvu zilizokosewa, kutubu dhambi zetu za taifa, na kuomba kupata huruma na msamaha.
Kwa hivyo sasa, katika kuzingatia ombi, na kwa kukubaliana kwa kikamilifu na maoni ya Seneti, kwa tamko hili, ninateua na kutenga siku ya Alhamisi, Aprili 30, 1863, kama siku ya kunyenyekea ya taifa, kufunga na kuomba. Ninawaomba watu wote wasitishe shughuli zao za kawaida, na kuungana katika mathehebu yao ya maombi na manyumbani mwao, katika kuweka ile siku takatifu kwa Bwana, na kujitolea kwa kazi nyenyekevu ya wajibu wa dini kwa tukio hili muhimu.
Haya yote yakifanywa kwa uaminifu na ukweli, acha tupumzike kwa unyenyekevu katika matumaini, iliyoidhinishwa na mafundisho ya kimungu, ya kwamba kilio kilichoungana cha taifa kitasikika juu mbinguni na kitajibiwa na baraka, sio chini ya msamaha wa dhambi za taifa, na urejesho wa taifa letu ambalo limetawanyika na linateseka kurudi kwa hali yake ya mbeleni ya furaha ya umoja na amani.
Katika kuweka Ushahidi, nimeweka mkono wangu na kupiga muhuri wa Marekani.
Imefanyika katika jiji la Washington, siku hii ya 13, Machi katika mwaka wa Bwana wetu elfu moja mia nane sitini na tatu, na uhuru wa Marekani themanini na saba.