Tofauti zilizoko kati ya Plainfield na Boston |

Tofauti zilizoko kati ya Plainfield na Boston


Tunaelewa Mary Baker Eddy kuwa ni yeye mwanamke aliyetabiriwa katika sura ya 12 ya Ufunuo.

Kanisa la Plainfield lilifukuzwa zamani. Unaweza soma kuhusu “Historia ya uhuru wetu” hapa {kiungo}. Uhuru wetu umekuwa matamanio ya kurudi kwa Sayansi ya Kikristo iliyo safi kama ilivyofundishwa na Mary Baker Eddy.

Tunashikilia toleo la 88 la mwongozo wa kanisa na toleo la 1910 la Sayansi na Afya na funguo la maandiko ya Bibilia. Matoleo haya yaliidhinishwa na Mary Baker Eddy wakati wa uhai wake na haijachakatwa na shirika.

Tunashikilia vile Mama Eddy alisema kwa makala hii hapa {kiungo} kuhusu dhana ya” maandishi yaliyoidhinishwa” na kujua ya kwamba kila mtu binafsi “ako na uwezo wa kuchagua chochote atakacho kisoma.” kwa sababu kila mtu ako na hisia za kiroho za kusikiza na kutii Mungu bila uangalizi wa kibinadamu.

Tunatoa tu maandishi yaliyo bora ya Sayansi ya Kikristo, na baadhi yake ni ya wale waliofanya kazi nyumbani mwa Bi Eddy na walifunzwa moja kwa moja na yeye. {Bonyeza hapa kwa makala} na {bonyeza hapa kwa vitabu|.

Tunaandika masomo yetu, tunachapisha jarida na vitabu zetu na kuendesha tovuti yetu sisi wenyewe na tunapatiana yote tunayoweza kwa dunia bure.

Tunakesha kulingana na amri ya Kristo Yesu:”Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote, kesheni.” {Marko 13:37} Zaidi ya hayo hii {kiuongo} inaonyesha vile kukesha ilikuwa ni muhimu kwa Bi Eddy.

Tunawahimiza washirika wetu kusoma na kutafiti toleo la Mfalme Yakobo la Bibilia na vitabu vya Mama Eddy ambazo zimechapishwa na ni Sayansi na Afya na ufunguo wa maandiko na kazi za insha na pia kazi yoyote ya Sayansi ya Kikristo ambayo wanawezafaidika nayo; na zaidi ya hayo tunatarajia waonyeshe na waishi kwa sayansi hii kila siku na kuelewa ya kuwa kulingana na matunda yetu ndio tunajulikana na kwa kazi zetu ndio tunadhibitishwa ama kuhukumiwa.

Tunawahimiza washiriki wetu kujifahamisha na maisha ya Mary Baker Eddy na historia ya kanisa lake, ndio waweze kuwa waponyaji na wanfanyikazi wanaostahiki sayansi hii. Tunapatiana tu maelezo ya maisha yake yaliyo bora na sahihi. {kiungo}

Hakuna ambaye anafukuzwa ama kushtumiwa kwa kutafuta msaada wa matibabu.

Hakimiliki 2025 ya Kanisa huru la Sayansi ya Kikristo la Plainfield