Usiogope
Iliyoandikwa na A. L. Roth
Wakati mmoja Yesu aliwaagiza wafuasi wake wachukue mashua na waende Bethsaida. Jioni, wakati mashua ilikuwa katikati mwa bahari, upepo ulikuwa dhidi yao na wafuasi walikuwa wanapambana na maboya. Kuelekea asubuhi Yesu alienda kwao, akitembea juu ya maji. Wakati wafuasi walimuona Yesu akitembea juu ya bahari, walitaabika kwa sababu walifikiri ilikuwa ni mzimu. Lakini Yesu mara moja akatamka maneno ya kuhifadhi amani, ambayo yamekuwa kwa karne nyingi kufariji na kudumisha wanadamu, ” Kuwa na furaha: ni mimi; msiwe na hofu.”
Kwa mtu anayeteseka na magonjwa au kushinda dhambi, au aliechokeshwa na huzuni, Sayansi ya Kikristo inapatiana hakikisho lile lile la upendo na udhibitisho ya uhuru kutokana na hofu. Kwa mtu anayeteseka, kutishika kwa sababu ya utambuzi wa magonjwa yasiyokuwa na tiba au ugonjwa hatari, Sayansi ya Kikristo inaleta uwezo na ujasiri wa kustahimili, na kutarajia kupona kamili. Inaambia mwenye hofu na wasiwasi kuangalia mbali na giza na mambo mandogo ya ugonjwa , na kutazama mtu mkamilifu wa maumbile ya Mungu.
Mbinu ya kuponya magonjwa ya Mwanasayansi Mkristo inatangaza kuwa ulimwengu, ikiwemo binadamu,umeumbwa na Mungu. Katika uumbaji huu ambao ni kamili na umekamilika, hakuna kitu ambacho kinaweza ingia ambacho ni tofauti na Mungu, wema. Haijalishi ukali wa ugonjwa na maumivu, wala wasiwasi wala hofu inaweza sababisha kuwa na shaka kwa athari za hakika za uponyanji wa Ukweli. Mama Eddy anasema, ” Utendaji wa Sayansi ya Kikristo unaanzia na dokezo kuu ya uwiano, “Usiwe na hofu” {S&H}
Sayansi ya Kikristo inatupa ujasiri wa kushinda kila kitu ambacho ni tofauti na wema, na kuonyesha nguvu za Mungu. Kupitia imani iliyoangaza , kulingana na ufahamu wa roho, ya kwamba Mungu anatekeleza kusudi lake la Kimungu maishani mwetu, tunaweza pumzika kwa uhakika ya kwamba ni wema pekee unawezatujia, na kupata uponyaji na amani kwa wale wanaoweka imani yao kwa Mungu.