Wito wa Maombi
na Benjamin Franklin
Wakati baada ya wawakilishi waliokuwa wamekutana mwakani 1787 kuandika Katiba ya Marekani waling’ang’ana kwa wiki kadha wakipata ufanisi mdogo au kutofanikiwa, Benjamin Franklin mwenye miaka themanini na moja alihutubia kongamano lile lililokuwa limesumbuka na lililokuwa karibu kusitisha mkutano kwa kuchanganyikiwa . Ilionekana kama jitihada zao za kuunda umoja wa kudumu hazikufaulu.
Benjamin Franklin alisema, “ Mwanzoni mwa mashindano na Uingereza , wakati tulihisi hatari, tulikuwa na maombi ya kila siku kwenye chumba hiki ili kupata ulinzi wa Mungu. Maombi yetu bwana, yalisikiwa na kujibiwa kwa rehema. Sisi wote tuliohusika katika mapambano ilikuwa ni lazima tumeona matukio mara kwa mara ya uangalizi wa Mungu kwa faida yetu….na sasa tumemsahau huyu rafiki mwenye nguvu? Au tunafikiria hatuhitaji tena usaidizi wake?”
“Nimeishi, bwana, mda mrefu, na kadri ninavyoendelea kuishi, kadri ndio naendelea kupata Ushahidi wa kuaminika zaidi wa ukweli huu: ‘ya kwamba Mungu hutawala kwa shughuli za mwanadamu.’ Na kama njiwa hawezi anguka chini bila yeye kujua, kuna uwezekano himaya inaweza inuka bila usaidizi wake? Tumehakikishiwa, bwana, katika maandiko matakatifu ya kwamba ghairi Bwana ajenge nyumba, wanafanya kazi ya bure wanaoijenga, ninaamini haya kwa nguvu.
“Pia naamini ya kwamba bila usaidizi wake, hatutafanikiwa kwa jengo hili la kisiasa kama wajenzi wa Babeli; tutagawanyika kulingana na matakwa yetu ndogo ya mitaa; miradi yetu itatatanishwa; na sisi wenyewe tutakuwa aibu na hadithi kwa vizazi vijazo. Na ni gani mbaya zaidi, wanadamu wanaweza baadaye, kutokana na tukio hili mbaya , kukata tamaa ya kuimarisha serikali ya hekima ya mwanadamu na kuiacha kwa kibahatisho, vita au ushindi. Kwa hivyo nawasihi kukata kauli kwamba, kutoka sasa, maombi ya kuitisha usaidizi wa Mbinguni na baraka zake kwa majadiliano yetu yafanyiwe katika mkutano huu kila asubuhi kabla hatujaendelea na shughuli.”
Alafu Benjamin Franklin akapendekeza ya kwamba kongresi iairishe kwa siku mbili kutafuta muongozo wa Kimungu. Waliporudi, walianza kila kikao chao kwa maombi. Hotuba ya kusisimua ya Benjamin Franklin iliashiria mwanzo mpya katika uadishi wa Katiba, kamilifu ikiwa na Katiba ya haki.