Tatizo ufahamu
au Suluhisho – Ufahamu
NA PARTHENS
Zaburi 25, mstari wa 10, ni mfano mwingine wa hali ya asili ya ahadi za Mungu. Inasema, “Njia zote za Bwana ni za huruma na ukweli kwa wale wanao hifadhi agano lake na ushuhuda.”
Kila changamoto inayodai kukesha, maombi, vita vya kiroho kila wakati hujumuisha kuhama kwa akili kutoka kwa ufahamu wa tatizo mpaka ufahamu wa suluhisho. Kuangazia shida ni makosa. Kuangazia suluhisho la tatizo ni Ukweli. Hali hizi mbili za akili zinapingana: Moja inavunja ahadi na ingine inaweka ahadi. Ushindi unahakikishwa nikienda juu zaidi, nikielekeza akili yangu {na hisia} kwenye suluhisho, nikikataa kuzama kwenye tatizo.
Kwa wale majasusi kumi na mbili walio patiana ripoti ya mpango wa nchi ya ahadi, wawili tu ndio walikuwa wa suluhisho na kuleta ripoti nzuri. Wengine wa majasusi walikuwa na mwelekeo wa matatizo kufikia kukata tamaa.
Kama Churchill alitangaza, “Hofu ni majibu. Ujasiri ni uamuzi.”
Mwalimu aliwahimiza wanafunzi kuwa na hekima kama nyoka, ikimaanisha, kamwe usikubalishe imani ya uhai na hisia katika kimwili kuweka kimya kinyume, sayansi ya uwepo.” { Sayansi na afya, toleo la kwanza, ukurasa 250}
Kumi mwa wale majasusi kumi na mbili “waliweka kimya sayansi ya uwepo” na matokeo hatari. Hofu huweka kimya sauti ya Malaika wanaoshikilia kifunguo cha suluhisho la kila tatizo linaloweza kufikiriwa na mwanadamu.
“ Tuliona majitu…na tukajioana kama nzige, machoni mwao.” { Hesabu 13:33} Hivyo kama wale majasusi kumi waliweka macho yao kwa ushuhuda wa uongo wa hisia zao tano, kukata tamaa kwao kukaongezeka: hawakujiona tu kama wadudu wanaoweza kusagwa , lakini wakawafikiria adui zao wakitazama Israeli kama mawindo rahisi pia.
Mfano unaofanana wa utumiaji mbaya wa mawazo unaonekana katika apokalipsi ya Yohana, wakati akili ya kimwili imeifanya kuwa kubwa nyoka ya Mwanzo kuwa joka ya mraba mkubwa.
Kama usemi unasema:
“ Wanaume wawili waliangalia nje kupitia dirisha yenye vyuma ya gereza: Mmoja Aliona matope, na mwingine akaona nyota.”
Majasusi wawili wa Israeli waliona “nyota” – kwa jina uwezo wote,uwepo wa kila mahali, uwezo wa kujua yote, na utendaji wote – na tatizo la “majitu” likatokomea: kwa kutokuwepo kwake.