Uponyaji wa taratibu
Na JUDGE JOHN D. WORKS
Nilipokuja ndani ya Sayansi ya Kikristo, nilikuwa mtu aliyevunjika, kiakili na kimaumbile.
Nikaomba usaidizi kutoka kwa mtendaji kwa nafuu ya kimaumbile pekee. Wakati niliomba usaidizi huu, nilikuwa kwenye hali ya kukosa matumaini, na karibu na kuwa na imani ya kutosha kuipa hukumu ya haki.
Nilikuwa naugua ugonjwa wa tumbo, ambao nilikuwa nao kwa miaka mingi. Ilikuwa inasababisha uchungu mwingi mchana na usiku, nilikuwa nimepoteza paundi thelathini, na nilikuwa naendesha shughuli zangu kwa shida kuu. Nilikuwa kwa shida kubwa.
Sayansi ya Kikristo ilinipa nafuu ya haraka. Ilinipa nafuu ya hali ya akili, ikapunguza uchungu na mateso na ikanijaza na imani. Uponyaji wenyewe ulikuwa wa taratibu. Nilitoka kwenye shimo la kukata tamaa, na kuingia kwenye hali ya baraka ya afya, imani na amani, polepole lakini kwa uhakika. Ilikuwa kama miezi nne kabla kusema nilikuwa nimeponywa kabisa, na mwaka moja kabla kurudiwa na nguvu kamili na uzito nilioupoteza. Lakini na shukuru kwa wakati wote kuwa uponyaji wangu ulikuwa wa pole. Ulinipatia wasia niliouhitaji sana, na motisha wa kusoma Sayansi ya Kikristo, ambayo nilifanya kwa hamu na bidii.
Katika wakati huu nilipata ufahamu bora wa Mungu na wema wake. Nilijawa na imani ndani yake ambayo ilikuwa ni ya halisi na ya dhati. Ufahamu ya kwamba Mungu ni usaidizi uliokaribu kwa wakati wote wa dhiki, Pamoja na uongo wa uovu ambao nimepata kwa kusoma Sayansi na Afya, imeniondolea hofu ambayo ilikuwa juu yangu kama ndoto mbaya.
Matumaini, amani, na kutosheka ambako kumekuja katika maisha yangu, kupitia mafundisho ya Mary Baker Eddy, katika Sayansi ya Kikristo, haiwezi kadiriwa au kulipwa, ila kupitia upendo wangu, shukrani na huduma aminifu.