Wale wote wamelelewa katika imani ya Ukristo |

Wale wote wamelelewa katika imani ya Ukristo

Kutoka kwa toleo la Novemba 1916 la jarida la Sayansi ya Kikristo na William D. McCrackan


Wale wote ambao wamelelewa katika imani ya Ukristo wanaweza kumbuka hadithi ya kutoroka kwa Maria kuelekea Misri. Wasanii wengi katika karne nyingi wameshawishiwa na msisimuko wa tukio hili na picha ya kisasa inayojulikana vema inawakilisha Maria kama amembeba mtoto Yesu mikononi mwake na kama anapumzika katika makucha za nondo, na kama Yusufu analala kwenye ardhi na nyota zinang’aa kwenye anga ya mashariki. Lakini ni nini kilimfanya mama wa kiyahudi kumpeleka mwanae Misri kwa usalama? Ingekuwa bora mahali kwingine kokote ila Misri kupata usalama kwa mtoto wa Israeli wa umri mdogo vile. Bado ilikuwa ni maelezo ya kimetafizikia ya kigezo hiki kilivyoonekana ambacho kiko na somo na himisho kwa wale wanaolenga njia ya kiroho.

Ukweli unaojulikana ambao ulielekeza Maria kutoroka hadi Misri ndio huu: wanaume wenye Hekima waliotoka mashariki walikuwa wamekuja Yerusalemu, wakisema, “Ako wapi aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi?” Haya yalimwamsha Herode na kabla kufanya mikakati ya kumgundua Yesu, ujumbe wa ajabu ukamjia Yusufu “ katika ndoto”: Amka na uchukue mtoto huyu mchanga na mama yake, na utorokee Mistri, na ukae pale mpaka nikuletee ujumbe; kwa ajili Herodi atamtafuta mtoto huyu mchanga ili kumuangamiza.”

Mwaandishi wa kitabu cha Sayansi ya Kikristo na ufunguo wa maandiko,’’ amefumbua kwa wanadamu maana kamili ya kuzaliwa kwa Yesu. Hakuna mwaandishi wa dini ashawai elezea mimba ya Yesu na maoni ya kiroho yenye nguvu na juhudi zenye upendo kama Mama Eddy, mfumbuzi na mwanzilishi wa Sayansi ya Kikristo. Katika ukurasa 29 wa kitabu chake tunapata maneno haya: “ Yesu alikuwa uzao wa umoja wa ushirikiano wa ufahamu wa Maria na Mungu;” na pia, Kristo aliishi milele kama wazo kifuani mwa Mungu, kanuni ya kimungu ya mtu Yesu, na mwanamke akaona wazo hili la kiroho, ingawa mwanzoni kwa kiasi kidogo,’’ ambalo Maria alikuwa analinda wakati alitorokea Mistri. Sasa, kila Mkristo mwenye Sayansi lazima awe tayari kuokoa maono yake ya Kristo kutokana na kushikwa na yule atakayekuwa mharibifu. Nani kati ya waliojitakasa katika Sayansi ya Kikristo hawajapata tajiriba ya wakati Herodi alikuwa anapapasa gizani ya uvutio ili kumuangamiza mtoto yule mchanga. Si wazo hili la kiroho , linapozaliwa katika ufahamu wa kibinadamu, ndio umiliki wa mali ya dhamana zaidi, na hakuna dhabihu yoyote duniani ambayo ni kuu ili kuhakikisha usalama wake mbali na kuadhirika.

Saa ya uchaguo saa zingine inafika bila kutarajiwa. Mkristo mwenye sayansi anaweza jipata katika mazingira starehe ya maada ambayo hukubalika kwa hisia za kusinzia za kutosheka kwa nafsi. Katika mazingira kama ile wazo la kiroho halikui na kupata nguvu, Labda mateso ya aina fulani yanajaribu kugandamiza wazo lile la kiroho, ndio lisiweze kuchukua mahali pake sahihi katika kiti cha enzi cha utakatifu katika ufalme wa ufahamu. Mbadala unapendekezwa saa zingine ambao utakubalika kwa kikamilifu kwa imani ya uongo na hautakasirisha hisia za kimwili. Tena kunaweza kuja wakati shughuli za dunia na mlio wake mkubwa wa kejeli zisizo kuwa na maana zifanye kupuuza kwa Kristo. Kwa kweli, utendaji wa kina ambao wema wa kibinadamu huwa , kiburi chaweza kuwa hafla ya kupuuza na kuachilia wazo la kiroho. Martha “ mwenye kina na kusumbuka juu ya mambo mingi” katika mashirika ya kanisa yaweza pooza uwepo wa Kristo ambaye huja kuokoa, kuponya na kufufua wafu. Kwa hivyo wakati chaguo linakaa muhimu kati ya Kristo na mateso ya Herodi, kusikuwe na kusita. Ili kuokoa ufahamu wa kiroho, saa zingine ni muhimu kutorokea Misri yenyewe hata kwa kiwango cha kuenda mahali popote, hali yoyote, mahali wazo la kiroho linaweza lindwa. Hakutakiwi kuwa na mda wa kungoja au kupoteza; Ushawishi wowote wa mazungumzo lazima ukataliwe. Kitu kimoja tu chahitajika juu ya Mkrito wa sayansi, kwa jina, kumiliki ufahamu wa Kikristo; kuwa na yale, wokovu umikononi, wagojwa wameponywa, waliona hofu wanafarijiwa, waliofungwa wanapata uhuru.

Kama saa itakuja ambapo wale wako na jina lakini hawajahifadhi ufahamu wa Kristo, watajaribu kutenganisha Mkristo mwanasayansi na Mwana wa Mungu, tusiache dhambi hii ya siri, iliyoundwa kuwahadaa walioteuliwa , kumdanganya. Atafuata kwa uaminifu wazo la kiroho, atailisha, ataithamini, ataizingatia, na kwa udhabiti kuitii. Wakati tumechagua kitu kile kimoja kinachohitajika, sehemu bora zaidi, Kristo, Ukweli, utatuongoza mbali na hatari, na kuvunja kila nira, kurahisisha kila mzigo, na kuangamiza kila tashwishi.

Alafu, wakati hatari imepita, wakati Herodi amekamilisha imani ya uharibifu alioishikilia juu ya wengine, Malaika au mjumbe mwingine atakuja “akisema, Amka, na umpeleke mtoto huyu mchanga na mama yake , na mwenende katika nchi ya Israeli: kwa ajili wamekufa waliotaka kuangamiza uhai wake mtoto.” Kuwa na uhakika kwamba hakuna kulipa kifungu cha kumi cha nanaa, na badyani na jira, inayohitajika na mtazamo wa wafarisayo, na hakuna wema wakibinadamu usiokuwa na muongozo, hakuna kulenga kwa shughuli za kibinafsi, sio kuepuka tu mambo yasiokubaliana, hakuna utelezi wa ulimi au makubaliano ya nje, ambayo yataokoa waliowagonjwa au kufufua wafu. Lakini Kristo ametosha kwa mambo yote. Kupitia ripoti njema na mbaya, mwana sayansi ya Kikristo anasoma kulinda maono yake ya Kristo na asiogope Misri, kwa kuwa kwa ukweli hata giza inayoonekana inaweza badilishwa kuwa makazi ya mda ya usalama na ufahamu wa “Mungu pamoja nasi.’’