Vyote nilivyonavyo ni vyako |

Vyote nilivyonavyo ni vyako

Vyote nilivyonavyo ni vyako. Na Mabel W. Dunham


Sayansi ya Kikristo ilinijia wakati kila kitu kilionekana kukosa matumaini. Moja kwa moja, nilikuwa nimewapoteza watu kadhaa katika familia. Nilikuwa na deni kubwa, na nilikuwa na machungu na mwenye huzuni. Alafu siku moja nikakopeshwa Sayansi na Afya iliyoandikwa na Mama Eddy. Nikaenenda peke yangu nikiwa na uhakika ya kwamba huu ndio ujumbe niliokuwa nautafuta uhai wangu wote. Nilisoma kwa masaa kwa furaha kubwa ambayo mfungwa anaweza soma barua ya radhi kwa sababu kitabu hiki kilielezea Mungu kwa njia ambayo nilikuwa nimetaka kuamini. Niliendelea kusoma kila wakati ulipopatikana, na nikaanza kuona njia ya kuepuka shida zangu zote. Nikaanza kuhisi upendo mkuu kwa kila mtu, sanasana wale ambao walikuwa wamenikosea. Kwa kweli, kitu cha kwanza nilichokifanya ni kuwaandikia barua na kuwaambia ya kwamba niliwapenda na nimewasamehe.

Wiki kadha baadaye, nikapoteza sauti yangu. Daktari akanichunguza, na akaniambia sitapata matumizi sahihi ya sauti yangu kama sitafanyiwa upasuaji. Kwa ajili mimi ni mwalimu wa sauti, hii ilikuwa jambo nzito. Hata hivyo, nilijua Mungu angeniponya.

Kupitia matibabu moja kutoka kwa mtendaji wa Sayansi ya Kikristo, sio tu sauti yangu iliyorejeshwa, lakini pia kitu kizuri kilifanyika. Hasara yote na majonzi, ambayo yalikuwa yamenikumba kwa miaka mingi, yalitoweka. Sitawai sahau amani na uhakika ambao ulijaa mawazo yangu wakati mtendaji alinipatia maneno haya kutoka kwa Bibilia: “ Mwanangu, uko nami, na vyote nilivyonavyo ni vyako.” {Luka} Nilienda nikiwa na uhakika kabisa ya kwamba singepoteza kitu chochote ambacho kingebadilishwa na wema.

Sasa, kila siku yaleta wema zaidi, na nafasi kubwa zaidi. Nimepata amani na afya kupitia Upendo wa Mungu ambao unaonyeshwa katika Sayansi ya Kikristo.