Umaakini
Kutoka kwa toleo la Februari 19, 1927 la mlinzi wa Sayansi ya Kikristo na Mary T. Johnson
Jina “maakini” inatokana na jina la kifaransa alerte, kwa kiasili a l’erte, “katika kukesha,….{kusimama} kwa urefu, ambapo mtu anaweza tazama kwa mzunguko.” Pia inaashiria uangalifu, kuwa macho, na kuwa tayari kwa Kutenda mara moja. Kusimama inamaanisha utendaji katika kudumisha mizani, uthabiti, na usawa. Kusimama mahali ambapo mtu anaweza tazama kwa mzunguko inapendekeza urefu wa juu, mwinuko, mahali penye juu pa kutazamia.
Mtazamo wa aina ile wa neno unakumbusha picha ya walinzi wale waaminifu ambao kutoka nafasi za amri juu ya mlima au mahali kwingine ambako kumeinuka, anaweka macho yenye kutazama kwa kuendelea juu ya maeneo kubwa ya msitu. Ni wajibu wao wa kugundua pumzi za kwanza za moshi ambazo zinaonyesha kuanza kwa moto unaochoma msitu, na kuchukua hatua za dharura za kuuzima. Hivyo unaokoa kila mwaka mbao za thamani na labda maisha ya wengi wanadamu.
Katika muongozo wa kanisa la kwanza la Sayansi ya Kikristo {ukurasa 42} chini ya Kichwa, “Umaakini katika wajibu,” Mama Eddy anasema, “ Itakuwa wajibu wa kila mshirika wa kanisa hili kujikinga kila siku dhidi ya mapendekezo ya kiakili yenye ukali, na wasifanywe kusahau wala kuachilia wajibu wao kwa Mungu, kiongozi wake na kwa wanadamu.” Wanafunzi wanaoanza masomo ya Sayansi ya Kikristo mara nyingine hushangaa vile mtu ataweza kujikinga kwa njia yenye ufanisi. Katika jina “umaakini” inaweza patikana ufunguo.
Wakati mtu yupo katika mahali palipo juu, anaweza kuona vema; maono yake haijazibwa na vizuizi vya maada; upeo wa macho ni mpana zaidi, mtazamo wake una uzuri zaidi. Ili kufika urefu wa kiroho ambao atasimama juu yake na kutazama kwa mzunguko wake, lazima atainuka juu ya ushuhuda wa hisia za maada. Mtu hufanya haya kwa kufikiria asili ya Mungu, mwenye nguvu zote, aliye kila pahali, na mwenye Akili yenye kujua yote, na juu ya mwanadamu wa kweli, aliyeumbwa kwa umbo na mfano wa Mungu. Maono kama yale yanapatikana kwa kukubali, kwa ufahamu na imani, ukamilifu wa Mungu, wema, na kukataa kwa kusisitiza na uthabiti uwezekano wa nguvu ingine yoyote na uwepo; kwa kukataa kukubali ushahidi wa hisia za maada, na kwa kupanda mwenyewe kwa udhabiti bila kutingika juu ya ushahidi wa hisia za kiroho. Hivyo ndivyo tunapofika “ mahali palipo fiche pa aliye juu,” mahali palipo juu ambapo tunaweza tazama ulimwengu ulioumbwa na Mungu.
Kutoka sehemu hii ya juu ya kuangalia ya ufahamu wa kiroho, ni nini kinachoweza kuonekana? Kama Mungu ndio uwepo pekee, nguvu pekee, ukweli pekee, lazima tumtafute Mungu. Mungu anaweza kuwa adui ya kile ambacho anaumba? Hii haiwezi fikirika. Katika Mungu tunapata wema pekee, usalama pekee, ukamilifu wa kudumu pekee. Kwa kuwa uovu sio sehemu ya uumbaji wa Mungu, lazima tuwe maakini kuona na tayari Kutenda juu ya maagizo ya Mungu, tukikataa kila madai kinyume na wema.
Tunaambiwa tujikinge “ kila siku dhidi ya mapendekezo makali ya kiakili.” Yanatoka wapi mapendekezo haya? Kwa kuwa kuna Akili moja, Mungu, na kwa kuwa Mungu ni mwema kila wakati, hakuwezi kuwa na akili ambayo mapendekezo ya uovu yanaweza patikana. Tujikinge dhidi ya nini? Kutokana na imani zilizo na makosa na hitimizo zisizo sahihi. Hakuna adui mwingine. “Uovu sio mtu, mahali, wala kitu” {Sayansi na Afya na ufunuo wa maandiko, na Mary Baker Eddy, ukurasa 71} ; ni uongo, undanganyifu. Na ni katika ufahamu usio wa kweli ambao hudai kuwa na utu kando na Mungu ambapo mpinzani lazima akumbwe na kudhibitisha sio wa kweli. Katika imani zetu zilizo za kielimu katika kiumbe kinachompinga Mungu, wema, lazima tujikinge wenyewe.
Hii kazi lazima ifanywe kila siku, hata kwa kila saa. Kuweka kando mzigo mzito wa imani zilizo potofu, maoni, nadharia, na falsafa zinadai kazi ya mara kwa mara na yenye mpangilio, na iliyo kamilifu, ambayo mwana sayansi wa kweli anashiriki na furaha inayoongezeka msukumo wa ghafla. Anajua ni kupitia bidii ya kuaminika ataweza kutazama ulimwengu wa Mungu na kutangaza na mfunuo, “ Nilisikia sauti kubwa ya watu wengi mbinguni, ikisema, Alleluia; Wokovu, na ukuu, na heshima, na nguvu, kwa Bwana Mungu wetu.”