Uovu hauna makazi maalum |

Uovu hauna makazi maalum

iliyoandikwa na DORIS WHITE EVANS


Katika Sayansi na Afya Mama Eddy anasema , “ Uovu hauna makazi maalum wala jina.” {ukurasa 537} Unaweza tumia kauli hii kwa hali yoyote ambayo inaweza tokea. Uovu umewasilisha picha kwetu sisi wote juu ya hali zisizokuwa na uwiano. Wakati unajaribiwa kuwekwa kwenye masikitiko, kumbuka, “Uovu hauna makazi maalum.” Uovu hauwezi kuishi mahali popote. Hauwezi ishi kwa nyumba ya mtu yeyote, na hauwezi jiita kwa jina la yeyote. “Uovu hauna makazi maalum.” Uovu hauna makazi kifuani cha yeyote. “Hakuna makazi maalum.” Hauna makazi katika tumbo ya yeyote, moyo, Kichwa, au kwa kiungo kingine chochote cha mwili; kwa mkono, mguu, au nyayo. “Uovu hauna makazi maalum.” Haya ni matibabu ya ajabu.

Uovu hauna jina, hauwezi jiita maumivu ya Kichwa, hauwezi jiita homa, hauwezi jiita saratani, hauwezi jiita hofu, ugonjwa, au matatizo. Hauwezi jiita upumbavu. Hakuna wanadamu wapumbavu katika ufalme wa Mungu. Hii kauli yenye ukweli na yenye nguvu inafuta madai ya uongo ya uovu. Nimeona kauli hii ikileta uponyaji katika kesi mingi.

Ni ukweli mkubwa. “Uovu hauna makazi maalum wala jina.” Kataa kupatia uovu jina, kataa kuupatia makazi. Uovu wakati wote ni kitu kimoja na jina lake ni bure. Ukiona uovu kwa njia ile, kama hakuna kitu, uovu hauwezi fanya kile ungetaka kufanya kwako. Uovu hauna uzuri wowote.

Sayansi na Afya inaendelea kusema, “Uovu unajiondoa kutoka kwa uwiano.” [ ukurasa 537} Uovu ni muongo. Hauwezi ishi katika ufahamu uliojaa ukweli. Unajitoa nje. Wakati wote ni muongo na utajiangamiza wenyewe, usipoaminiwa.

Na mwisho, Sayansi na Afya inatuambia ya kwamba, “Dhambi ndiyo adhabu yake yenyewe.” { ukurasa 537} Hatupaswi kumuadhibu mtu yeyote. Mtu akikosa kutii sheria ya upendo, atajiadhibu mwenyewe. Sheria ya haki ya kimungu inafanya kazi wakati wote. “ Uovu unajiondoa kutoka kwa uwiano.” Adhabu mara nyingi inakuja haraka na mara nyingi kwa ukali sana.

Yote yaliyopo katika kipendekezo chochote ambayo uovu wa kinyama inaweza onyesha ni bure! Wakati wote ni bure. Usiiamini. Sio lazima uwe nayo. Kwa nini? Kwa sababu Mungu hakuiumba, au kuiidhinisha . Mungu hakuipatia nguvu; kwa hivyo haina nguvu. Ni ajabu aje ya kwamba tunaweza tembea juu ya hali yoyote mbaya. Hatutakiwi kuzuiliwa ndani yake.

Kama, hata hivyo hatuko waaminifu kwetu wenyewe, au kwa wanadamu wenzetu, tunapatia uovu mahali pa kupumzika. Nafikiria sisi ni werevu sana kufanya vile. Wito wa kanisa la Plainfield ni: “Uaminifu ni nguvu ya kiroho.” {S&H ukurasa 453} Tudai nguvu hii. Tuishi nguvu hii. Tuwe waaminifu na Mungu. Kamwe usiende nyuma ya milango iliyofungwa katika fikira zako, au nyumbani mwako, na kipimo cha viwango viwili ambayo hungependa ndugu na dada kanisani waone. Usifanye kisingizio kwa uovu. Usiwe mzuri kwa uovu. Kama ni uovu, yote ni makosa. “Hakuna makazi maalum.” Haina makazi katika mawazo ya mtu mwenye akili sahihi.

Sayansi na Afya milele ni mpya. Unaweza pata kitu ndani yake kinacho kuhamasisha, na kuponya chochote kinachoweza kuwa kikijaribu kukusumbua. Fungua moyo wako kwa Mungu, na atakuonyesha mpango wake mkamilifu. Shukuru Mungu ya kwamba Sayansi ya Kikristo inaponya. Inafanya kazi. Inapanguza uovu wote, tukisimama kwa uaminifu na ukweli tuliousoma, na kuamini Upendo wa Mungu na utayari wake wa kututunza, sisi Watoto wake wapendwa.