Umiliki |

Umiliki

Na ADAM H. DICKEY


Kuna imani kati ya wanadamu ya kwamba wanaweza kuwa wenye haki maalum ya kumiliki kitu. Wakati kupitia njia ya kawaida ya sheria mtu anapata mali isiyo hamashika, yeye hupata hamu kubwa ya kuweka ukuta ambao unaizungukia ile mali na kuwaweka wengine mbali. Baadaye hufuata imani ambayo inakubalika ulimwenguni, ya kwamba anamiliki kipande cha ardhi na kwamba sheria inahifadhi na kumkinga kwa umiliki ule wa binafsi. Yeye hujenga nyumba na kuishi ndani na kuiita yake, na hakuna anayeruhusiwa kuikaribia au kuingia kinyume na matakwa yake bila kuchukuliwa kama mhalifu. Katika kiwango chetu cha sasa cha maendeleo, inaeleweka kwa ujumla ya kwamba mali ni kitu ambacho lazima kiwe na mwenyewe; ya kwamba dunia na yote yaliyomo yanaweza gawanywa katika vipande na sehemu, na kwamba watu tofauti binafsi wanaweza dai umiliki ya wingi au udogo wake na kutenga wengine. Haya yote hata hivyo inalingana na dhana ya kwamba kimwili ni dutu na kwamba binadamu ni mmiliki wake.

Kupitia michakato midanganyifu ya imani za kimwili, ukweli unageuzwa; mawazo yanatolewa nje kuwa vitu, na hizi vitu zinadaiwa, zinashikwa na kutawaliwa na watu binafsi. Watu wengine wako na mali mingi, wengine wako na kidogo, na wengi hawana mali hata kidogo. Hii ionekanayo kama mgawanyo wa mali usio sawa wa mali unasababisha wivu na ugomvi, mara nyingi ikichochea mwenye kujipata amenyimwa matamanio ya moyo wake kutumia mbinu za kutatanisha, kama sio za nguvu za mwili, kufikia lengo lake. Ni salama kusema tisa juu ya kumi ya vita vyote na ubishi duniani zimeanzishwa na kufanyika kwa sababu ya uvamizi wa ijulikanayo kama haki ya umiliki wa mali, au kwa sababu ya hamu ya kuongeza umiliki wa mali au utawala.

Mara tu mtu anajipata amemiliki kiasi fulani cha mali, – cha nyumba au shamba, cha hisa au mashirika ya fedha,- yeye huzungukwa na hisia ya wajibu binafsi kwa mali yake na hofu ya kuwa anaweza nyang’anywa. Mfumo wote wa haki za mali na ugawanyaji wa mali unatokana na kuonekana kwa uzito wa kimwili, udanganyifu ambao lazima siku moja utaondolewa na sheria ya Mungu, ambayo inatangaza ya kwamba akili ndio dutu pekee. Haya mabadiliko hayaji mara moja, lakini kwa mawazo sahihi na maadili itaimarishwa kwa siku zijazo dhana ya kweli, kwa jina, ya kwamba “Dunia ni ya Mungu, na ukamilifu wake,” Tukiongea kwa usahihi, kila kitu katika dunia kinamilikiwa na Mungu na kupitia uakisi kinamilikiwa na binadamu pia, ambaye ni mfano wa Mungu. Wakati tumefika kwenye hatua katika udhihirisho wetu ambapo tunaweza tatua vitu kuwa mawazo, kuongezeka kwa mawazo haya itawezekana ili kwamba kila mtu binafsi ataakisi na kumiliki yote ambayo inamilikiwa na muumbaji wake. Katika mistari miingine ya mawazo, hali hii halisi tayari inatawala; kwa mfano katika ithabati. Hebu tuone ya kwamba tarakimu zinazotumiwa kufanya hesabu, badala ya kukubalika kama mawazo, ilionekana kama vitu vya kiasili. Katika hali kama hii, kila mwana ithabati au mhasibu angefaa kujipatia ugavi wa tarakimu, zile ambazo labda zingekuwa zimetengenezwa na nyenzo inayodumu kama mbao au chuma, na ambayo angeweka kwa rafu au imefungiwa kwa kabati. Wakati mwanahisabati angependa kutumia tarakimu zile, angezitoa nje, kuzipanga kwa mpangilio sahihi, na kuwezeshwa kusuluhisha tatizo lake.

Ikiwa katika msimu wenye kazi mingi ugavi wa mhasibu wa tarakimu zitakuwa zimeisha, ingembidi anunue zingine au labda aombe zingine kutoka kwa jirani yake. Anaweza mkaribia mfanyi kazi mwenzake na kumwambia, “ Ninatamani ungalinikopesha tano mbili ama tatu na saba kadha asubuhi hii; tarakimu hizi zimeniishia.” Marafiki wake wanaweza mjibu, “ Samahani ,lakini nimekuwa nikitumia tano mingi na saba hivi karibuni katika kazi yangu ya kwamba nahitaji nilizonazo nasiwezi kukukimu.” Hata kunaweza kuwa na uhaba wa tarakimu ambao unaweza athiri watu wote na kunaweza kuwa na kung’ang’ania kwa ugavi. Bei ya tarakimu inaweza panda, na kama watu wangeamini ya kwamba vitu hivi ni vya umuhimu, kungekuwa na mashindano makali ya kwamba bei ya tarakimu za kutosha za kufanyia biashara ingekuwa imepotoka kwa bei ya uzalishaji na wangeziacha.

Hali ya shughuli hata hivyo haiwezekani kwa sababu ya ukweli ya kwamba tarakimu badala ya kuwa vitu ni mawazo, na kwa hivyo ziko kila mahali bila upungufu au kizingiti. Hakuna mipango ya akili za kimwili au muandamano wa kudhibiti inaweza chukua tarakimu hata moja kutoka kwetu au kuzuia upatikanaji kwa yale yote tunawezataka kutumia. Hakuna vita ambayo ishawai tangazwa kwa sababu taifa moja limejilimbikiza zaidi ya ugawi wake wa meza ya kujumlisha, wala mtu yeyote kupatikana na hatia ya kutumia tarakimu ambazo amechukua kwa siri kutoka kwa jirani yake.

Tarakimu sio vitu lakini ni mawazo; ni dhana za akili, na kwa hivyo zinapatikana kwa kila mtu. Wakati mwingine itatambuliwa ya kwamba haya sio kweli tu kuhusu tarakimu, lakini kila kiitwacho chombo cha kiasili katika ulimwengu ni bandia ya wazo la kimungu na sio vile akili ya kimwili huionyesha kuwa. Wakati waja akili za kimwili zitaachana na imani yake ya kwamba mawazo yanawakilishwa na vitu vya kiasili,na wakati huu ukiwadia hakutakuwa na hofu ya kupoteza , au kuharibika kwa yale tunaelewa kama wazo na sio kitu. Tutaweza kutambua vile Yesu alimaanisha aliposema, “Usiweke utajiri wako duniani, ambapo mende na kutu zinaharibu, na ambapo wezi watavunja na kuiba: lakini weka utajiri wako {mawazo sahihi} mbinguni, ambapo mende wala kutu haziwezi haribu, na ambapo wezi hawawezi vunja na kuiba.”

Unaweza uliza haya yote yanahusu nini udhibitisho wetu wa sasa. Ni kiasi kikubwa. Wanasayansi ya KIkristo wanaweza ongeza kwa amani yao ya akili na uhuru kutokana na wajibu kwa kufikiria kwa njia na kuendelea Kuweka kwa utendaji wa haraka mafundisho ya Sayansi ya Kikristo. Kama mtu amejishughulisha kwenye biashara ambayo anaamini ni yake, ambayo anafikiria ni yeye ameiumba na kuimiliki, na kuwajibika kwa ufanisi wake, kunaweza kuwa na hisia za mzigo ulioambatana na nafasi ile. Anaweza tatizika kutokana na biashara mbaya, kukosa biashara, au kutokana na Imani zozote ambazo zinaambatana na kazi yake; mradi tu anahisi ya kwamba biashara ni yake pekee, hatakuwa huru kamwe kutoka kwa imani zingine zisizohesabika ambazo zinatakiwa kuathiri biashara kwa jumla na kazi yake hasa. Dawa ya hali hii ni yule mtu aanze kutangaza na kujua yote ni Akili na mawazo ya Akili; Ya kwamba hakuna kitu chochote kidogo au cha kimwili kuhusu biasara yake. Kama Mungu ndiye muumba wa yote, na kama kila kitu ulimwenguni ni chake , basi hii biashara ambayo huyu mtu anaiita yake ni yake Mungu na mtu yule na kuwa mkubwa wa ile biashara kwa kiwango ambacho anaendanisha mawazo yake na shughuli zake za kila siku kwa sheria ya Mungu. Akitambua haya, na kutumia ufahamu wake wa kanuni ya Sayansi ya Kikristo kwa kazi yake, hofu yake na kukosa uhakika zitaangamia. Atajipata akiedesha biashara vile Mungu anataka ifanywe, na atatumia utawala na udhibiti juu yake kwa kiwango cha vile amejiweka chini ya mwelekeo usio na makosa wa Akili ya Kimungu.

Kama mwanamke anajichukulia kama mwenye nyumba na kila kitu kilichomo ni chake; kama anaamini ako na Samani na vifaa ambazo ni mali yake; kama ako na hisia ako na watumishi wa kusimamia na lazima awadhibiti yeye mwenyewe na juu ya kifaa kigine chochote cha nyumba, anaweza kuwa na mzigo mkubwa wa majukumu hata kujipata duni kudhibiti hali ile. Lakini kama ako tayari kukubali Mungu kama mtawala wa nyumba yake, kubadilisha vitu kuwa mawazo na kuelewa ya kwamba vitu zote ziliumbwa na Mungu; na bila yeye hakuna kitu kiliumbwa ambacho kiliumbwa;” Kama anaweza tambua ya kwamba akili ya kimungu inatawala na kudhibiti watumishi wake,nyumba yake na kila kitu kinachojumuishwa, atapoteza mara moja hisia za kujali, hofu, na kuchanganyikiwa, na kupata sheria ya kimungu ya amani na uwiano imechukua umiliki wa nyumba yake na inaisimamia.

Akigundua ya kwamba watumishi wanamfanyia Mungu kazi na sio yeye, na kwamba kila kitu kuhusu ile nyumba kimeundwa kuonyesha sheria ya ukamilifu, mambo yataenda sambamba zaidi kwa wote wanaohusika na ile nyumba, na amani na furaha zitakuja kwa wale watakaoingia mle.

Kuna awamu ingine ya umiliki ambayo labda ndiyo yenye nguvu katika imani ya kimwili. Wazazi wanaamini ya kwamba wao ndio wenye haki maalum ya kuumba kitu; ya kwamba wanaweza hodhi nguvu ya kuumba ya Akili takatifu na kupata Watoto wao wenyewe, ambao kulea kwao, elimu, na ustawi wa mustakabali wao wako na jukumu lake. Hisia hii kwa wazazi hufungua mlamgo ulio wazi kwa mapendekezo ya kutofaulu, na majaribu na dhiki ambazo zinatakiwa kuambatana na umiliki na udhibiti wa watoto zinawashambulia kutoka pande zote. Lazima waelewe ya kwamba Mungu ndiye Baba na mama pekee; ya kwamba binadamu ni kizazi cha Mungu; ya kwamba yeye si wa kimwili na wa undongo, lakini wa kiroho, akiakisi na kuonyesha hekima, upendo na maarifa ya uwepo usio na mwisho. Mara tu wazo hili linapitiwa , hisia ya uongo ya majukumu ambayo akili za kimwili zimewekelea wazazi zinaondolewa, na wanaweza kwa njia inayofaa amini Mungu kuwachunga Watoto wao, wakijua hakuna kitu kinachoweza ingilia kati ya matokeo iliyo na uwiano ambayo inaambatana na ulinzi wa kimungu.

Yote inamilikiwa na Mungu; hatumiliki kitu chochote. Binadamu sio muumbaji wala mmiliki. Kama wanasayansi wakristo tunaweza anza utambulizi wa haya mara moja, na matokeo yatakuwa ya haraka na ya kutosheleza. Lakini tunapoachilia mawazo yote ya umiliki, hii haimanishi ni lazima tutoe kila kitu ambacho kina dhamani kwetu au tutanyimwa kitu chochote. Kwa kinyume, inamaanisha, kupitia kuongezeka kwa ufahamu ya kwamba yote ni Akili na mawazo ya Akili hatimaye tutakuja kumiliki yote ambayo ni muhimu. Hii kwa kweli ni njia inayoridhisha kuleta Mungu kwa tajiriba yetu badala ya kushikilia ndoto za kimwili. Tendo tu la kuachilia kitu sio wema, wala hakuna faida kuchukua hisia ya uongo ya unyenyekevu. Ni kweli ya kwamba ni mengi ya kuachilia, lakini wakati wote ni mambo ya zamani, Imani zisizotosheleza ambazo tunaachana nazo, na kama zinaondoka , zinabadilishwa na mawazo sahihi, ambazo zinatupatia hisia kuu ya uhuru, nguvu na umiliki ambayo hatujawai kuwa nao.

Yesu alimaanisha nini kwa kauli hii, “Yule ambaye anayo, kwake atapatiwa: na yule ambaye hana, kwake itachukuliwa hata kile anacho.” Kwa nini hii: ya kwamba yule ambaye ako na wazo sahihi ni yeye ambaye ” anayo” na mali yake itaongezeka; wakati yule ako na mawazo mabaya ni yeye ambaye “hana,” na ni lazima kwa umuhimu kupoteza hata yale ambayo anakaa kuwa nayo. Yale ambayo tunatakiwa kufanya, basi, ni kubadilisha mbinu za mawazo yetu. Usemi wa Yesu, “Utafute ufalme wa Mungu, na utakatifu wake; na hizi vitu zingine utaongezewa,” inawezekana kupitia Sayansi ya Kikristo.

Katika ukurasa wa 62 wa “ Mikusanyiko ya maandiko,” kiongozi wetu anasema, “Nikishikilia wazo sahihi kuhusu binadamu katika akili yangu, naweza boresha yangu, na binafsi za watu wengine, afya na tabia.” Mambo yote yanatimika kupitia wazo sahihi, ambayo inajizatiti katika ufahamu wa binadamu na kutuondolea imani zetu za uongo. Kitu pekee ambacho kinaweza fanyika kwa hisia za kibinadamu za vitu ni kwamba inatoweka kwa kiwango ambacho tunashikilia wazo sahihi.

Ni sheria ya metafizikia ya kwamba mawazo hujionyesha kwa nje. Kwa hivyo wazo sahihi katika Sayansi ya Kikristo kiasili inapanuka kuwa imisho na kuleta mawazo udhihirisho. Wakati tunafikia mtazamo ambao tunaweza kuona vitu zote za kimwili kama imani pekee, na kwamba hizi imani zinaweza geuzwa na kuboreshwa kupitia kushikilia wazo sahihi, tutaweza kuleta kwenye tajiriba yetu vitu ambazo zilisemwa na Paulo wakati alisema, “ Ambayo macho haijaona, wala sikio kusikia, wala kuingia kwa roho ya mwanadamu, vitu ambavyo Mungu ametayarishia wale wanao mpenda.”

Hoja ingine ya mawazo ambayo inajipendekeza wakati huu ni kwamba wanadamu huamini wana umiliki wa akili ambayo wanaita yao, na kwamba wanaweza fikiria na wafanye watakavyo kwa kulingana na akili hii. Imani hii inaelekeza kwa hitimisho mbaya, linaloitwa ya kwamba tuko katika umiliki wa mwili ambao ni wetu, ya kwamba tuko na macho yetu, masikio, mapafu na tumbo ya kibinafsi, yote ambayo tunaamini kuwa ya kimwili na tuko na jukumu ya ustawi wake. Wakati uovu huu unatumiliki, kitu kinachofuatia ambacho akili ya kimwili inadai ni uwezo wa kukatisha kuona, kusikia, na kadhalika na ya kwamba tumbo yetu inaweza vurugika au kuwa na ugonjwa. Hii yote ni juu ya imani ya muumbaji mwingine kando na Mungu, maarifa na nguvu ingine ambayo tunapatia utiifu. “Enyi mnajua,” Paulo anasema, “ ya kwamba yule mnayejipatia kwake kama watumishi kutii, nyinyi ni watumishi wake.” Dawa ya magonjwa ya mwili ni kusahihisha imani ya uongo inayoyazalisha kwa kuleta mawazo sahihi. Katika ukurasa 415 wa Sayansi na Afya kiongozi wetu anasema: “ Tazama vile wazo linafanya uso kuwa na kijivu. Haisimamishi mzunguko wa damu au kuuharakisha ukisababisha shavu isio na rangi. Kwa njia kama ile wazo linaongeza au kupunguza unyevu wa viungo, kazi ya mapafu, ya tumbo na moyo. Musuli, ukisonga kwa haraka au polepole na kuhamasishwa au kupoozwa na mawazo, inawakilisha utendaji wa viungo vyote vya mwili wa mwanadamu ikiwemo akili na viungo vya ndani. Kutoa uovu unaoleta ugonjwa, lazima utulize na kuelekeza akili ya kimwili na Ukweli wa milele.”

Katika mbinu ya akili ya kimwili, mawazo yanatolewa nje kama ya kimwili na yanaitwa mwili. Wakati tunaelewa haya na kushika yale Mama Eddy anafundisha kuzingatia kutolewa nje kwa mawazo, tutaona kwamba miili yetu sio kitu zaidi ama chini kuliko onyesho la nje ya mawazo yetu. Kwa hivyo kuponyesha ambayo inakaa hali ya ugonjwa ya mwili, lazima tuachilie mawazo yake ya kuwa kama ya kimwili na kutambua ni matokeo ya akili, hali iliyoumbwa na hisia za kimwili, usahihisaji wake ambao, kwa kubadilisha imani za uongo na mawazo ya kiroho, itakuwa kulingana na sheria za Mungu yataleta afya na uwiano.

Mungu ni yeye muumba pekee, na yale yote anaumba lazima iwe kama yeye. Binadamu kuunganishwa kwa mawazo sahihi, Kikundi cha mawazo ya Mungu ambayo inajumuisha haya mawazo sahihi. Kujua ni uwepo; “kwa Mungu kujua ni kuwapo” {Ndio na La, ukurasa 16}. Kwa hivyo yale binadamu anajua kuhusu Mungu inatengeneza uwepo na ufahamu wa binadamu inajumuisha kujua pekee kwa mawazo hayo sahihi ambayo ipo tayari katika Akili ya Mungu. Haiwezekani kisayansi kuweka wazo mbaya katika ufahamu, na hakuwezi kuwa na kutokamilika katika Akili kwa sababu yale Mungu anajua imekamilika na haiwezi ingiliwa na haiwezi badilishwa kwa njia yoyote. Hakuna kitu kilicho na uhai ila Mungu na kile Mungu anachokiumba, kwa hivyo kuna wazo sahihi ya kitu chochote. “Akili ya kimungu huhifadhi utambulisho wote, kutoka nyasi mpaka nyota, kama ya kipekee na ya milele” { Sayansi na Afya, ukurasa 70}

Imani ya kimwili katika juhudi zake za kuona kimwili huumba jicho la kibinadamu na kutangaza kuwa kiungo cha kuona, ila katika ukweli, kuona ni uwezo wa Akili, kikamilifu huru mbali na vipande vya jicho ikiwemo kiungo cha kuona. Wakati Yesu alisema ya kwamba “mwangaza wa mwili ni jicho,” hakuwa anarejelea jicho la kimwili lakini hali ya akili. Hivyo, yale Akili inajua kuhusu kitu tunachokiita macho ndio yote yaliyomo. Haya pia ni kweli kuhusu ile akili ya kimwili huita moyo, maini, mapafu na yale yote yanayo jumuisha uitwao mwili. Akili ya kimwili inadai ya lkwamba binadamu ni kimwili iliyopangwa, lakini imani za kimwili hazina dutu, na ukweli unabakia ya kwamba mpangilio ulioko pekee au utawai kuwa, ni ujumuisho wa wazo la kiroho ambao hiki kiumbe cha kimwili ni cha uongo. Kama vile kunaweza tu kuwa na wazo moja sahihi kuhusu kila kitu, kuna dhana moja sahihi kuhusu tumbo. Haijatengenezwa na undongo; sio kitu cha kimwili. Ni dhana ya akili, na kwa hivyo iko na mahali pake sahihi katika Akili ya Kimungu.Dhana ingine yoyote ya tumbo ni ya uongo na ya kupotosha na hatimaye lazima iharibiwe. “Kila kitu katika akili za kimwili lazima kiharibiwe. Lakini wazo la kiroho ambalo dutu yake iko katika Akili, ni ya milele” { Sayansi na Afya, ukurasa 267}.

Ni wakati Wanasayansi wa Kikristo waache kutibu viungo vilivyo gonjeka na kujitolea kubadilisha miundo isio kamilika kwa imani bora na zilizoimarishwa ambayo ni njia pekee ya uponyaji. Mungu ndiye sheria ya afya na uwiano kwa mawazo yake yote , na hii sio tu kweli, lakini sheria ya Mungu ambayo inatawala wazo lililokamilika la kiroho pia ndio sheria ya ukamilifu kwa imani ya binadamu ya vitu, na hii hutambaa kwa kila kiungo cha mwili wa binadamu. Chochote Mungu anajua kuhusu mkono, jicho, nyayo, ndiyo pekee kujua kuhusu yale. Anajua ya kwamba sio ya undongo, lakini ya kwamba imekamilika, iko na uwiano, na ni mawazo yaliyo na faida na kwamba utambulisho wake ni wa kipekee na wa milele. Kama mtu ako na dhana mbaya kuhusu mkono, jicho, nyayo, wokovu wake pekee ni kupata wazo sahihi kuhusu viungo hivi. Kama mwili wake ungeumia , ingekuwa dhana yake ya mwili ambayo imeathiriwa, sio ya Mungu, na dawa ni yeye kwa haraka kuachilia imani yake mbaya ya mwili na kujifahamisha na wazo la Mungu. “Jifahamishe na yeye sasa { Mungu}, na uwe na amani.”

Katika ukurasa 218 wa mkusanyiko wa maandishi, Mama Eddy anaandika: “Wala agano la kale au jipya linapatiana sababu au mifano ya uharibifu wa mwili wa binadamu, lakini kwa urekebishaji kwa uhai na afya kama udhibitisho wa kisayansi wa ‘Mungu Pamoja nasi.’ Nguvu haki ya kipekee ya ukweli ni ya kuharibu magonjwa yote na kufufua wafu – hata Lazaro. Mwili wa kiroho, wazo lisilo la kimwili, lilikuja na ufufuo.”

Hatuwezi kuwa na mwili mwingine ila ule wa wazo lisilo la mwili na lililo kamilika. Binadamu akiwa wazo lililo na vipengele vingi la Mungu, kwa kiasili hufuata yale yamejumuishwa katika ufahamu wa binadamu lazima iwe ya kiroho na kamilifu, au sio ufahamu ambao Mungu anajua na ambao binadamu anastahili kuwa nao. Udongo au kimwili hauwezi fanywa wa kiroho; lakini imani yetu iliyopotoka ambayo inajithihirisha kama kimwili inaweza rekebishwa na kwa hivyo kufanywa kiroho. Kuponya moyo usiyo kamilika, ambayo ni kwa urahisi imani mbaya kuhusu moyo, mtu lazima akatae ushahidi wa hisia za kimwili na kudai uwepo wa wazo la Mungu, ili kuboresha dhana yake mbaya. Sio muhimu ya kwamba anastahili ajue ni nini wazo la kimungu nyuma ya imani ya binadamu kuhusu moyo. Yale yote anatakiwa kujua ni kwamba hisia yake ya moyo iliyopotoka , ambayo inaonekana kuwa ya kimwili, sio sahihi. Kuna wazo sahihi la Mungu ambalo imani ya kibinadamu ya moyo ndio bandia, na wazo hilo la Mungu lipo sasa na hapa na hakuna linguine. Kama mwanaume ako na imani mbaya kuhusu tumbo, dawa pekee ni kutambua uongo wa yale yote akili za kimwili inasema kuhusu tumbo na kudai umuliki wa wazo la Mungu, ambalo ndio ukweli ulio kamilika.

Magonjwa yote ni juu ya imani mbaya kuhusu mambo, na dawa pekee ni kupata wazo sahihi. Kwa sababu kuna wazo sahihi la moyo na wazo sahihi la tumbo, tunaweza fahamu yale kiongozi wetu anamaanisha wakati anaposema, “ Sayansi ya Kimungu…inaondoa kimwili, inarekebisha vitu kuwa mawazo, na inabadilisha vitu za kimwili na mawazo ya kiroho” {Sayansi na afya, ukurasa 123}. Hakungekuwa na mawazo ya kiroho ambayo ni ya kugeuza vitu vya hisia ya kimwili, imani zetu zilizogonjeka hazingerekebishwa kamwe na miili yetu haungeponya kisayansi. Mungu hajajitenga na mawazo yake; wazo la kiroho la kila kitu lipo kila wakati na lipo na nguvu na utendaji wa Akili ya milele, na wakati wazo la kiroho linakutana na imani ya uongo, linatoa matokeo iliyo na uwiano.

Ni ukweli ya kwamba imani mbaya kuhusu mwili inajionyesha kama hali mbaya ya kimwili, kuliko wazo sahihi ambalo linarekebisha imani ile mbaya lazima itatoa onyesho lililoboreshwa la mwili. Hatuwezi ponya kwa kujaribu kufanyisha kazi nguvu ya Ukweli kwa mwili uliogonjeka. Ni zoezi la nguvu za Ukweli katika imani ya ugonjwa ambayo huleta matokeo ya uponyaji.

Sayansi ya Kikristo ni sayansi sahihi, na kwa hivyo haitarusu kupotoka kutoka kwa kanuni yake na sheria. Inadai ya kwamba mwanafunzi , ndio aweze kudhihirisha ukweli wake lazima aweze kutimiza matakwa yake. Yesu alisema, “ Utaujua ukweli na ukweli utakuweka huru.” Alafu ufahamu wa ukweli kuhusu yale Sayansi ya Kikristo inafundisha hakika ni muhimu kwa udhihirisho wake.

Sisi wote tunafanya kazi chini ya imani ya kwamba binadamu ni kiumbe kilichotenganishwa na muumbaji wake, akiwa na akili na maarifa yake . imani hii lazima iharibiwe, na njia pekee ya kufanikisha uharibifu wake ni kwa wakati wote kushikilia kwa mawazo sahihi na kutangaza uwepo na utendaji wa mawazo yote ya Mungu. Kama mawazo haya yanakuwa kweli zaidi kwetu, ijulikanayo kama akili ya kibinadamu itaondoka na tutajipata tukikuwa kama yeye. – zaidi kama hekima ya milele, zaidi kama Ukweli na Upendo. Alafu itakuja kupita kama ilivyoandikwa na nabii, “ Dunia itajaa ufahamu wa Bwana, kama vile maji inajaza bahari.”