Wote wanstahili upendo wa Mungu |

Wote wanstahili upendo wa Mungu

Iliyoandikwa na FLORENCE ROBERTS


Niashukuru sana kusoma kupitia Sayansi ya Kikristo ya kwamba ninastahili, na kila mtu mwingine pia , tunastahili Upendo wa Mungu kama haki ya kuzaliwa ,na kwamba hii inanipatia utawala wa kukataa hofu yangu. Bila kusoma huku nilibaki kwa urahisi nemoogopa na mapendekezo yoyote ya uongo ambayo hisia za uongo zilitwika njiani mwangu. Kwa urahisi inachosa kuishi kwa hofu. Kwangu inaifanya haramu, na sio sehemu ya haki yetu ya kuzaliwa. Nilisoma hata wakati magoti yangu yanatetemeka lazima nijue Mungu ni uwepo wa usaidizi wa milele na hataniacha. Hii inaleta faraja. Kuna vifungu vingi katika Bibilia zinazo tukumbusha kama “Bwana ni mchunganji wangu sitahitaji kitu chochote.” Zaburi 23

Napenda yale Mama Eddy anaandika katika kutazama nyuma na kujichambua; ukurasa 61, “ Sayansi inasema kwa hofu, “wewe ndio sababu ya magonjwa yote; lakini wewe ni uongo wa kujitengeneza, – wewe ni giza, pasipo na kitu, hauna matumaini, na bila Mungu katika dunia.” Haupo, na hauna haki ya kuwepo, kwa kuwa “Upendo uliokamilika unaondoa hofu.” Mungu yupo kila mahali. Hakuna hotuba wala lugha, ambapo sauti yao haisikiki,” na hii sauti ni Ukweli ambao unaharibu uovu na Upendo unaoondoa hofu.”

Nashukuru sana kwa masomo haya kwa sababu kila mara ni hofu ambayo tunatakiwa kuondoa ili kuishi kama Baba Mama yetu anataka tuishi kama wana wake Mungu. Ninamshukuru Mungu, Kristo Yesu, Mary Baker Eddy, na wale wote wanaodhihirisha hii Sayansi, kusaidia kuwaamsha wengine kwa huu Ukweli ambao unamfanya mwandamu huru.