Yote niliyo nayo ni yako
Na Elma S. Whitmore
Je, mtoto mmoja wa Mungu anaweza kuwa na baraka zaidi kuliko mwingine? Je Mungu, Upendo wa Kimungu anamimina ufanisi, afya, na utu wema juu ya mtu mmoja au taifa na kuwapa kiasi kidogo wengine? Katika Bibilia tunapata uhakikisho dhabiti wa ugavi usio egemea upande mmoja kwa kila mwana wa Mungu katika maneno haya, “ Mwanangu, uko nami kila wakati, na yote niliyo nayo ni yako.” Sheria hii iliyo na upendo na ya ulimwengu, ikielezewa katika mithali ya mwana mpotevu, ilipatiwa sauti na babake wakati kakake mkubwa alilalamika juu ya mapokezi ya raha, na zawadi nyingi alizotunukiwa mwana yule mpotevu aliyerudi, ilhali hakuna furaha aliyo onyeshwa juu ya uaminifu na utiifu wake.
Ni nini zaidi baba yao angewapa wana wake ila kile alichokuwa nacho! Na ilikuwa inapatikana kila wakati kwa nduguye mkubwa aliyebaki nyumbani, na pia kwa aliyepotea ambaye alikuwa ameondoka na akarudi.
Kauli hii rahisi ya sheria ya Mungu ya wema ni ahadi kwa wanadamu wote. Yote Mungu aliyo nayo ni ya mwanadamu, na kwa ajili Mungu ni wa milele, chanzo kilichokamilika, urithi wa binadamu hauwezi kuwa haujakamilika, au ukikosa. Urithi wake hauwezi pungukia kuliko wema. Mungu habadiliki, kwa hivyo binadamu hawezi badilika. Hakuna kitu chochote kinachoweza kusumbua sheria hii iliyoimarishwa ya wema na utendaji wake mkamilifu.
Mama Eddy, kwa kuelezea umoja wa binadamu na muumbaji wake, anaandika katika Sayansi na afya, ya kwamba binadamu “ huakisi kwa kiroho yote ambayo ni ya muumbaji wake.”
Tukiendelea kudai urithi wetu uliokamilika kama wana wa Mungu, tutafahamu kwa wazi kuwa utoaji wa Mungu kwa wana wake upo kila wakati, kwa wingi, bila mapendeleo, na bila kuisha.